Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Waziri Rajab Salum, ameielekeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kuimarisha usimamizi wa utoaji wa Leseni za biashara kundi A ili kulinda fursa za kiuchumi zilizotengwa kwa Watanzania.

Hayo ameyazungumza leo Novemba 12,2026 jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika ofisi ya BRELA kwa lengo la kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa taasisi hiyo.

“Naielekeza BRELA, kuhakikisha wageni hawapati Leseni za biashara kundi A ambazo kwa mujibu wa katazo la Serikali Na.487A la mwaka 2025 kuhusu biashara zilizopigwa marufuku kufanywa na wasio raia wa Tanzania na kwa Leseni zilizotolewa awali kabla ya katazo hilo pindi zitakapo kwisha muda wake hampaswi kuzihuisha tena”, amesema.

Aidha Balozi Salum amewataka vijana wabunifu wenye mawazo na bidhaa bunifu wanazipa ulinzi wa Miliki Ubunifu sambamba na kuwahamasisha wafanyabiashara wadogo kusajili biashara zao.

Na kuongeza kuwa, kampuni zenye changamoto hasa zenye migogoro ya hisa zinapaswa kutembelea ofisi za BRELA ili kusaidiwa na kupata suluhu ya changamoto zao.

Sambamba na hilo, ameielekeza BRELA kuandaa kliniki maalumu ya kuwahudumia wasanii ili kuwapa huduma ya kusajili na kulinda bunifu zao ili waweze kunufaika, na kuepusha kuibiwa bunifu hizo zitakazopelekea kuwa na migogoro.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw.Godfrey Nyaisa, amemueleza Katibu Mkuu Mhe.Balozi Salum kuwa, Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 BRELA imeendelea kuwezesha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi na wadau wa biashara.

Katika kipindi hicho, BRELA imesajili Kampuni 5,811 sawa na asilimia 96, Majina ya biashara 11,044 sawa na asilimia 109, Leseni za Biashara kundi A 8,171 zimetolewa sawa na asilimia 69, vyeti vya usajili wa viwanda tisa (9) sawa na asilimia 47, pamoja na Leseni za Viwanda 283 sawa na asilimia 163 zimetolewa.

Aidha, Wakala amesajili Alama za Biashara na Huduma 1,075 sawa na asilimia 96, huku maombi ya Hataza yakiwa ni 95 sawa na asilimia 396 yamepokelewa. Mafanikio haya yanaonesha juhudi za BRELA katika kuimarisha utoaji wa huduma na kuwezesha ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini.” Alisema Nyaisa.

Ziara ya Katibu Mkuu Viwanda na Biashara katika ofisi za BRELA imelenga kujionea shughuli na huduma zinazotolewa na BRELA na kutathmini utekelezaji wa majukumu yake. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...