Dodoma, 8 Agosti 2026
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kutafuta na kufungua masoko ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, hatua inayolenga kuwawezesha wazalishaji kupata masoko ya uhakika na kuongeza tija katika sekta za uzalishaji.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Agosti 8, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane) Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya John Malecela, Nzuguni, Dodoma. Amesema Tanzania imeendelea kufungua milango zaidi kwa biashara na uwekezaji, huku Serikali ikiweka mazingira wezeshi kwa wazalishaji na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Katika kuimarisha uzalishaji wa ndani, Kiwanda cha K4 cha Kilombero Sugar kimetajwa kuwa uwekezaji muhimu katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, kupunguza utegemezi wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi na kuchangia katika safari ya Tanzania kuelekea kujitosheleza kwa sukari.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nane Nane, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano na Wadau wa Kilombero Sugar, Bw. Victor Byemelwa, amesema kampuni inajivunia uwekezaji wa K4 ambao umeongeza uwezo wa uzalishaji wa sukari na unatarajiwa kuchochea ukuaji wa kilimo cha miwa pamoja na uchumi wa maeneo yanayozunguka shughuli za kampuni.

Amesema uwekezaji huo hauishii katika uzalishaji wa sukari pekee, bali pia una uwezo wa kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na matumizi ya mabaki ya miwa, hatua inayoweza kuchangia katika kuimarisha upatikanaji wa nishati na kuongeza mchango wa kampuni katika gridi ya Taifa.

"Uwekezaji wa K4 ni hatua kubwa katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini. Pamoja na kuongeza uzalishaji, unafungua fursa nyingi zaidi kwa wakulima wa miwa, ajira, biashara na shughuli nyingine ndani ya mnyororo wa thamani wa kilimo," amesema Byemelwa.

Ametoa wito kwa wananchi, hususan wakulima, kutumia fursa zinazotokana na uwekezaji huo kwa kushiriki kikamilifu katika kilimo cha miwa na shughuli mbalimbali zinazohusiana na mnyororo wa thamani, akisema ukuaji wa sekta ya sukari una uwezo wa kuongeza kipato cha kaya na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano na Mawasiliano wa Kilombero Sugar, Bw. Derick Stanley, amesema kampuni imejipanga kuongeza uzalishaji wa sukari nchini ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Stanley amesema katika kuongeza uzalishaji wa miwa, Kilombero Sugar inatarajia kushirikiana na wakulima wa nje ya mashamba ya kampuni ambao wanakadiriwa kuzalisha takribani tani milioni 1.5 za miwa, hatua inayotarajiwa kuwawezesha wakulima hao kupata zaidi ya shilingi bilioni 150, hivyo kuongeza kipato cha kaya na kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo ya uzalishaji.

"Tunaendelea kuangalia fursa za kuongeza uzalishaji na kujenga uwezo wa muda mrefu wa sekta ya sukari. Uwekezaji huu unalenga si tu kuongeza uzalishaji wa sukari, bali pia kuimarisha mnyororo wa thamani, kuongeza fursa kwa wakulima na kuchangia katika maendeleo ya viwanda nchini," amesema Stanley.

Akizungumzia ushiriki wa Kilombero Sugar katika Maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Biashara wa Kilombero Sugar, Bw. Fimbo Butala, amesema pia kampuni imetumia maonesho hayo kusogeza bidhaa na huduma zake karibu na wananchi, huku ikitoa elimu kuhusu uzalishaji wa sukari, kilimo cha miwa na mchango wa kampuni katika maendeleo ya sekta ya kilimo na viwanda.

Amesema Nane Nane ni jukwaa muhimu la kukutana moja kwa moja na wakulima, wateja na wadau wengine wa sekta ya kilimo, kusikiliza maoni yao na kujenga ushirikiano unaolenga kukuza uzalishaji na kuongeza thamani katika mnyororo wa kilimo.

