Jane Mwakyoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 mkoani Rukwa.
Maadhimisho hayo yatafanyika Oktoba 14, 2026 katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na maendeleo ya vijana Joel Nanauka akizungumza katika kikao na wanahabari kilichofanyika mjini Sumbawanga leo ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa vijana,ajira na uwekezaji Zanzibar Ali Suleiman Ameir .
Alifafanua kuwa maadhimisho ya kilele hicho yanaenda sambamba na kuzimwa rasmi kwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao uliwashwa Zanzibar Aprili 04 mwaka huu na Rais na Mwenyekiti wa Mapinduzi ya Nzanzibar Ali Hassan Mwinyi ambapo umekumbizwa katika Halmashauri 195 zilizopo katika mikoa 31 Bara na Visiwani.
Aliongeza kuwa kuelekea maadhimisho hayo Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda kwa niaba ya Waziri Mwigulu Nchemba akifungua wiki ya Vijana Kitaifa Oktoba 10 mwaka huu ambayo ilianza rasmi Oktoba 08 katika Uwanja wa Ndua mjini hapa na itahitimishwa 0ktoba 14.
Aidha maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Kitaifa kitaendana na ibada takatifu ya kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere itakayo fanyikana katika kanisa Katoliki la mtakatifu Epifani saa 12:00 asubuhi mjini Sumbawanga.
Aidha Nanauka amewaalika wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...