Na Victor Masangu, Pwani

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh milioni 29 zilizokuwa mikononi mwa wakusanyaji wa ushuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, kinyume na taratibu za ukusanyaji na uwekaji wa mapato ya Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Ezekia Sinkala, amesema fedha hizo zilikusanywa kupitia mfumo wa mashine za POS lakini hazikuwekwa benki kama inavyotakiwa.

Amesema TAKUKURU iliingilia kati baada ya kufuatilia utaratibu wa ukusanyaji na uwekaji wa mapato katika akaunti ya Imprest na kubaini fedha hizo zikiwa bado mikononi mwa wakusanyaji.

Katika hatua nyingine, TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeokoa Sh milioni moja zilizotolewa na wananchi wa Kijiji cha Nyamwage, Wilaya ya Rufiji, kwa ajili ya kumpatia mtumishi wa RUWASA ili kuwaunganishia huduma ya maji kinyemela.

Pia, taasisi hiyo imeokoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh laki nane vilivyokuwa vimeelekezwa kinyume na matumizi yaliyokusudiwa katika mradi wa ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Shikizi ya Nyamitumba, katika Kituo Maalumu cha Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji.

Aidha, katika kipindi hicho, TAKUKURU imefanikiwa kutoa elimu kuhusu masuala ya rushwa kwa wananchi zaidi ya 27,000 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.

TAKUKURU imewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo, ikiwemo kujitokeza mahakamani kutoa ushahidi katika kesi za makosa ya rushwa zinazoendelea kusikilizwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...