●Mkakati ni kuongeza viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani madini.

●Lengo ifikapo mwaka 2030 utafiti wa kina kufikia asilimia 50.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufungua milango ya uwekezaji katika Sekta ya Madini kwa lengo la kuongeza uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani madini ikiwemo ujengaji wa viwanda vya kusafisha dhahabu na uongezaji thamani wa madini.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 18, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One.

Dkt.Kiruswa amesema kuwa, sekta ya madini ina wigo mpana katika nyanja za kiuchumi kuanzia uchimbaji , usafishaji, uchenjuaji, usafirishaji na uuzaji, wigo ambao unahusisha sekta mbalimbali katika uwekezaji.

Akielezea kuhusu fursa zilizopo katika mkutano wa TMIC 2026, Dkt.Kiruswa ameeleza kwamba, fursa zitakazojitokeza ni pamoja na kubadilishana teknolojia ya uchimbaji, utafiti, uchenjuaji na uongezaji thamani madini.

Aidha, kwa upande wa vijana waliopo katika mnyororo mzima wa thamani madini watapata fursa ya kuongeza maarifa na kubadilishana uzoefu katika upatikanaji wa mikopo na kuongeza mtandao wa mawasiliano kwenye nyanja ya uwekezaji.

Kwa upande wa utafiti wa madini , Dkt.Kiruswa amesema makakati wa serikali ni kugundua maeneo mapya yenye rasilimali madini ili kufikia asilimia 50 za utafiti ifikapo mwaka 2030.

Kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika mnyororo wa madini , Dkt.Kiruswa amebainisha kuwa watanzania wanaendelea kujihusisha kwenye sekta ya madini kila siku ambapo mpaka sasa zaidi watanzania 19,000 wanajihusisha na biashara ya madini katika maeneo mbalimbali ya nchi ambapo zaidi ya leseni 64,000 zimetolewa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...