Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imesema eneo maalum la uwekezaji linaloendelezwa Zinga, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, litafungua fursa kubwa za kiuchumi na ajira, hususan kwa vijana.

Mradi huo unatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 9,800, huku awamu ya kwanza ikilenga kuendeleza maeneo ya kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa kongani za viwanda na teknolojia.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo linaloendelezwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema TISEZA inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji pamoja na kuweka miundombinu muhimu itakayowezesha shughuli za uzalishaji.

Nyongo amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Pwani kushirikiana na TISEZA katika kuwaandaa vijana ili wawe tayari kunufaika na fursa zitakazotokana na uwekezaji huo.

Amesema maandalizi hayo yanapaswa kuhusisha kuwawezesha vijana kushiriki katika fursa mbalimbali, ikiwemo kutambua na kunufaika na asilimia 10 ya fursa zinazotengwa kwa ajili ya makundi hayo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi wa TISEZA, Anna Lyimo, amesema vijana wanapaswa kujiandaa mapema ili kuchangamkia fursa za ajira zitakazotokana na uwekezaji katika eneo hilo.

Amesema fursa hizo zitapatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo uzalishaji, ufundi na uendeshaji wa viwanda.

Lyimo amesema jumla ya viwanda 150 vinatarajiwa kuendelezwa katika eneo hilo, huku viwanda 25 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Amesema kukamilika kwa viwanda hivyo kutachochea shughuli za kiuchumi na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa Bagamoyo na maeneo mengine ya Mkoa wa Pwani.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...