SHIRIKA la Room to Read, limeingia makubaliano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ikiwa ni sehemu ya kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana.
Akizungumza
katiha hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read, Bi. Joan Ndaambuyo Minja alisema
wanatambua na kuthamini
dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, jumuishi na
yenye kumjengea maarifa, stadi na uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya Taifa,
hivyo lina kila sababu ya kuunga mkono juhudi hizo.
Alisema
shirika hilo linauchukulia
ushirikiano na Serikali kuwa ni sehemu ya kutekeleza vipaumbele vya kitaifa
katika sekta ya elimu, badala ya kuwa utekelezaji wa programu za Room to Read
moja kwa moja.
“…Leo
ni siku muhimu katika historia ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania
na Shirika la Room to Read Tanzania. Utiaji saini wa Hati hii ya Makubaliano
unaweka msingi rasmi wa kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano wetu
katika maeneo mawili muhimu: uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa
watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana,
hususan wasichana,” alisema, Bi. Minja.
Alibainisha kuwa makubaliano waliosaini yanaendana na mwelekeo wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014, Toleo la 2023, inayosisitiza umuhimu wa elimu yenye ubora, usawa wa
fursa, ujumuishi na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuendeleza elimu
nchini.
Aliongeza kuwa Sera inatambua kuwa jukumu la
kuboresha elimu si la Serikali pekee. Linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya
Serikali, taasisi zake, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa
maendeleo, wazazi na jamii kwa ujumla.
“…ushirikiano huu
unaendana na matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga
kujenga Taifa lenye watu wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uwezo wa kukabiliana
na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Dira hii inatukumbusha umuhimu wa
kuwekeza katika rasilimali watu kuanzia hatua za awali za ujifunzaji,
kuimarisha elimu yenye ubora na kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume, wasichana
na wavulana wanapata fursa sawa za kujifunza, kuendeleza vipaji vyao na kushiriki
katika maendeleo ya Taifa,” amesisitiza, Bi. Joan Minja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla hiyo, alisema miongoni mwa malengo makuu ya Hati ya Makubaliano waliosaini ni Kushirikiana katika uandaaji, kupitia na kuhuisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili viendane na viwango vya Mitaala ya Taifa, kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, na Mwongozo wa Kitaifa wa Mitaala ya ElimuMsingi, kwa lengo la kuimarisha ubora na ufanisi wa ujifunzaji wa stadi za msingi.
Alisema mengine muhimu waliokubaliana na katika
ushirikiano huo ni, kuimarisha umahiri wa walimu kupitia mifumo ya mafunzo ya
ualimu kabla ya kuanza kazi na mafunzo endelevu kwa walimu walio kazini, kwa
kuandaa na kutekeleza mafunzo kwa kuzingatia Mkakati wa Taifa wa Maendeleo na
Usimamizi wa Walimu pamoja na vipaumbele vya kitaifa vya kuimarisha umahiri wa
walimu na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji darasani.
Aidha alibainisha na
Pia tumekubaliana; kuwezesha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa na bila ubaguzi,
kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia, kwa mujibu wa Mkakati wa Taifa wa
Maendeleo ya Jinsia pamoja na vipaumbele vya elimu jumuishi vilivyoainishwa.
| Picha ya pamoja. |
BODI ya Korosho Tanzania (CBT) imewahakikishia wawekezaji wanaojenga viwanda vya kubangua korosho nchini kuwa watapata malighafi za kutosha kuendesha shughuli zao, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uwezo wa viwanda vya kubangua korosho nchini ifikapo mwaka 2030.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Francis Alfred, amesema bodi itahakikisha wawekezaji wanaotumia fedha nyingi kujenga viwanda hawajikuti wakishindwa kuviendesha kutokana na uhaba wa korosho ghafi.
Alfred ametoa kauli hiyo Novemba 7, 2026, mkoani Mtwara, wakati wa kikao cha wadau wa korosho kilichoandaliwa na Benki ya NMB, kikihusisha wabanguaji, wanunuzi na wafanyabiashara kujadili fursa za ufadhili zinazolenga kutatua changamoto katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.
Amepongeza hatua ya NMB kuwakutanisha wadau hao, akisema ushirikiano kati ya taasisi za fedha na wafanyabiashara wa korosho ni muhimu katika kuongeza uzalishaji na kufanikisha azma ya nchi ya kupanua uwezo wa viwanda vya kubangua korosho ifikapo mwaka 2030.
Aidha, amezihimiza taasisi nyingine za fedha kuwa karibu na wadau wa sekta hiyo ili kutambua mahitaji yao na kutoa masuluhisho yanayochochea ukuaji wa biashara.
Alfred pia amezitaka benki kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kwa wakati ili kuwawezesha kutimiza mahitaji yao ya kifedha na kujiandaa kwa shughuli zinazofuata za uzalishaji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalugenge, amesema benki hiyo imejipanga kusaidia biashara za korosho katika msimu wa 2026/2027 kupitia masuluhisho mbalimbali ya kifedha.
Amesema huduma hizo zinalenga kuwawezesha wanunuzi wa korosho kupitia minada na masoko ya awali kupata mitaji ya kununua mazao kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika, huku wabanguaji wakipata fedha za kununua malighafi za kuendesha viwanda vyao.
Mwalugenge amesema NMB pia inatoa masuluhisho ya kifedha yanayokidhi mahitaji ya wasafirishaji wa korosho nje ya nchi, ili kuwawezesha kufanya manunuzi kwa wakati na kutekeleza mikataba yao ya biashara katika masoko ya kimataifa.
Ameongeza kuwa benki hiyo imeimarisha huduma zake za malipo na miamala ili kurahisisha shughuli za biashara katika hatua mbalimbali za mnyororo wa thamani wa korosho.
Kikao hicho kinatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za fedha na wadau wa korosho, hususan katika kuongeza upatikanaji wa mitaji, kuchochea ubanguaji wa korosho nchini na kuhakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati.






Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vigae pamoja na masinki ya choo kutoka kampuni ya Twyford wenye thamani ya shilingi milioni 24, ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya. Na Janeth Raphael - MichuziTv
BENKI ya CRDB kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (OR-MV) imesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuwawezesha vijana wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kupitia majukwaa ya vijana yanayojulikana kama Campus Connect.
Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha uendeshaji wa makongamano ya Campus Connect na kuwafikia vijana zaidi ya 300,000 ndani ya kipindi cha miaka mitano, kwa kuwajengea uwezo katika maeneo ya ubunifu, ujasiriamali, biashara, vipaji pamoja na matumizi ya fursa mbalimbali za kiuchumi.
Hafla ya uwekaji saini wa makubaliano hayo imefanyika leo, Novemba 9, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, jijini Dodoma, ikiwa ni hatua inayodhihirisha dhamira ya CRDB katika kuchangia maendeleo na uwezeshaji wa vijana nchini.
Kupitia ushirikiano huo, vijana pia wataunganishwa na fursa za mitaji na masoko, hatua itakayowawezesha kubadilisha mawazo na bunifu zao kuwa biashara na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, amesema uwezeshaji wa vijana unapaswa kuanza mapema wanapokuwa vyuoni ili kuwajengea maarifa, uelewa na ujasiri wa kujiajiri badala ya kutegemea ajira rasmi pekee.
Amesisitiza kuwa jukwaa la Campus Connect linapaswa kuwa mfumo endelevu wa kuwafuatilia na kuwaendeleza vijana kuanzia wanapokuwa vyuoni hadi wanapohitimu na kuanza maisha ya kujitegemea, ili kuhakikisha wanatumia ipasavyo maarifa na fursa wanazopatiwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Benki ya CRDB amesema ushirikiano huo unaongeza nguvu katika kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kifedha mapema, kuwawezesha kubuni mawazo, kuanzisha biashara na kutumia kikamilifu fursa za kujiajiri. Amesema kupitia ushirikiano huo, CRDB itaendelea kuwa sehemu muhimu ya safari ya kuwaibua na kuwawezesha vijana, ili waweze kukuza shughuli zao za kiuchumi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima kununua Mbegu za mazao ya bustani hususani parachichi ambazo zina stika maalum za TOSCI, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora na kuhakikisha wakulima wanapata miche inayokidhi viwango.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanunuzi kutambua miche bora kwa urahisi kupitia nembo ya TOSCI, pamoja na kujikinga na kununua miche isiyokidhi viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TOSCI wakati wa maonesho ya jukwaa la kwanza la HortiLogistica Africa yaliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Nyasebwa Chimagu, amesema matumizi ya stika hizo ni sehemu ya mikakati ya taasisi hiyo ya kuimarisha usimamizi wa ubora wa mbegu na miche ya mazao mbalimbali ya bustani.
Amesema kuwa upatikanaji wa miche bora ni muhimu katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima, huku ukichangia kuimarisha ushindani wa mazao ya horticulture katika masoko ya ndani na kimataifa.
Aidha, amewahimiza wakulima na wadau wengine wa sekta ya horticulture kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu ubora wa mbegu na miche ya mazao ya bustani, pamoja na kufahamu aina za mbegu zinazokidhi mahitaji ya masoko ya kimataifa.
TOSCI imesisitiza umuhimu wa wanunuzi kuwa makini wakati wa kununua miche kwa kuhakikisha wanapata miche yenye stika na utambulisho unaotambulika na taasisi hiyo, ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza tija katika kilimo.
Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima kununua Mbegu za mazao ya bustani hususani parachichi ambazo zina stika maalum za TOSCI, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora na kuhakikisha wakulima wanapata miche inayokidhi viwango.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanunuzi kutambua miche bora kwa urahisi kupitia nembo ya TOSCI, pamoja na kujikinga na kununua miche isiyokidhi viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TOSCI wakati wa maonesho ya jukwaa la kwanza la HortiLogistica Africa yaliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Nyasebwa Chimagu, amesema matumizi ya stika hizo ni sehemu ya mikakati ya taasisi hiyo ya kuimarisha usimamizi wa ubora wa mbegu na miche ya mazao mbalimbali ya bustani.
Amesema kuwa upatikanaji wa miche bora ni muhimu katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima, huku ukichangia kuimarisha ushindani wa mazao ya horticulture katika masoko ya ndani na kimataifa.
Aidha, amewahimiza wakulima na wadau wengine wa sekta ya horticulture kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu ubora wa mbegu na miche ya mazao ya bustani, pamoja na kufahamu aina za mbegu zinazokidhi mahitaji ya masoko ya kimataifa.
TOSCI imesisitiza umuhimu wa wanunuzi kuwa makini wakati wa kununua miche kwa kuhakikisha wanapata miche yenye stika na utambulisho unaotambulika na taasisi hiyo, ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza tija katika kilimo.
Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imeshiriki katika Maonesho ya Tisa ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE) jijini Shanghai, nchini China, kwa lengo la kutangaza Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kuwaunganisha wanunuzi wa kimataifa na fursa za biashara ya mazao ya Tanzania.
Katika maonesho hayo ya siku tano (Novemba 5-10, 2026), WRRB imeeleza jinsi mfumo huo unavyowezesha uhifadhi wa mazao katika maghala yenye leseni, utunzaji wa ubora wake na uuzaji wake kwa uwazi.
Akizungumza alipotembelea banda la Tanzania katika maonesho hayo, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shabaan, amepongeza ushiriki wa Tanzania, hususan wa taasisi za serikali, akisema maonesho hayo yanazipa taasisi hizo fursa ya kutangaza huduma zinazotolewa nchini.
Amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutumia maonesho hayo kujitangaza kimkakati na kufikia wanunuzi wa kimataifa wanaotafuta bidhaa za Tanzania.
Aidha, Mwakilishi wa kampuni ya Chengdu Jintao Yunhui International Trade Co., Ltd. ameonesha kuvutiwa na ufuta mweupe wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa mazao yanayouzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.


