Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka viongozi wa Mkoa huo kuimarisha uwajibikaji, weledi na ubunifu katika utendaji wao ili kuboresha huduma za umma na kuhakikisha changamoto za wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Ametoa agizo hilo Oktoba 8, 2026, wakati akiongoza kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Sekretarieti ya Mkoa katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mhe. Senyamule amesema viongozi wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia dhamana waliyopewa na Serikali, kusimamia watumishi walio chini yao na kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinaendana na misingi ya utawala bora, huku wakilinda amani na utulivu katika maeneo yao.
Amesisitiza pia umuhimu wa viongozi kuwa karibu na wananchi kwa kuwasikiliza, kuwahudumia kwa upendo na kuhakikisha kila anayefika katika ofisi za umma anapokelewa vizuri na kupata msaada unaostahili.
“Wananchi wanahitaji kuona tabasamu kutoka kwa viongozi wao, jambo linaloashiria upendo, ukaribu na utayari wa kuwahudumia,” amesema Mhe. Senyamule.
Aidha, amewahimiza viongozi kutumia ubunifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kubuni njia mpya za kutatua changamoto za wananchi, kuharakisha shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Akizungumzia vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma, amewataka viongozi kuelekeza nguvu katika sekta za elimu, afya, mazingira, uchumi, kilimo, viwanda na madini ili kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.
Amesisitiza kuwa mafanikio ya uongozi yanapaswa kuonekana kupitia matokeo ya kazi zinazofanyika, ubora wa huduma zinazotolewa na mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi, akiwataka viongozi kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yao unaleta manufaa yanayoonekana kwa jamii.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...