Uchimbaji wa madini kwa kubahatisha umeelezwa kuwa miongoni mwa sababu zinazowafanya wachimbaji wadogo kutumia muda, nguvu na fedha nyingi bila uhakika wa kufikia miamba yenye madini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Geoffrey Wiliam Mkurugenzi wa Kampuni za Amogtech Mine Services,One4s Geomi na Afrex, amesema matumizi ya teknolojia katika utafiti wa madini yanaweza kusaidia kubaini maeneo yenye uwezekano wa kuwa na miamba yenye madini kabla ya kuanza uchimbaji.
Mwaselela amesema kampuni hizo hutumia wataalamu na vifaa kufanya uchunguzi wa maeneo ya uchimbaji, ikiwemo geophysical survey, unaosaidia kubaini mwelekeo wa miamba chini ya ardhi na kumpa mchimbaji taarifa za kitaalamu za kuongoza uchimbaji.
Amesema hatua hiyo inaweza kupunguza uwezekano wa wachimbaji kutumia fedha na muda mwingi katika maeneo yasiyo na uhakika wa kupata madini.
Amesema wachimbaji wadogo wanaweza pia kushirikiana kugawana gharama za huduma za utafiti, hasa pale ambapo wataalamu wanatakiwa kusafiri kutoka maeneo mengine, huku akisisitiza umuhimu wa kuachana na utegemezi wa imani za kishirikina na uchimbaji wa kubahatisha na badala yake kutumia taarifa za kisayansi katika kufanya maamuzi ya uchimbaji.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Migodi na Meneja wa Uendeshaji wa Kampuni hizo Bi. Martha Mwakajaba, amesema huduma za utafiti wa madini si lazima zitolewe na kampuni za nje pekee, kwa kuwa Tanzania ina kampuni za kizawa zenye wataalamu waliobobea.
Amesema upatikanaji wa wataalamu hao ndani ya nchi unatoa fursa kwa wachimbaji wadogo kupata huduma za kitaalamu kwa gharama nafuu na kufanya maamuzi ya uchimbaji kwa kuzingatia taarifa za kisayansi.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...