Na Janeth Raphael - MichuziTv

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa muda wa wiki moja wamiliki na waendeshaji wa kampuni za mabasi makubwa ya mikoani kuhakikisha wanaanza kutumia Stendi ya Magufuli kama kituo cha kuanzia na kumalizia safari zao, katika hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Chalamila ametoa agizo hilo leo jijini Dar es katika Mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema mabasi hayo hayatapaswa tena kuingia katikati ya jiji kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria, isipokuwa kampuni sita ambazo tayari zimepewa vibali maalum vya kushusha abiria katika maeneo ya katikati ya jiji. 

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, kampuni nyingine zote zinatakiwa kutumia Stendi ya Magufuli na kuzingatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali.

Chalamila amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi hayo wametakiwa kutumia muda uliopo hadi Agosti 17, 2026 kufanya maandalizi muhimu, huku utekelezaji wa agizo hilo ukianza rasmi baada ya tarehe hiyo. 

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mfumo wa usafiri na kupunguza msongamano unaoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa mabasi makubwa yanapoingia katikati ya jiji kwa ajili ya kushusha au kupakia abiria, yanaongeza idadi ya magari katika maeneo ambayo tayari yana msongamano mkubwa, hivyo matumizi ya Stendi ya Magufuli yatasaidia kuyapunguza mabasi hayo katika maeneo ya katikati ya jiji na kuweka utaratibu mzuri wa usafirishaji wa abiria wanaoingia au kutoka Dar es Salaam.

Chalamila amesema abiria watakaofikishwa katika Stendi ya Magufuli hawataachwa bila usafiri wa kuendelea na safari zao, kwani wataweza kutumia huduma mbalimbali za usafiri wa ndani kuelekea maeneo wanayokwenda. 

Miongoni mwa usafiri huo ni mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji na pikipiki, huku kampuni za mabasi zikiruhusiwa pia kuweka huduma za shuttle kwa ajili ya kuwasaidia abiria kutoka stendi hiyo kwenda maeneo mbalimbali ya jiji.

Kwa mujibu wa Chalamila, utaratibu huo hautalenga tu kupunguza msongamano wa magari, bali pia unalenga kulinda na kuongeza fursa za ajira na biashara kwa waendeshaji wa usafiri wa ndani. 

Amesema mabasi makubwa yanapoingia hadi katikati ya jiji na kufanya shughuli ambazo zinaweza kufanywa na watoa huduma za usafiri wa ndani, yanaathiri moja kwa moja shughuli za kiuchumi za kundi hilo la wadau.

Amesema mfumo huo mpya utawezesha kuwepo kwa mgawanyo mzuri wa majukumu katika sekta ya usafirishaji, ambapo mabasi makubwa yatabeba abiria kutoka mikoa mbalimbali na kuwafikisha katika Stendi ya Magufuli, kisha usafiri wa ndani kuchukua jukumu la kuwaunganisha abiria hao na maeneo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam.

Chalamila amewataka wamiliki na waendeshaji wa mabasi makubwa kutumia muda uliotolewa kufanya maandalizi ya kutosha, ikiwemo kupanga namna ya kuwasaidia abiria wao kuendelea na safari kutoka Stendi ya Magufuli. 

Amesisitiza kuwa baada ya Agosti 17, 2026, utekelezaji wa utaratibu huo utaanza rasmi, huku kampuni ambazo hazina vibali maalum vya kushusha abiria katikati ya jiji zikitarajiwa kuzingatia kikamilifu agizo hilo.

Hatua hiyo inatarajiwa kuwa sehemu ya mabadiliko katika mfumo wa usafiri wa Mabasi ya masafa marefu jijini Dar es Salaam, huku Serikali ikilenga kuhakikisha mabasi makubwa yanafanya shughuli zake katika vituo vilivyotengwa na abiria wanapata huduma rahisi na salama za usafiri wa ndani kuelekea wanakokwenda.



FARIDA SAID, MOROGORO 

Ng'ombe 56 waliokuwa mali ya mfugaji Clement Bernad sasa wamebaki kuwa sehemu ya historia yake ya ufugaji, ukame unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi na kupungua kwa malisho vimemlazimisha kubadili mfumo wa ufugaji, akipunguza idadi ya mifugo na kuanza kuangalia zaidi uwezo wa kuzalisha malisho na kuihudumia mifugo aliyonayo.

