TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 28, 2026, imekutana na mtaalam wa uchunguzi wa patholojia Dkt Ahmed Mattaka pamoja na mtaalam wa vilipuzi Inspekta Raphael Maira.

Mkutano huo wa Tume na wataalam hao umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo kulingana na utaalam wao.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ikiwa na lengo la kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.







-Tume Ya Madini Yaeleza Mzabuni Kuendesha Minada ya Kimataifa Amepatikana

-Wazalishaji wa Chumvi Lindi kicheko, Februari Kiwanda kuanza Kazi


Na Wizara ya Madini Dodoma.

 Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba ameongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kupitia na kujadili hatua za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa Bungeni na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Hotuba yake kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara ya Madini pamoja na kuweka mikakati ya kutekelezwa, ilipanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali; kuongeza mchango wa Sekta kwenye Pato la Taifa; kuhamasisha uwekezaji na uongezaji thamani madini; kuimarisha uendelezaji minada na maonesho ya madini ya vito, kuongeza uwekezaji kwenye tafiti zake za kina; kuwarasimisha wachimbaji wadogo na kuzijengea uwezo taasisi zake.

Akizungumza katika kikao hicho, Eng. Samamba amesisitiza kutekelezwa kikamilifu kwa ahadi zilizotolewa na Wizara ili kuendelea kuongeza tija kwa taifa kupitia rasilimali madini.

Naye, Katibu Mtendaji Tume ya Madini Eng. Ramadhan Lwamo amesema tayari mzabuni atakayesimamia minada ya kimataifa ya Madini ya vito amekwishapatikana. Kufanyika

kwa minada ya kimataifa ya Madini ya vito  pamoja na mambo mengine kutaongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kupitia fedha za kigeni, kuitangaza Tanzania  na madini yake yanayopatikana nchini, kuvutia uwekezaji zaidi, kuimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa kupitia minada hiyo ya madini ya vito, kuwepo kwa bei halisi ya soko, uwazi na kuongeza washiriki wa ndani na kimataifa. 

Manufaa mengine ni pamoja na kukuza  wachimbaji wa ndani,  masoko ya uhakika ya madini ya vito na bei za uhakika.  

Pamoja na masuala mbalimbali yaliyojadiliwa, taarifa ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imeeleza kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kiwanda cha kusafisha chumvi katika Mkoa wa Lindi ambapo imeeleza kwamba matarajio ni kuwa ifikapo mwezi Februari, 2026 kiwanda hicho kitaanza kazi na hivyo kuondoa changamoto ya soko kwa wazalishaji wa chumvi.







 


📍 Njedengwa, Dodoma, 

Serikali imekabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi bilioni 23.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji , huku Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ikipongezwa kwa kazi kubwa inayofanya kuhakikisha sekta ya Umwagiliaji inakuwa nguzo ya uchumi wa taifa. 

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na mitambo mikubwa 19 ya kuchimba visima vyenye uwezo wa kufikia urefu wa mita 300 hadi 1800, magari 17 ya kubeba vifaa na malighafi, trela 2 na pikipiki 23.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, alisema hatua hiyo itaongeza chachu katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji kote nchini. 

“Serikali iliongeza bajeti ya maendeleo kutoka shilingi bilioni 46.5 mwaka 2021/22 hadi shilingi bilioni 308.7 mwaka 2025/26.

 Wizara itaendelea kusimamia na kufuatilia upatikanaji wa fedha ili ikamilike kwa wakati,” alisema, huku akiielekeza Bodi ya Uongozi ya NIRC na watumishi wa NIRC kusimamia vizuri rasilimali hizo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, alisema hafla hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Agosti 8, 2022

“Leo tunashuhudia jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukabidhi mitambo mikubwa ya visima 19, magari 16 ya kusaidia uchimbaji, trela 2 na pikipiki 23.

 Tume imepanga kuchimba visima 67,000 ndani ya miaka 5, vitakavyohudumia hekta 16,000. Katika mwaka huu wa fedha pekee, visima 1,027 vimepangwa kuchimbwa na tayari visima 260 vimeshachimbwa kwa majaribio katika mikoa 12,” Ameeleza.

