. Asisitiza busara na utu, akipendekeza mwekezaji kuridhia kumega ekari 100 kwaajili ya Kitongoji cha Zaburi chenye usajili na miundombinu ya Msikiti, Kanisa, Maji, Umeme na chekechea
. Eneo lingine la Ekari 100 lenye makazi ya kudumu nje ya Eneo la Ekari 100 ya miundombinu ya jamii, Mwekezaji kukaa na wavamizi na kukubaliana
- Awataka wananchi kuwa watulivu, kusitisha uvamizi na uendelezaji wa eneo hilo mpaka kukamilika kwa makubaliano
- Baada ya makubaliano aitaka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kupanga maeneo yatakayoachwa na Mwekezaji
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, leo Ijumaa, Novemba 6, 2026, ametatua mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Makuyuni, Wilaya ya Monduli, uliodumu kwa takribani miaka 20 baada ya wananchi kuvamia eneo la mwekezaji la ekari 200 na kufanya shughuli za uzalishaji na kuweka makazi.Akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Zaburi, Mhe. Makalla amebainisha kuwa kampuni ya Rhino Equipment & Transportation ndiyo mmiliki halali wa eneo hilo, huku Serikali ikipendekeza mwekezaji huyo aridhie kutenga ekari 100 kwa ajili ya kitongoji hicho ambacho tayari kimesajiliwa na kina miundombinu mbalimbali ya kijamii ikiwemo msikiti, kanisa, shule ya awali pamoja na huduma za maji na umeme.
Katika maelekezo yake, Mhe. Makalla ameutaka uongozi wa Rhino Equipment & Transportation kukaa na kuzungumza na wananchi walioingia katika eneo lake lingine lenye ukubwa wa ekari 100 na kuweka makazi na kufanya shughuli mbalimbali ili kwa pamoja waweze kufikia makubaliano yatakayowezesha matumizi sahihi ya ardhi hiyo na kuondoa mgogoro.
Mhe. Makalla kadhalika amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuwa watulivu na kusitisha uvamizi na uendelezaji wa maeneo hayo hadi pale makubaliano yote yatakapokamilika suala ambalo limeungwa mkono na Uongozi wa eneo hilo, huku akiiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo na kuhakikisha kunakuwa na mpango mzuri wa matumizi ya ardhi itakayotengwa na mwekezaji kwa ajili ya wananchi hao.





.jpeg)





.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...