Bernad mkazi wa kijiji cha Mtanana wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma ni mfano wa mabadiliko yanayowakabili wafugaji katika eneo hilo, uhaba wa malisho unalazimisha mifugo kutafuta chakula nje ya maeneo ya wafugaji na wakati mwingine kuingia katika mashamba ya wakulima, hali inayochochea migogoro kati ya pande hizo mbili.

Bernad anasema baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalam kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo ( SUA ) kuhusu ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabianchi, ameamua kupunguza idadi ya ng'ombe wake na kubaki na idadi anayoamini anaweza kuihudumia kwa malisho na rasilimali alizonazo.

"Nilikuwa na ng'ombe 56 wa kienyeji, lakini baada ya kupata elimu nimeona umuhimu wa kuwa na mifugo ambayo ninaweza kuihudumia vizuri badala ya kuwa na mifugo mingi ambayo inakosa chakula," anasema Bernad.

Uamuzi huo unaakisi changamoto kubwa inayowakabili wafugaji nchini ambapo mabadiliko ya tabianchi yamekuwa yakibadilisha upatikanaji wa malisho na maji, hali inayogusa moja kwa moja uzalishaji wa mifugo ikiwemo maziwa.

Afisa Ugani wa Kata ya Mtanana Dominica Samweli Swai, anasema mabadiliko ya tabianchi yamekuwa miongoni mwa sababu zinazoendelea kuchochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwasababau wafugaji wakikosa malisho wanalazimika kuuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Anasema suluhisho mojawapo ni kuwahamasisha wafugaji kuanza kuzalisha malisho katika maeneo yao ili kupunguza utegemezi wa malisho ya asili na ulazima wa kupeleka mifugo kutafuta chakula maeneo mengine.

"Wafugaji wengi wamehamasika kupanda malisho katika maeneo yao. Kama wafugaji watabadilika na kuacha mfumo wa kuchunga mifugo yao bila kuwa na uhakika wa malisho, tunaweza kupunguza migogoro mingi kati ya wakulima na wafugaji," anasema Swai.

Kata ya Mtanana pekee wafugaji 1,320 wenye jumla ya mifugo 7,829, idadi inayoweka wazi ukubwa wa mahitaji ya malisho katika eneo ambalo linakabiliwa na changamoto ya ukame.

Hata hivyo, kupanda malisho pekee kunaweza kusiwe jibu la muda mrefu iwapo aina ya malisho inayotumika haiwezi kustahimili vipindi virefu vya ukame.

Hapo ndipo watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameingia kazini kutafuta aina za malisho zinazoweza kustahimili ukame, huku wakilenga kutoa suluhisho linaloweza kuwasaidia wafugaji kuendelea kuzalisha mifugo hata katika mazingira yanayobadilika kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungmza na waandishi wa habari Mkuu wa mradi kutoka Idara ya sayansi za wanyama, ufugaji viumbe maji na nyanda za malisho Chuo kikuu SUA, Prof. Sebastian Chenyambaga amesema utafiti huo ni sehemu ya mradi unaolenga kuimarisha uwezo wa wafugaji kustahimili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, unaofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Mradi huo wa miaka mitatu ulianza Oktoba 2025 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2028, ukiangalia namna mabadiliko ya tabianchi yanavyowaathiri wafugaji na kutafuta mbinu zinazoweza kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na athari hizo.

Mradi unatekelezwa katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Kishapu mkoani Shinyanga na Miatu mkoani Simiyu, maeneo ambayo yamechaguliwa katika utekelezaji wa utafiti huo.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka Idara ya sayansi za wanyama, ufugaji viumbe maji na nyanda za malisho Chuo kikuu SUA, Dkt. Doris Lutatenekwa amesema utafiti pia unaenda sambamba na kupima aina za malisho zinazostahimili ukame.

Lengo la utafiti huo si kutafuta malisho ya kuokoa mifugo pekee, bali pia kuangalia namna wafugaji wanavyoweza kuendelea kuzalisha maziwa na bidhaa nyingine za mifugo katika mazingira yenye changamoto ya ukame.