Mndolwa aliongeza kuwa Tume imenunua pampu 1,000 kwa ajili ya kutoa maji ziwani, ambazo zitagawiwa kwa makundi maalum ya wanawake na vijana.Tume inaendelea na utekelezaji wa miradi 146 ya Umwagiliaji , ambapo miradi 18 imekamilika na ipo tayari kukabidhiwa.

“Watumishi wa Tume wako tayari na tumejipanga kuongeza eneo linalomwagiliwa ili kufikia malengo ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030,” Amesisitiza .

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema asilimia 72 ya wananchi wa mkoa huo wanategemea kilimo, hivyo ujio wa vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa ya kiuchumi. 

“Rais alishasisitiza kuwa shida siyo ukame bali ni maarifa ya namna ya kukabiliana na changamoto hiyo. Dodoma imejipanga kuwa mkoa wa kimkakati katika uzalishaji wa alizeti na kupitia umwagiliaji wananchi wanaweza kulima hadi mara tatu kwa mwaka,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mariam Ditopile, pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga, walipongeza Serikali na Rais Samia kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji

“Tume inafanya kazi nzuri, visima vinaendelea kuchimbwa na miradi mikubwa ya umwagiliaji inatekelezwa,” amesema Ditopile. 

“Rais ametekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na sasa Dodoma inakuwa mfano wa mapinduzi ya kilimo cha umwagiliaji.” Ameongeza Mbaga.









Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid,leo tarehe 28 Januari, 2026, amekutana na Katibu wa Pili - Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini,Bw. Jack Fenwick.

Bw. Jack amefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano.





-Zaidi ya Kaya 5,600 kunufaika

Wananchi wa vitongoji vya Msokole na Funguni Kijiji cha Mnazi Kata ya Nalingu Mkoani Mtwara wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi wa Umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao wamesema unakwenda kubadili maisha yao.

Wametoa shukrani hizo kwa nyakati tofauti Januari 28, 2026 wakati wa kumtambulisha Mkandarasi atakayetekeleza mradi wa Kusambaza Umeme mkoani humo Kampuni ya DIEYNEM Co Ltd.

“Tunaishukuru Serikali, hatimaye nasi tumefikiwa na mradi ambao utaimarisha shughuli zetu za uvuvi, umeme utatuwezesha kuhifadhi mazao ya uvuvi tofauti na ilivyo sasa kwani inatulazimu kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hii,” amesema Issa Mohamed Mkazi wa Kitongoji cha Msokole.

Mjasiriamali Kitongoji cha Funguni, Himid Ramadhan amesema kuwa umeme ni fursa na kwamba kufika kwa mradi kutamuwezesha kupanua biashara yake na kuanza kuuza vinywaji baridi lakini pia vijana wengine kitongojini hapo wataweza kubuni miradi ya kuwaongezea vipato ikiwemo biashara ya saluni.

Kwa upande wake Fadhila Hassan Mkazi wa Kitongoji cha Msokole amesema umeme unakwenda kuwakwamua kimaisha kwani kwa sasa biashara na shughuli nyingi za kijamii zinahitaji umeme na ameipongeza Serikali kwa mradi.

Awali akimtambulisha Mkandarasi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, Meneja Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme wa REA, Mhandisi Deogratius Nagu alisema REA inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 15,369,843,407.29 wa kusambaza umeme katika vitongoji 175 utakaonufaisha kaya 5,646 mkoani humo.

Pia Mha. Nagu alisema mradi utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu na ameiomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kushirikiana na REA kufikisha elimu na taarifa sahihi kwa wananchi, ushirikiano kwenye ulinzi na usalama wa vifaa vya Mradi sambamba na kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme hasa ikizingatiwa kuwa umeme ni fursa ya kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe.Kanali Patrick Sawala alimemsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anafanya kazi kwa kuwashirikisha viongozi katika ngazi mbalimbali ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

“REA mnatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo, ninawapongeza kwa hili ila ninawasisitiza mnapofika kwenye maeneo ya miradi jitambulisheni viongozi na wananchi wa maeneo husika wawatambue na mtafanikiwa kuepuka migogoro isiyo ya lazima na pia ulinzi na usalama utakuwa mikononi mwao kwakuwa mmewashirikisha,” amesisitiza Mkuu wa Mkoa Kanali Sawala.

