Na Victor Masangu, Kibaha
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha inatarajia kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani kupitia uboreshaji wa mradi wa maegesho ya malori katika eneo la Misugusugu, kwa kuweka huduma mbalimbali za kijamii zitakazowanufaisha watumiaji wa eneo hilo.
Mradi huo unatarajiwa kuwa mkombozi katika kupunguza changamoto ya malori kuegeshwa kiholela pembezoni mwa barabara, hali inayoweza kusababisha usumbufu na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Warda Maulid, wakati akijibu maswali ya madiwani katika kikao cha baraza la madiwani kilichojadili utekelezaji wa shughuli za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 (Julai–Septemba).
Maulid amesema halmashauri imejipanga kuweka huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo, hatua itakayosaidia kuboresha mazingira ya maegesho na kuongeza mapato ya ndani kupitia huduma zitakazotolewa.
Amesema ameyapokea maoni na mapendekezo ya madiwani na kwamba halmashauri itaweka mipango ya muda mfupi na mrefu kuhakikisha mradi huo unakuwa na manufaa zaidi.
Awali, Diwani wa Kata ya Misugusugu, Ally Simba, aliomba eneo hilo liboreshwe kwa kuweka huduma mbalimbali za kijamii pembezoni mwa maegesho ili kuongeza ufanisi wake.
Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu, Sara Uledi, amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha malori yanayoegeshwa kiholela barabarani yanaondolewa na kuelekezwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili hiyo.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas, amelipongeza baraza la madiwani kwa ushirikiano na kumkaribisha Mkurugenzi huyo mpya, akiahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya halmashauri.
Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Emanuel Nkurlu, amewataka viongozi wa chama na Serikali kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa, bila kuingiliana katika maeneo ya kiutendaji.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Amiri Nyamka, amesisitiza umuhimu wa uzalendo, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa madiwani ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...