▪️︎ Asema hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya ubadhirifu
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaendelea kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya ubadhirifu.
Amesema hayo leo (Ijumaa, Novemba 6, 2026), wakati akiwasilisha hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Bunge la 13, Bungeni jijini Dodoma.
Dkt. Mwigulu amewakumbusha Maafisa Masuuli na watendaji wote wa Serikali kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma kwa mujibu wa mipango na bajeti, ili kuepusha hoja za ukaguzi na upotevu wa fedha.
“Niwakumbushe watumishi wote kuwa fedha za umma ni kodi za wananchi, na hivyo Serikali haitafumbia macho wale watakaobainika kufanya ubadhirifu,” amesema.
Amesema Serikali itazingatia mapendekezo yote yaliyotolewa na Bunge kupitia maazimio na hoja zilizowasilishwa, pamoja na kufanyia kazi matokeo ya taarifa za ukaguzi.
Vilevile, amelipongeza Bunge kwa kuchambua kwa kina hoja za ukaguzi kuhusu matumizi ya fedha za umma na kutoa maazimio ambayo ni maelekezo mahususi kwa Serikali.
Amesema Wabunge wamechangia kwa hisia kubwa, wakionesha namna walivyo na uchungu na rasilimali za Taifa.
“Wabunge katika Bunge lako Tukufu wanawawakilisha vyema wananchi wa Tanzania, hususan katika usimamizi wa rasilimali na kuisimamia Serikali,” amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amezitaka wizara na taasisi zote kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, tarehe 30 Oktoba, 2026.
Amempongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua hiyo, akisema tarehe hiyo itabaki kuwa ya kihistoria kwa Taifa.
Dkt. Mwigulu ameelekeza shughuli za Serikali kufanyika Dodoma, Makao Makuu ya nchi, na kuacha kuendesha ofisi sambamba jijini Dodoma na Dar es Salaam kwa kuwa majengo ya ofisi yamekamilika.
“Kwa kuwa ofisi zimeshakamilika, tuache kuendesha ofisi sambamba, ofisi za Dodoma na ofisi za Dar es Salaam. Makao Makuu ya nchi yetu ni Dodoma,” amesema.
Vilevile, amezitaka wizara na taasisi kutumia majengo ya Mji wa Serikali na kuacha kuendelea kutumia majengo ya kukodi.
Aidha, ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa kushirikiana na wadau wa usafirishaji, kuhakikisha usafiri wa umma unapatikana kwenda Mji wa Serikali ili kuwawezesha wananchi kufika kupata huduma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...