Naye Meneja Miradi wa Mkandarasi, Mha. Novatus Lyimo amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa mradi utatekelezwa kwa ufanisi na utakamilika kwa wakati na kwamba watafanya kazi kwa ukaribu na wananchi na kwamba watatoa ajira zisizo za kitaalam kwa wananchi wa maeneo ya mradi.









Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro.

Tofauti na vijana wa mjini hasa wa Dar es Salaam ambao wengi wao hutahiriwa wakiwa wadogo hospitalini tena kwa ganzi, tohara kwa vijana wa kimasai hufanyika wakiwa mabarobaro na mashabaro na tena bila ganzi na hivyo kusikia maumivu makali ya kitendo hicho.

Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeungana naye kwa kupanda miti aina ya Olorien katika kijiji cha Oloirobi Wilayani Ngorongoro.

Miti hiyo hukatwa na hutumika mara baada ya vijana wa kimasai kufanyiwa Jando/kutahiriwa, kijana akishatahiriwa miti huo huwekwa mlangoni wa nyumba yenye kijana aliyetahiriwa kisha akina mama huzunguka ulipowekwa mti husika huku wakiimba kwa furaha na vigelegele kuashiria kwamba zoezi la tohara limefanyika na kukamilika.

Kwa mujibu wa imani ya kabila hilo nyimbo za shangwe na faraja zinazoimbwa na kina mama kwa kuzunguka mti huo ukiwa kwenye nyumba humfanya kijana kuwa na faraja kutofikiria maumivu aliyoyapata wakati wa tohara.

Tohara katika kabila la wamasai inahusisha mafundisho yote ya msingi kwa mwanaume ikiwa ni pamoja na kuwafanya wawe majasiri na shujaa wanaoweza kukabiliana na changamoto zozote za kimaisha tofauti na vijana wanaozaliwa mjini maarufu kama vijana wa elfu mbili (2000) ambao wengi wao maumivu ya jando hawayafahamu kutokana na kutahiriwa wakiwa wadogo tena wengi wao wakifanyiwa tohara hospitali.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo la upandaji wa miti Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro anayesimamia Idara ya Maendeleo ya Jamii Gloria Bideberi amesema kuwa mamlaka itaendelea kuithamini miti hiyo na kushirikiana na jamii ya kabila hilo kuhakikisha miti hiyo haitoweki

Kiongozi wa kimila wa kata ya Ngorongoro bwana Sembeta Ngoidiko amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miti na kusema na wananchi wa kijiji cha Oloirobi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wameamua kupanda miti hiyo pamoja na miti mingine inayotumika kama miti dawa ili kuendelea kudumisha uhifadhi,mila na desturi.






















LIGI ya Mabingwa Ulaya (UEFA) itaendelea leo hii ambapo mechi zote za mwisho kwenye msimamo zitapigwa huku nafasi ya wewe kuondoka na mkwanja mrefu ikiwa kubwa. Je beti yako unaiweka kwa nani leo?

AS Monaco atamenyana dhidi ya Juventus ambao wapo nafasi ya 15 huku wenyeji wao wakiwa nafasi ya 21 hadi sasa. Kila timu inahitaji ushindi siku ya leo kujiweka sawa kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa au kuangukia Play offs. Meridianbet wameipa mechi hii ODDS KUBWA. Bashiri hapa.

Mechi nyingine ni hii ya Barcelona vs Copenhagen ambapo vijana wa Hans Flick wanahitaji ushindi wa magoli mengi kwenye mechi hii. Wageni wao wapo nafasi ya 26 ambayo haiwezi kuwapeleka sehemu yoyote. Nafasi ya kushinda mechi hii wamepewa Barca pale Meridianbet. Jisajili hapa.