Mkurugenzi wa Costech Dkt. Amos Nungu anasema mradi huo ni miongoni mwa hatua zinazolenga kutekeleza Dira ya Tanzania ya 2050 kwa kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Anasema tafiti zinazolenga kupata suluhisho la changamoto za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu katika kujenga jamii yenye uwezo wa kustahimili mabadiliko ya mazingira na kulinda shughuli za kiuchumi za wananchi.

Kwa wafugaji kama Bernad, mabadiliko hayo hayapo tena kwenye vitabu au mijadala ya wataalamu, yameingia moja kwa moja katika maisha yao yakimlazimisha mfugaji kujiuliza si tu “nitafuga ng'ombe wangapi?”, bali pia “nitawapataje chakula wakati mvua hazitoshelezi?”









LEO jioni, kuanzia saa 18:00 uwanja wa Aspmyra ulioko ndani ya Arctic Circle kaskazini mwa Norway utakuwa jukwaa la mojawapo ya mechi kali zaidi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Bodø/Glimt watawakaribisha Union Saint-Gilloise wakiwa na lengo moja tu kufuta hesabu iliyobaki wazi baada ya mechi ya kwanza kumalizika kwa sare ya kutisha ya mabao 3-3 huko Brussels, ambapo Patrick Berg aliwafungulia Bodø/Glimt bao, kabla Raul Florucz kulipiza kwa Union. Mechi hiyo ya kwanza ilikuwa na mizunguko mingi ya hisia Ole Didrik Blomberg aliongeza bao la penalti kwa ajili ya Union, Florucz akasawazisha tena nyakati za nyongeza, kisha Promise David akawaweka Union mbele dakika mbili kabla ya muda wa kawaida kwisha, kabla Odin Bjørtuft kuokoa mechi kwa Bodø/Glimt dakika ya mwisho kabisa.

Hali hii inamaanisha kwamba kwa sasa, iwapo mechi ya leo itaisha sare bila mabao (0-0), ushindi wa jumla utakwenda kwa Bodø/Glimt kutokana na sheria ya mabao ya ugenini. Hii inaweka Union Saint-Gilloise katika hali ngumu zaidi kisaikolojia lazima washinde, au wafunge angalau bao moja zaidi ya mwenyeji katika sare, ili kuendelea na safari yao kuelekea raundi ya playoff. Kwa upande wa mwenyeji, Bodø/Glimt wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kasi ya ajabu ya kimchezo. Timu hiyo haijafungwa katika mechi kumi na moja mfululizo katika mashindano yote, huku ikiwa juu ya msimamo wa ligi ya Eliteserien nyumbani Norway.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Baada ya mechi ya kwanza dhidi ya Union, Bodø/Glimt waliendelea na msukumo wao kwa kuwafunga Vålerenga mabao 2-1 katika ligi ya taifa ushahidi kwamba safu yao ya mashambulizi bado iko makini licha ya mzigo wa mechi za Ulaya.

Kocha Kjetil Knutsen ana rekodi nzuri ya kuongoza timu hii dhidi ya wapinzani wakubwa wa Ulaya, kwani msimu uliopita waliweza kuzifikia hatua za mwisho 16 baada ya kuzishinda Manchester City, Atletico Madrid, na Inter Milan.

Union Saint-Gilloise nao hawaji mkono mtupu. Baada ya mechi ya kwanza, waliifunga Westerlo kwa mabao makubwa ya 5-1 katika ligi ya Ubelgiji siku ya Jumamosi, ikionyesha kwamba safu yao ya mashambulizi bado ina uwezo wa kuleta madhara popote wanapocheza. Hata hivyo, wasiwasi mkubwa upo upande wa ulinzi timu hiyo imefunga mabao 12 katika mechi zao tano za mwisho, hali inayoonyesha udhaifu ambao Bodø/Glimt watataka kuutumia kikamilifu wakiwa nyumbani mwao.

Kutoweka kwa viongozi wa zamani wa ulinzi kama Christian Burgess na kipa Kjell Scherpen msimu huu kumeongeza changamoto kwa kocha David Hubert katika kuimarisha safu ya nyuma. Hata hivyo, historia ya mechi hizi mbili ikiwemo mkutano wao wa awali katika Europa League uliomalizika sare ya bila mabao inaonyesha kwamba timu hizi mbili zinafanana kimtindo na uwezo, hivyo kutabiri matokeo dhahiri si rahisi.

