Ujumbe wa Mabalozi na Naibu Mabalozi 11 wanaowakilisha Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake nchini Tanzania utafanya ziara ya siku tatu mkoani Tanga kuanzia tarehe 23 hadi 25 Novemba 2026.
Ziara hiyo italenga kuangalia fursa zilizopo mkoani humo za kukuza uchumi kwa njia endelevu, pamoja na namna ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania unavyoweza kusaidia kufungua fursa mpya kwa wananchi na wafanyabiashara. Ushirikiano huo unajumuisha pia mpango wa Umoja wa Ulaya wa Global Gateway.
Katika ziara hiyo, Mabalozi watakutana na viongozi wa serikali, wananchi wanaonufaika na miradi mbalimbali, wajasiriamali na wawakilishi wa sekta binafsi. Mikutano hiyo itawapa nafasi ya kujionea shughuli na miradi inayoendelea, kusikiliza uzoefu wa wananchi na kuelewa vipaumbele vya maendeleo vya Mkoa wa Tanga.
Ujumbe huo unajumuisha wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Slovakia, Hispania na Sweden.

Ziara hii ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake kutembelea kwa pamoja mikoa mbalimbali ya Tanzania. Mwaka jana, Mabalozi hao walitembelea Mkoa wa Kilimanjaro.
Mabalozi Watakaoshiriki Katika Ziara:
Umoja wa Ulaya: Jean-Marc Pisani – Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania (Kiongozi wa Ujumbe)
Ubelgiji: Lot Debruyne – Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania
Denmark: Jesper Kammersgaard – Balozi wa Denmark nchini Tanzania
Finland: Anna Merrifield – Balozi wa Finland nchini Tanzania
Ujerumani: Maximilian Mueller – Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania
Ireland: Nicola Brennan – Balozi wa Ireland nchini Tanzania
Italia: Giuseppe Coppola – Balozi wa Italia nchini Tanzania
Uholanzi: Marjo Crompvoets – Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania
Slovakia: Lancaric Ivan – Balozi wa Slovakia nchini Tanzania
Hispania: Paloma Serra – Balozi wa Hispania nchini Tanzania
Sweden: Sandra Diesel – Naibu Balozi wa Sweden nchini Tanzania

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...