Nao Bayer Leverkusen kutoka kule Ujerumani watakuwa kibaruani dhidi ya Villarreal ambao wapo nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa ligi wakitoa sare moja kwenye mechi 7 walizocheza. Mwenyeji anahitaji ushindi huu leo kwani mechi iliyopita, alipoteza huku mgeni naye akipoteza. Tandika jamvi hapa.

Pesa ipo kwenye michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roulette,Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Bingwa mara nyingi wa michuano hii Real Madrid atakuwa ugenini kukiwasha dhidi ya Benfica ambao mpaka sasa kwenye mechi 7 walizocheza wameshinda mbili pekee na kupoteza mechi zote 5. Wakali wa ubashri Meridianbet wanampa nafasi kubwa ya kushinda Real. Wewe nani unampa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi?. Beti hapa.

Borussia Dortmund yeye atamenyana dhidi ya Inter Milan huku tofauti ya pointi kati yao hadi sasa ikiwa ni 1 pekee. Wote wametoka kupoteza mechi zao zilizopita, hivyo basi leo hii ushindi ni muhimu kwenye timu zote mbili. Je nani kuondoka na ushindi mechi hii ya mwisho?. Bashiri hapa.

Vijana wa Pep Guardiola, Manchester City atamenyana vikali dhidi ya Galatasaray ambao wapo nafasi ya 17 kwa 11, huku tofauti ya pointi kati yao mpaka sasa ni 3 pekee. City wametoka kupoteza mechi yao iliyopita huku mechi hii ikiwa ni muhimu sana kwao kushinda pale Etihad. Je wageni watakubali kupoteza mechi hii ugenini?. Suka jamvi hapa.

Mechi nyingine kali ni hii ya Napoli vs Chelsea ambapo hawa wote wanahitaji ushindi kwenye mechi hii ya leo. Mara ya mwisho kukutaa hawa wawili ilikuwa 2012 ambapo The Blues waliondoka na ushindi. Je leo hii katika dimba la Maradona nani kuondoka na pointi 3?. Jisajili hapa.

Kwa upande wa Bayern Munich watamenyana dhidi ya PSV ambao wapo nafasi ya 22 kwenye msimamo wa ligi. Vijana wa Kompany wao wameshafuzu hivyo mechi hii haina umuhimu mkubwa sana kwao ukilinganisha na wenyeji. Machaguo zaidi ya 1000 yapo mechi hii. Tandika jamvi hapa.

PSG vs Newcastle United ni moja kati ya mechi kali ambayo itapigwa hii leo ambapo mwenyeji ametoka kupoteza mechi iliyopita, huku wageni wao wakishinda. ODDS KUBWA zipo mechi hii leo huku nafasi ya wewe kuondoka na maokoto ikiwa nje nje. Jisajili hapa.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya ALAF Tanzania imezindua rasmi Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka wa 2025, ambapo wanaotarajiwa kushiriki shindano hilo wametakiwa kuwasilisha kazi zao kwa ajili ya kupitiwa na majaji.

Hiyo ni tuzo ya 10 tangu kuanzishwa kwake 2015 na inafadhiliwa na kampuni ya ALAF Limited ya Tanzania na Mabati Rolling Mills ya Kenya (kampuni tanzu za Safal Investments Mauritius Limited).

Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited Tanzania, Hawa Bayumi amesema tuzo hiyo inaendelea kukua mwaka hadi mwaka huku ikivutia washiriki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Hadi leo hii, zaidi ya kazi 3000 zimeshawasilishwa katika shindano hilo na washindi 29 wameshapokea zawadi zao ndani ya miaka hii 10. Miswada 22 kati ya iliyoshinda imeshachapishwa na Mkuki na Nyota Publishers na iliyobakia ipo kwenye mchakato wa kuchapishwa,” ameeleza.