Mchezo huu utaamua ni nani atakayeendelea kupambana kwenye raundi ya playoff ya kufuzu Ligi ya Mabingwa. Bodø/Glimt wanahitaji tu matokeo ya sare bila mabao au ushindi ili kuendelea, wakati Union Saint-Gilloise hawana budi ila kushinda au kufunga zaidi katika sare ili kuepuka kutolewa nje ya mashindano. Ukiangalia msukumo wa sasa wa pande zote mbili, hii itakuwa mechi ya mvutano mkubwa kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho. Jisajili leo
MAWIMBI ya burudani yamepanda tena kwenye ulimwengu wa kasino huku Meridian Scatter Whale ikiwasili kwa kishindo ndani ya Meridianbet, mchezo mpya unaowapeleka wachezaji kwenye safari ya kipekee ndani ya kina cha bahari. Ukiwa na mandhari ya kuvutia, alama zenye mvuto na msisimko wa kila mzunguko, mchezo huu unakualika kugundua hazina zilizofichwa huku ukifurahia kila sekunde ya burudani.

Kwenye Meridian Scatter Whale, kila mzunguko ni mwanzo wa tukio jipya. Nguvu ya nyangumi mkubwa wa baharini ndiyo inayoongoza safari hii ya kusisimua, ikileta hali ya matarajio na furaha kila unapocheza. Wachezaji wanaweza kujiachilia kwenye mazingira ya kuvutia yaliyojaa vipengele maalum vinavyoongeza msisimko wa mchezo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa wapenzi wa kasino wanaotafuta uzoefu tofauti, mchezo huu umebeba mchanganyiko wa burudani, ubunifu na nafasi ya kupata zawadi za kuvutia. Kila alama inapojipanga kwenye mchezo inaweza kuwa sehemu ya safari kubwa zaidi, huku kila mzunguko ukiweka matarajio mapya ya ushindi na starehe.

Meridian Scatter Whale ni zaidi ya mchezo wa kawaida wa sloti, ni safari ya chini ya bahari inayokupa nafasi ya kuingia kwenye ulimwengu wa mawimbi, viumbe wa baharini na matukio ya kusisimua. Kwa wachezaji wanaopenda changamoto mpya za kasino, huu ni muda wa kupiga mbizi na kujaribu bahati yako kwenye tukio hili la kipekee.

Usikose kujiunga na msisimko wa Meridian Scatter Whale leo. Cheza sasa, fuata mwongozo wa nyangumi mwenye nguvu na ujionee burudani ya kipekee inayokungoja ndani ya kina cha bahari. Safari yako ya ushindi na zawadi inaanza na raundi moja tu ndani ya Meridianbet.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 10 Agosti, 2026.




Katibu NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Kihongosi amesisitiza kuwa  Vijana ndio walinda Nchi hivyo wanatakiwa kuilinda amani ya nchi ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya Taifa na familia zao.

Ndugu Kenani ameyasema hayo leo tarehe 10 Agosti 2026 wakati akitoa mada kwenye Mafunzo ya Uongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo Ihemi mkoani Iringa.

Pia, ametumia jukwaa hilo kukemea lugha chafu zinazotolewa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mitandao ya kijamii na kuwasihi vijana kuwa mstari wa mbele kumtetea Rais na wasikae kimya.

Aidha ametoa wito kwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  ndani na nje ya Tanzania kulipa Ada ya uanachama akieleza uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unatokana na wanachama kulipia ada.












