Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amekabidhi viwanja 340 vya makazi kwa wahanga wa mafuriko katika Kata ya Tindiga, katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Malui.
Akizungumza katika hafla hiyo, Shaka amebainisha kuwa pamoja na viwanja hivyo vya makazi, Serikali pia imetenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii katika eneo hilo lililotengwa kwa ajili ya wahanga hao.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha wahanga hao wanapata makazi salama na mazingira bora ya kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
"Baada ya mafuriko, Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alimtuma Mhe. Waziri Mkuu Mwigulu kuja kutoa pole kwa wahanga na alihakikisha huduma zote za kibinadamu zinapatikana. Lakini Mhe. Rais Samia alielekeza kutafutwa maeneo ya Serikali ili tuwahamishe mabondeni kule. Leo maelekezo ya Rais Dkt. Samia yametimia, tuko hapa kuyatekeleza kwa vitendo." Alisema Shaka
Hata hivyo, Shaka amewataka waliopokea viwanja hivyo kuvitumia kwa ajili ya makazi kama ilivyokusudiwa, akisisitiza kuwa hawaruhusiwi kuviuza viwanja hivyo.
Katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya amekabidhi Hati za Umiliki wa viwanja hivyo kwa wahanga hao, na kuongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini ili kuwabaini wahanga wengine wenye uhitaji ili nao waweze kupatiwa viwanja.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...