Kuhusu zawadi alisema katika kipengele cha Riwaya mshindi wa kwanza atazawadiwa Dola 5,000 na Mshindi wa pili Dola 2,500, katika kipengele cha ushairi mshindi wa kwanza ataondoka na Zawadi ya Dola 5,000 na Mshindi wa pili Dola 2,500 wakati katika kipengele kipya cha hadithi fupi kutakuwa na mshindi mmoja tu atakayepokea Dola 2500.

Miswada itaanza kuwasilishwa kuanzia leo hii tarehe 28 Januari hadi tarehe 31 Machi 2026 ambapo zoezi hilo litafungwa rasmi ili kuwapa majaji nafasi ya kupitia miswada husika. Hafla ya utoaji tuzo inatarajiwa kufanyika Julai 2026 ambapo washindi watatangazwa.

“Tunatoa rai kwa waandishi duniani kote watumie fursa hii kujitangaza, wachapishe kazi zao ili wachangie katika kukuza lugha adhimu ya Kiswahili,” amesisitiza Bi. Bayumi.

Amebainisha kampuni ya ALAF inajivunia na itaendelea kutoa mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili kama chachu ya maendeleo ya kiuchumi, taaluma na utamaduni nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Dk.Ramadhani Kadallah ameipongeza ALAF Kwa jitihada zake ze Mukunza Lugha ya Kiswahili."Tutaendelea kushirikiana na waandaaji kwani tuna maslahi makubwa na jambo hili.”

Mmoja wa washindi wa mwaka jana, Bashiru Abdallah alitoa Rai Kwa watunzi kutumia fursa hii kujitangaza na kuhakikisha wanaiandaa kazi zao vizuri ili wawe katika nafasi nzuri ya kushinda. "Ukiachia kushinda, tukio hili ni sehemu nzuri yakukutana na watu mbalimbali na kubadilishana uzoefu," alisisitiza.

Tuzo hiyo, iliyoanzishwa mwaka wa 2014 na Dkt. Lizzy Attree (Mkurugenzi wa Tuzo ya Caine) na Dkt. Mukoma Wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell), lengo kuu likiwa ni kutambua kazi nzuri za uandishi kwa lugha za Kiafrika sambamba na kuhimiza kazi za tafsiri kutoka lugha moja hadi nyingine miongoni mwa lugha za Kiafrika.

Safal Investments Mauritius Limited na matawi yake (Mabati Rolling Mills Limited ya Kenya na ALAF Limited nchini Tanzania) kwa pamoja yanajulikana kama The Safal Group. Safal Group ndiyo mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kuezekea Barani Afrika ambapo kampuni hiyo inafanya jumla ya shughuli za uwekezaji 36 katika mataifa 11 Barani Afrika.



Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mheshimiwa Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, ametembelea Kivuko cha Mabrouk na Kivuko cha Matembezi vilivyopo Mtaa wa Kibamba, Kata ya Kibamba, kwa lengo la kujionea hali halisi ya miundombinu ya vivuko hivyo na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi wanaovitumia katika shughuli zao za kila siku.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Kairuki amesema amechukua hatua ya kugharamia kiasi cha shilingi 2,745,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kivuko cha Mabrouk ili kiweze kupitika kwa usalama na waenda kwa miguu.

Hatua hiyo inalenga kupunguza adha kwa wananchi pamoja na kuzuia matukio ya vifo vilivyokuwa vikijitokeza mara kwa mara, hususan nyakati za mvua kubwa ambapo baadhi ya wananchi walikuwa wakisombwa na maji.

Kwa upande wa Kivuko cha Matembezi, ambacho kimekuwa kwenye mipango kwa zaidi ya miaka 15 bila kutekelezwa, Mheshimiwa Angellah Kairuki aliwahakikishia wananchi wa Mtaa wa Kibamba kuwa atalifuatilia kwa karibu na kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi wa kudumu ili kuondoa changamoto hiyo ya muda mrefu.

Wananchi wa Kibamba wamepongeza jitihada za Mbunge wao, wakieleza kuwa hatua hizo zinaonesha dhamira ya dhati ya kiongozi wao katika kusikiliza, kushughulikia na kutatua changamoto za msingi zinazowagusa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.