Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL)limekabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhamisisha usafi.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na TTCL vimekabidhiwa leo Oktoba 10,2026 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliyekuwq ameambatana na Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya bada ya kufanyika kwa shughuli ya kufanya usafi katika maeneo ya Posta ambapo pia watumishi wa TTCL wameshiriki kufanya usafi huo.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo ametoa Shukrani kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania CPA. Moremi Marwa kwa dhamira yao ya kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kufanya usafi katika Jiji hilo.

“Kwa niaba ya Serikali nitoe shukrani kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na wafanyakazi wote kwa kuona umuhimu wa kushiriki katika kutekeleza maelekezo ya Rais wetu npendwa Dk.Samia Suluhu Hassan aliyeelekeza tufanye usafi katika Jiji letu la Dar es Salaam.

“Tunawashukuru TTCL kwa kazi kubwa ambayo mmeendelea kuifanya nchini Tanzania lakini kwa kazi kubwa ambayo mmeendelea kuifanya kwa Jiji letu la Dar es Salaam .Leo hii TTCL

mnatamba kila mahala.Leo hii mmeamua kuwika na kutamba katika eneo la usafi,tunawashukuru na tunawapongeza.”

Amesisitiza suala la usafi ni muhimu katika eneo na Taifa lolote kwani ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na TTCL wameona kuna kila sababu ya kushirikiana na Jiji la Dar es Salaam kwa vitendo .

“Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na kwa niaba ya Serikali tunawashukuru TTCL kwa vifaa mlivyotoa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za usafi katika Jiji la Dar es Salaam, mmetupa vifaa vingi ikiwemo mabuti ,vifaa vya kuhifafhi taka ,fagia.Thamani ambayo sisi tunaiona sio fedha iliyopitishwa kununua vifaa hivi bali ni dhamira ya TTCL kuona Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi.

“Umuhimu wa usafi katika maendeleo ya Taifa lolote ninyi TTCL tunawaona katika thamani hiyo ,vifaa hivi ambavyo mmetukabidhi maana yake kuna watu mmewakinga kupata magonjwa ya kipindi hiki ambacho tunakwenda kwenye matur iko kwa kuhakikisha tunaondoa uchafu katika mitaro.”

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa taasisi zote zinazounga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuitaka Tanzania kuwa safi na salama kwani dhamira ya Rais Samia ya kutaka Jiji la Dar es es Salaam kuwa safi na salama.

“Tuwaombe wale ambao bado wanachechemea njooni tushirikiane mkongo wa Taifa wa TTC

umeshika hatamu. rai kwa mashirika na taasisi nyingine kushiriki kikamilifu katika kufanya usafi wa mazingira kwani haipendezi kuona mbele ya taasisi au Shirika la umma mazingira ni mchafu lakini walioko wala hawachukui hatua kusafisha maeneo yao.

Wakati huo huo Mpogolo ametoa shukrani kwa niaba ya Serikali kwa wote walioshiriki kufanya usafi wakiongozwa na wenyeviti wa Serikali za mitaa ,madiwani na maofisa afya kwa kushiriki kufanya usafi katika mitaa yote 159.

Awali Wakati akikabidhi vifaa vya usafi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL ,Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika hilo Mhandisi Cecil Francis amesema wanampomgeza jitihada za kuunga mkono maelekezo kutoka kwa Rais na viongozi wote ambao katika kipindi hiki wanahimiza usafi kama utamaduni lakini kama kinga dhidi ya janga ambalo linaweza kutokea kama mvua kubwa itanyesha.

“Mungu ametupa maarifa kwamba kuna hatari inakuja hivyo kama tusipofanya usafi kwa ajili ya kuzibua mitaro maji yapite vizuri tunaweza kutengeza janga jingine. Hivyo tunawapongeza Jiji la Dar es Salaam kwa kuchukua jitihada hizo na katika kuunga mkono TTCL tumeshiriki kufanya usafi na tutaendelea na kubwa zaidi tumeamua kuchangia vifaa na kusisitiza Shirika letu litaendelea kutoa huduma bora za mawasiliano.”
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...