Waswahili husema Mchumia janga hula na wa kwao wakimaanisha unaweza sababisha hatari ya jambo kutokea na kudhuru wengine; Ndivyo ilivyo hatari ya kuwa karibu na faru ukiwa katika Hifadhi ya Ngorongoro hasa Kasoko ya Ngorongoro (Ngorongoro Crater) ambapo wanyama hao wamekuwa wakionekana kwa wingi na ukaribu usiozidi meter 150.

Wageni mamia kwa maelfu  wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro ambayo ni urithi wa dunia huwa na mshawasha au shauku ya kuwasogelea faru hasa kwa karibu wakiongozwa na waongoza watalii.

Jambo hili kisheria halikubaliki na kumsogelea Faru kwa ukaribu zaidi inapobainika  utapigwa faini kwani unaweza kusababisha usumbufu kwa mnyama, kumpa msongo wa mawazo na kusababisha maafa kwa wageni ambao wapo kwenye chombo cha usafiri hasa kutokana na tabia za faru za kutopenda usumbufu, bughdha au kelele

Faru hasa F aru Mweusi akiwa amekasirika anaweza kupindua gari na kusababisha kuua wageni wote ndani ya gari na ndiyo maana imekuwa ikisisitizwa kwamba unapokuwa ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ni muhimu kufuata sheria na taratibu za uhifadhi.

Kitabia Faru ni miongoni mwa Wanyama wakali, wanahitaji eneo kubwa la malisho (home range), muda mwingi wa mchana anautumia kupumzika katika eneo ambalo ni tulivu lisilokuwa na wanyama wengi wasumbufu na mara nyingi kila eneo analopita huweka alama maalum ambazo kwake zinaashiria eneo la utawala.

Faru hapendi Kelele au sauti zenye usumbufu mithili ya Kariakoo au Mbagala na ndiyo maana akisikia kelele husimama kwa uangalifu na kusikilizia harufu na sauti inapotoka, akigundua ulipo hapo ndipo mwisho wa maisha yako na msemo wa Mchumia  janga hula na wa kwao huwa umetimia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...