TAASISI ya Tanzania House of Talent (THT) imeendesha kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza jamii kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira.

Akizungumza katika kikao na watumishi hao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri, Mratibu wa Mradi wa Pika Smart, Denari Ruhumbika, amesema majiko janja yanayotumia umeme yana gharama nafuu za uendeshaji, yakitumia kati ya unit 0.5 hadi 1 ya umeme kwa saa moja, huku yakiwa na uwezo wa kupika kwa ufanisi mara mbili ya majiko ya gesi.

Amesema matumizi ya teknolojia hiyo ni sehemu ya mabadiliko yanayolenga kuboresha maisha ya kaya, kulinda mazingira na kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi, hususan kuni na mkaa.

Kwa upande wake, Balozi wa Kampeni ya Pika Smart, msanii wa muziki Mrisho Mpoto, amesema kampeni hiyo ni hatua muhimu katika kuunga mkono malengo ya Taifa ya kuimarisha afya za wananchi na kuongeza kasi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Peter Ngussa, ameiomba THT kufikisha salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa Halmashauri hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi, ikiwemo matumizi ya gesi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Mafinga Technical.

Kampeni ya Pika Smart ilizinduliwa Juni 2025 kwa ushirikiano na Wizara ya Nishati pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, ikiwa na lengo la kuhamasisha Watanzania kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati safi ya kupikia.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...