Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Lindi, kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mwenge, Manispaa ya Lindi, limefanya zoezi la kusafisha mitaro ya maji katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo, ikiwa ni hatua ya kujiandaa na kukabiliana na mvua za El-Nino.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Theodory Hall, amesema zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, huku shirika hilo likikabidhi mashine mbili aina ya Moha kwa ajili ya kusaidia shughuli za usafi katika kata hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Juma, amewashukuru TANESCO kwa kushirikiana na Halmashauri katika kuimarisha usafi na maandalizi ya kukabiliana na mvua za El-Nino, akisema Halmashauri imefikia utayari wa asilimia 95.

Baadhi ya wananchi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Mwenge, Ali Kanjoro, wamesema usafishaji wa mitaro hiyo utasaidia kupunguza athari za mafuriko pamoja na magonjwa ya mlipuko wakati wa msimu wa mvua.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...