Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, ameonya baadhi ya vijana wanaopata ajira na vibarua viwandani kuacha vitendo vya udokozi na wizi wa mali za wawekezaji, akiwataka kuwa waadilifu ili kulinda uaminifu na kuvutia uwekezaji mkoani humo.
Aidha, amewataka wawekezaji kuhakikisha wanalipa wafanyakazi stahiki zao kwa mujibu wa taratibu na sheria za kazi, badala ya kuwakandamiza kwa kuwanyima haki zao, hali inayoweza kuwachochea kuingia katika tamaa na vitendo visivyo vya uadilifu.
Nyongo alitoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda cha Everwell Cable & Engineering Co. Ltd, kilichopo wilayani Mkuranga, kinachozalisha vifaa vya umeme, ambapo alielezwa miongoni mwa changamoto zinazokikabili ni udokozi wa baadhi ya malighafi, umeme kutokuwa wa uhakika pamoja na miundombinu mibovu ya barabara.
Alilitaka Jeshi la Polisi kuwafuatilia na kuwakamata wote wanaotajwa kuhusika na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria na iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kuharibu mali za wawekezaji.
"Serikali inafanya jitihada za kuhamasisha na kushawishi wawekezaji kuwekeza nchini kwa kuwa uwekezaji unasaidia kuongeza pato la Taifa na kutoa fursa za ajira, Isitokee mnapata bahati ya ajira kisha mnazichezea kwa kukosa uadilifu na kufanya wizi," alifafanua Nyongo.
Kuhusu changamoto ya barabara, Nyongo alizitaka taasisi zinazohusika kuhakikisha zinasimamia utatuzi wake ili kiwanda hicho pamoja na jamii inayokizunguka viweze kuondokana na adha hiyo.
Alisema kiwanda hicho kina umuhimu katika sekta ya nishati nchini kwa kuzalisha nguzo na nyaya zinazotumiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwemo katika mkakati wa kubadilisha nguzo chakavu.
Katika ziara hiyo, Nyongo pia alitembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kinachounganisha Mkuranga na Chalinze unaogharimu Sh bilioni 135 na kutekelezwa na mkandarasi kutoka China, ambao unatarajiwa kupunguza changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa viwanda na wananchi.
Kwa mujibu wa Meneja wa kiwanda hicho, Zilal Chen, kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 2015 na kinazalisha bidhaa mbalimbali za umeme, zikiwemo nyaya za aina tofauti, transfoma, nguzo za zege na vifaa vya kuunganishia umeme kwa matumizi ya majumbani na miradi mikubwa ya nishati.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...