Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson John Simon, amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya hiyo, Mhe. Fadhil Nkurlu, aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushika nafasi hiyo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo, Oktoba 2, 2026, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zilizopo wilayani humo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Simon, ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe mkoani Songwe, amesema anaondoka Kibaha akiwa ameacha kumbukumbu nzuri, ikiwemo kusimamia kwa karibu shughuli za ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini.
Amesema pamoja na kuondoka Kibaha kiutendaji na kiutumishi, moyo wake utaendelea kuwa na upendo mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo, ambao amesema walimpokea, wakamlea na kumpa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote alichohudumu.
“Naondoka Kibaha kiutendaji na kiutumishi, lakini moyo wangu umejaa upendo mkubwa kwa wana Kibaha ambao walinipokea, kunilea na kunifundisha. Kwa hakika, watu hawa watabaki kuwa sehemu muhimu ya historia ya maisha yangu,” amesema Mhe. Simon.
Kwa upande wake, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Fadhil Nkurlu, amesema mafanikio ya Wilaya hiyo yatahitaji ushirikiano wa viongozi wote pamoja na wananchi, akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuharakisha maendeleo.
Mhe. Nkurlu amesema atahakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaendelea kusimamiwa ipasavyo, huku akisisitiza umuhimu wa viongozi wote kufanya kazi kwa umoja.
Amesema maono yake ni kuendeleza kazi nzuri zilizoachwa na Mkuu wa Wilaya aliyemtangulia, huku akiahidi kushirikiana na viongozi wa Serikali, chama, madiwani na watendaji wa Halmashauri zote mbili za Kibaha.
“Jambo kubwa ni kuendelea kushirikiana kwa lengo moja la kuleta maendeleo. Tutaendelea pale alipoishia Mkuu wa Wilaya aliyepita na tunatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama na watendaji wa Halmashauri zote mbili,” amesema Mhe. Nkurlu.
Naye Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Mhe. Aziza Mruma, amemkaribisha Mkuu huyo mpya wa Wilaya na kumuahidi ushirikiano kutoka kwa Baraza la Madiwani katika kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ya Manispaa ya Kibaha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...