Na Mwandishi Wetu, Korogwe
WANAFUNZI wa Kike katika Shule za Sekondari nchini wametakiwa kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kuwawezesha kupata ufadhili wa Samia Suluhu ambao utakuwa chachu kwao kuweza kufikia ndoto zao za kielimu.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Kampuni ya Shemnyama African Association Business Consultancy and Insurance Agency Rajab Shemnyama ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa maafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Ambapo alisema kwamba masomo ya sayansi yatawawezesha kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kutokana na utandawazi uliopo

Alisema wanafunzi wanapaswa kutumia fursa za elimu kwa kujituma katika masomo ili shule hiyo iweze kuzalisha wataalamu wengi katika fani mbalimbali.
Pia, alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akiwataka wanafunzi kuitumia kujifunza na kuongeza maarifa badala ya kujihusisha na mambo yanayoweza kuathiri maadili na maendeleo yao.
Aliwaasa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na tabia hatarishi zinazoweza kuhatarisha afya na mustakabali wao, huku akisisitiza umuhimu wa kujitambua na kulinda heshima zao.
Aidha, alisema elimu inapaswa kwenda sambamba na ujuzi wa ziada utakaowawezesha vijana kujiajiri na kujipatia kipato, hasa kutokana na changamoto ya ajira inayoweza kuwakabili baada ya kuhitimu.
Alisisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kushiriki katika matamasha na shughuli za ujasiriamali ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
Akizungumzia suala la chakula shuleni, Shemnyama aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana, akieleza kuwa njaa huathiri umakini na uwezo wa kufuatilia masomo darasani.

