Zaidi ya vijana 400 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya madini muhimu (critical minerals) yanayotarajiwa kuanza kutolewa na Chuo cha VETA Shinyanga kuanzia mwaka ujao, katika hatua ya kuwaandaa kupata ujuzi unaohitajika katika teknolojia mpya za sekta ya madini.
Akizungumza katika Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Theophan Pantaleo Severine, amesema mpango huo utalenga kuwajengea vijana ujuzi unaoendana na mahitaji yanayojitokeza katika sekta ya madini.
Amesema mafunzo hayo yatazingatia teknolojia zinazohusiana na uchimbaji na uongezaji thamani wa madini muhimu, pamoja na ujuzi mwingine unaohitajika katika shughuli za sekta hiyo.
Aidha, amesema VETA Shinyanga itaendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa vijana na wadau waliopo katika maeneo ya uchimbaji, ikiwemo teknolojia ya uchimbaji, uongezaji thamani wa madini ghafi na ufundi wa mitambo.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha vijana kupata ujuzi utakaowasaidia katika kupata ajira, kujiajiri na kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa nchini.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...