Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amehitimisha safari yake ya udaktari wa falsafa baada ya kufaulu katika hatua ya mwisho ya masomo yake kwa kufanya utetezi wa mwisho (Viva Voce) kwenye jopo la wasomi na jumuiya ya wadau mbalimbali waliohudhuria tukio hilo kwenye makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tarehe 6 Novemba, 2026.
Chini ya usimamizi wa Profesa Deus Ngaruko na Dkt.Harrieth Mtae Kamishna Badru* alifanya utetezi wa shahada yake ya uzamivu katika mada iliyobeba kichwa cha habari Socio-economics Determinants of Housing Affordability for Public Servants in Tanzania:Case of Rent-paying house holds in Dar essalaam .
Baada ya utetezi na mahojiano ya zaidi ya saa tatu jopo la wasomi lilifanya hitimisho kwa kusema, "Abdul-Razaq Badru umefaulu udaktari wako wa falsafa”,(PhD).
Kamishna Badru atahudhurishwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria yatakayofanyika hivi karibuni na hivyo kuanza rasmi safari ya udaktari wa falsafa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...