Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewataka watumishi wake kuyafanyia kazi mafunzo ya kiutumishi waliyopata ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na ubora wa huduma katika maeneo yao ya kazi.

Wito huo umetolewa na Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia Huduma za Shirika, Aidan Makalla, wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano yaliyofanyika jijini Dodoma, yaliyolenga kuwajengea watumishi uelewa kuhusu utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uhifadhi, huduma kwa wateja na nidhamu mahali pa kazi.

Makalla amesema Mamlaka imewekeza kwa watumishi hao kwa kuwapatia mafunzo yanayohusu utumishi, maadili, uwekezaji, afya ya akili na itifaki, kwa kuamini kuwa elimu ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na utendaji wenye tija.

“Sisi viongozi wa Mamlaka ni kama wazazi, tuna wajibu wa kuwapa mafunzo ili msiharibikiwe na baadaye Mamlaka ikaja kulaumiwa. Yatumieni mafunzo haya kujijenga katika kazi zenu,” alisema Makalla.

Mafunzo hayo ni awamu ya pili kwa mwaka huu wa fedha, ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo watumishi wake, kwa kuzingatia msemo wa Kiswahili unaosema, “Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.”













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...