Na.Ashura Mohamed - Arusha


Benki ya CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 4.3 kwenye mazao ya horticulture ikiwa ndiyo mdhamini mkuu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa na Mazao ya Bustani, HortiLogistica Africa 2026.

Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inachagiza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo haswa mazao ya horticulture ambapo katika sekta kilimo fedha zilizotolewa zinafikiwa asilimia 45 ya uwezekezaji na mikopo yote ambayo inatolewa na taasisi za fedha hapa nchini.

Akizungumza kando ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Jijini Arusha, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara kutoka Benki ya CRDB, Bw. Maregesi Shaabani, alisema benki hiyo imeamua kuwekeza kwa nguvu katika kilimo kwa sababu ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.

"Kupitia mikopo hii ya trilioni 4.3, tunawawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kupata pembejeo bora, teknolojia ya kisasa na mitaji ya kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao yao," alisema Shaabani.

Aliongeza kuwa benki hiyo imeweka mifumo ya kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika baada ya kuvuna, kupitia Mkataba wa Pande Tatu unaosainiwa kati ya mkulima, benki na mnunuzi.

"Kwa leo tumejumuika na wadau mbali mbali wakulima wawekezaji kwenye mnyororo wa thamani wa horticulture lakini pia wanunuzi wetu katika mazao yetu ya kilimo bila kusahau wadau muhimu serikalini wakiwemo wizara ya kilimo,wizara ya mifugo na uvuvi,wizara ya uchumi wa bluu kutoka kule zanzibar,wizara ya kilimo zanzibar ambapo serikali imeweka nguvu kubwa kuhakikisha kuwa taasisi binafsi kama CRDB zinashirikiana na wadau katika kuendeleza guridumu la Uwekezaji katika sekta ya kilimo"Alisisitiza Shaaban

Aidha alisema kuwa CRDB kama mdhamini mkuu imeona mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya kilimo ikiwemo uchakataji mazao na uzalishaji wa kisasa ikiwa ni pamoja na vifungashio tofauti na awali ambapo imejipanga kuendelea kuwekeza zaidi ili kuhakikisha kuwa uchumi wa wakulima unakua na nchi pia inapata mapato makubwa.

Alisema kuwa benki hiyo ipo ndani ya Afrika na benki ya kikanda hivyo kutokana na hali hiyo wamejipanga kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya kutosha kwa wawekezaji kwa kuwa ubora wa benki hiyo umewezesha kupata idhibati ya mfuko wa umoja wa mataifa unaongalia uwekezaji himilivu,rafiki kwa mazingira mfuko wa Global Climate Fundi (GCF), ambapo ilipata dola za marekani milioni 200 ambazo zimewekezwa kwenye mazao ya chakula.

Maonyesho ya HortiLogistica Africa 2026 yamewakutanisha wadau kutoka nchi zaidi ya 40, kwa lengo la kuunganisha wazalishaji wa mazao ya bustani na soko la kimataifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...