EY Tanzania imezindua kwa mafanikio Ripoti ya Sekta Ndogo ya Benki Tanzania 2025, tukio lililowakutanisha viongozi wa sekta ya fedha, wadhibiti na wataalamu wa benki kujadili mwelekeo wa sekta hiyo katika mazingira yanayobadilika kwa kasi. Mada kuu ya mwaka huu ilikuwa“Akili Mnemba katika Sekta ya Benki: Faida ya Ushindani Ijayo”, ikilenga kuonesha jinsi Akili Mnemba (AI) inavyobadilisha ushindani katika huduma za kifedha.
Majadiliano hayo yaliongozwa na Bi. Irene Morris (EY) ambapo aligusia safari ya mageuzi ya sekta ya benki kutoka mifumo ya jadi inayotegemea mahusiano ya karibu na wateja (relationship banking) hadi benki za kidijitali, majukwaa ya kifedha (platform banking) na mifumo ya ikolojia ya huduma za kifedha (ecosystem banking). Washiriki walijadili namna AI, data na teknolojia vinavyoboresha uzoefu wa wateja, kuimarisha usimamizi wa hatari, kuongeza ufanisi wa shughuli za benki na kuibua fursa mpya za ukuaji wa biashara.

Tukio hilo pia liliangazia mwenendo muhimu unaoendelea kuunda sekta ya benki nchini Tanzania, ikiwemo ukuaji endelevu wa sekta, kuongezeka kwa ujumuishaji wa kifedha, matumizi yanayoongezeka ya huduma za kifedha za kidijitali, pamoja na umuhimu wa ubunifu katika kujenga taasisi za kifedha zilizo imara na zenye uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya siku zijazo.
Aidha, washiriki walipata fursa ya kujadili kiwango kipya cha utoaji taarifa za kifedha (IFRS 18) na athari zake kwa sekta ya benki. Majadiliano yalioongozwa na Bw. Joshua Luoga (EY) ambapo alitoa ufahamu kuhusu mabadiliko yajayo katika uwasilishaji wa taarifa za kifedha, upimaji wa utendaji wa kifedha pamoja na kuongeza uwazi kwa wadau wa sekta ya fedha.
EY Tanzania inawashukuru kwa dhati wazungumzaji, (Bw. Rweyemamu Barongo, Kiongozi wa Kitengo cha Ubunifu wa Akili Mnemba (AI) na Data katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Tobias Swai, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Fedha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Pamoja na Bw. Robert Bwana, Mwanasayansi Mwandamizi wa Data katika Benki ya NMB) washiriki na wadau wote waliochangia mjadala wenye tija kuhusu mustakabali wa sekta ya benki nchini Tanzania na nafasi ya teknolojia na ubunifu katika kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo.
Na Victor Masangu, Kibaha

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wawake (UWT) Wilaya ya Kibahaa mjini Elina Mgonja Katika kuuunga juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kiuchumi ameamua kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo kwa wanawake wapatao 400 wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuondokana na wimbi la umasikini.

Akizungumza katika ziara yake maaalumu ya kikazi yenye lengo la kuwatembelea wanawake wa (UWT) katika kata mbali mbali kwa ajili ya kuwapa maarifa na ujuzi na kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa za aina tofauti ambazo zitawapa fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuondokana na kuwa tegemezi kila kukicha.

Elina amebainisha kuwa amefanya ziara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa ya kuwasaidia wanawake wa UWT kutoka kata zote 14 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kwamba mafunzo hayo ambayo ameamua kuyatoa bure bila malipo yoyote yatakuwa ni mkombozi mkubwa katika kujikwamua kiuchumi,

Nao baadhi ya wanawake ambao wamepata mafunzo hayo akiwemo Mwajuma Makuka wamesema kwamba maffunnzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na kuwa tegemezi na kwamba watakwenda kuyafanyia kazi kwa hali na mali kwa lengo la kuweza kuondokana na wimbi la umasikini.

"Kwa kweli tunapenda kumshukuru kwa dhati Mwenyekiti wetu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonjwa kwa kuweza kufanya ziara hii na kuja kutupa elimu na mafunzo ya ujasiliamali na tumeweza kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo kutengeneza bidhaa kama vile kutengeneza batiki, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea pamoja na kupata ujuzi ambao tutakwenda kuufanyia kazi katika kutekeleza majukumu yetu,"amebainisha Mwajuma.

Mwenyekiti huyo wa UWT anaendelea na ziara yake ya kikazi ambapo hadi sasa ameshatembelea kata 7 ambazo ni Msangani, Mkuza, Tumbi, Maili moja, Kongowe, Kibaha pamoja na Kata ya Misususugu ambapo jumla ya wanawake 400 wameweza kunufaika na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vitendo.