šŸ“ŒAzindua Kitabu cha mwongozo wa bei za keki kwa waokaji nchini;

šŸ“ŒAsema sekta ya uoakaji ina ajiri  wajasiriamali wengi kwenye soko la ajira

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga (Mb), amezindua kitabu cha mwongozo wa upangaji bei za keki kilichoandaliwa na mjasiriamali wa ndani, Tahya, maarufu Leymax, huku akimpongeza kwa mchango wake katika kuwawezesha wajasiriamali nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kapinga alisema vijana wengi, hususan wanawake na wanaume, wamepata elimu na ujuzi wa ujasiriamali kupitia mafunzo yanayotolewa na Leymax, ikiwemo ujuzi wa utengenezaji wa keki.

“Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na wajasiriamali wadogo na wa kati hapa nchini na tunaahidi kuendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa waokaji,” alisema Kapinga.

Alisema mchango wa wajasiriamali katika kukuza uchumi ni muhimu, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha fursa za biashara na uzalishaji zinaimarishwa.

Kwa upande wake, Tahya alimshukuru Waziri Kapinga kwa kuitikia mwaliko wa kushiriki katika uzinduzi wa kitabu hicho, akisema kitakuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya uokaji na kuwawezesha waokaji kupanga bei zao kwa kuzingatia gharama halisi za uzalishaji.

Alisema mwongozo huo unalenga kuwasaidia wajasiriamali katika kufanya mahesabu sahihi ya gharama za kutengeneza keki na kupanga bei zinazoweza kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa tija na faida.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...