Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha
WAHITIMU wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wametakiwa kutafakari na kujiwekea mikakati ya namna ya kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata chuoni hapo katika kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha juu na shindani.
Wito huo umetolewa Novemba 12, 2026 na mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC), Profesa Mussa Chacha alipokuwa akitoa hotuba katika mahafali ya 18 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.
Profesa Chacha amewataka wahitimu hao wa ngazi mbalimbali za uhandishi kwa viwango vya Stashahada na Shahada kutambua kuwa elimu na ujuzi walioupata ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda, kukuza teknolojia na kuongeza uzalishaji nchini.
Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inahitaji nguvu kazi yenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uzoefu katika sekta mbalimbali, hivyo wahitimu wa elimu ya ufundi wana nafasi muhimu katika kufanikisha malengo hayo.
“Mnatakiwa kutambua kuwa kuhitimu si mwisho wa kujifunza, bali ni mwanzo wa safari ya kutumia maarifa katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi, lakini pia napenda kuishukuru Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan , wadau wa maendeleo, wazazi, walezi na washirika wa chuo kwa mchango wao katika kuendeleza elimu ya ufundi nchini.l,” amesema.
Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Fredrick Salukile, Kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prf.Carolyne Nombo amesema wahitimu hao wanatakiwa kuunganisha elimu ya ufundi na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda.
Dkt. Salukile amesema maendeleo ya taifa hayaishii katika kujenga miundombinu pekee, bali yanahitaji pia wataalamu wenye uwezo wa kuendesha, kuhudumia na kutengeneza mifumo na vifaa mbalimbali, akisisitiza kuwa teknolojia, ubunifu na ujuzi ni msingi muhimu wa kujenga uchumi imara.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa vijana wenye ujuzi katika sekta za uzalishaji na ndiyo maana imeendelea kuimarisha elimu ya ufundi, huku akizitaka kampuni, viwanda na taasisi mbalimbali kutoa nafasi kwa wahitimu ili wapate uzoefu wa kazi na kutumia maarifa yao katika mazingira halisi ya uzalishaji.
Aidha Dkt Salukile, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kituo cha Uhandisi wa Vifaa Tiba (Biomedical Engineering) kwa ajili ya mafunzo, tafiti, ubunifu na matengenezo ya vifaa tiba, huku akieleza kuwa chuo hicho kufanya ushirikiano na vyuo na taasisi za kimataifa ikiwemo Cornell University, Clemson University na vyuo vikuu vya Korea Kusini ni fursa ya kuongeza uwezo wa wataalamu wa ndani.
Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Dkt. Noel Mbonde, amesema chuo hicho kinaendelea kuimarisha mafunzo yanayozingatia ujuzi wa vitendo, sayansi, teknolojia, nishati endelevu na ujasiriamali ili kuandaa wahitimu watakaokidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa.
Dkt. Mbonde amesema bodi inatambua mchango wa wadau wa maendeleo na taasisi za kimataifa katika kuimarisha uwezo wa chuo, akitaja ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na UNESCO Global Skills Academy kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha elimu ya ufundi.
Amesema ushirikiano huo unapaswa kuzaa matokeo yanayoonekana katika viwanda, taasisi na maeneo mbalimbali ya uzalishaji badala ya kuishia katika maonesho na makubaliano, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya mafanikio ya mafunzo na matumizi ya teknolojia zinazozalishwa.
Aidha, ameeleza kuwa chuo kinaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mafunzo na uzalishaji wa mashine, ambapo vifaa na mashine kutoka Austria vinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa Novemba 2026 na kuanza kufungwa mara baada ya kufika ili kuwawezesha wanafunzi kupata mafunzo katika mazingira halisi ya viwanda.
Amewapongeza wahitimu kwa kufikia hatua hiyo na kuwataka kuendelea kuongeza maarifa, kuwa wabunifu na kutumia ujuzi wao kujiajiri na kuajiriwa, huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri wa chuo kwa kuonesha nidhamu, uadilifu na umahiri katika maeneo yao ya kazi.
Katika mahafali hayo ya 18, jumla ya wahitimu 1337 wametajwa kuhitimu katika ngazi mbalimbali za mafunzo ya ufundi katika kozi za uhandisi wa mitambo, uzalishaji wa umeme, petroli na gesi, ujenzi wa barabara, majengo.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...