Jiji la Dodoma limetakiwa kuimarisha maandalizi ya ardhi, mifumo ya kiutawala na taratibu za utoaji wa huduma ili kuwezesha wawekezaji kupata maeneo na kuanza utekelezaji wa miradi katika ujenzi wa mji wa kisasa wa Hombolo.
Wito huo umetolewa Novemba 9, 2026, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba kati ya Jiji la Dodoma na kampuni ya kimataifa ya usanifu majengo na mipango miji ya Heerim Architects and Planners, kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mpango kabambe wa mji huo.
Senyamule amesema maandalizi yanapaswa kuanza mapema ili kuhakikisha maombi ya wawekezaji wanaohitaji maeneo yanashughulikiwa kwa haraka, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa timu maalumu itakayoratibu changamoto na kusimamia hatua mbalimbali za mradi.
Amesema matarajio ni kuona mradi huo ukitekelezwa kwa vitendo na kuleta mabadiliko yanayoonekana kupitia majengo na miundombinu, badala ya kubaki katika mipango ya maandishi, huku akisisitiza utekelezaji wake kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amesema hakuna mpango wa sasa wa kutenga ardhi kwa matumizi mengine yanayoweza kuathiri maandalizi ya mradi huo, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wataalamu wa ardhi katika kupanga matumizi ya eneo hilo.
Amehimiza wananchi na wadau wa maendeleo ya ardhi kufuata taratibu zilizowekwa na kutumia fursa zitakazojitokeza kupitia mradi huo kwa manufaa yao na kukuza uchumi.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko, amesema ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha mradi huo, ambao unatarajiwa kuchangia kuipa Dodoma taswira mpya ya mji wa kisasa.
Mwenyekiti wa Heerim Architects and Planners, Young-in Jung, amesema mpango huo unalenga kuendeleza mji wa kisasa, kijani na janja (Smart City), utakaokuwa na huduma na miundombinu ikiwemo viwanja vya ndege, vituo vya mikutano, hoteli, maeneo ya makazi na biashara, amesema hatua ya awali itahusisha upembuzi yakinifu na maandalizi ya mpango kabambe wa matumizi ya ardhi utakaoweka msingi wa utekelezaji.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...