Pia, aliomba uongozi wa shule kuimarisha miradi ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kilimo, akibainisha kuwa sekta hiyo inaweza kuwa chanzo cha fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana.
"Lakini pia kupitia Kampuni Yetu hii tutatoa madaftari kwa ajili ya watoto wasiokuwa na wazazi (Mayatima) kwa lengo la kuwapunguzia makali "Alisema
Alisema amezipokea changamoto zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kutafuta namna ya kuzitatua.
Katika maafali hayo ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa maktaba ya Shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Mchango huo umetangazwa na Rajabu Shemnyama, ambaye ni mhitimu wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne, akisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za shule kuinua kiwango cha ufaulu na kuondoa daraja sifuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2026
Shemnyama alisema ameamua kuchangia maendeleo ya shule hiyo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu, akibainisha kuwa yeye ni zao la shule hiyo na anajivunia kuona mabadiliko yaliyofikiwa tangu alipokuwa mwanafunzi.
Alisema maendeleo ya elimu yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, hivyo kuwataka wahitimu na watu wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo kujitokeza kuchangia kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika shughuli za maendeleo, ikiwamo kuchangia madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Old Korogwe, Bilali Shemkai, alisema shule hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayepata daraja sifuri katika matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2026.
Alisema juhudi hizo zimeanza kuonyesha matokeo kutokana na kupungua kwa idadi ya wanafunzi waliopata daraja hilo kutoka 38 mwaka 2023 hadi 20 mwaka 2024 na 10 mwaka 2025.

Alisema mbali na kuondoa daraja sifuri, shule hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 ina jumla ya wanafunzi 520, wakiwamo wasichana 284 na wavulana 236, pamoja na watumishi 32, wakiwamo walimu 31 na mtaalamu mmoja wa maabara.
Ina vyumba 14 vya madarasa na maabara tatu, ambapo maabara za Kemia na Baiolojia zimekamilika, huku maabara ya Fizikia ikiwa bado haijakamilika.
Pamoja na kuwa na huduma za maji, umeme na barabara, shule hiyo pia ina mradi wa kilimo unaohusisha uzalishaji wa mahindi na majaribio ya kilimo cha mpunga kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa chakula.

Hata hivyo, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula cha mchana, hali inayoufanya uongozi kuendelea kuwahamasisha wazazi kushiriki katika uchangiaji wa chakula.
Kupitia utaratibu uliowekwa, kila mzazi anahamasishwa kuchangia kilo nane za mahindi, kilo mbili za maharage na Sh4,000 kwa kila muhula kwa ajili ya chakula cha wanafunzi. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa na changamoto kutokana na mwitikio mdogo wa baadhi ya wazazi.
Changamoto nyingine ni uchakavu wa baadhi ya vyumba vya madarasa na mazingira ya nje ya shule, ambayo wakati mwingine yanaweza kuathiri utulivu na maandalizi ya wanafunzi kitaaluma.
Kutokana na hali hiyo, shule imekuwa ikishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na kata kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri usalama na maendeleo ya wanafunzi.
Uongozi wa shule hiyo unaamini kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, wahitimu na wadau wengine wa elimu utasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kufanikisha malengo ya kuinua ufaulu.






Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru jana usiku tarehe 9 Novemba. 2026 alitua kwenye kambi ya timu hiyo inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA mkoani Morogoro kukagua hali ya kambi hiyo na maendeleo ya wachezaji.
Mara baada ya kukutana na wachezaji hao Dkt.Badru ametoa maelekezo ya wanamichezo wa Ngorongoro kutumia fursa hiyo Kama mojawapo ya kujifunza mambo mapya kutoka taasisi nyingine.
“Tumieni michezo kuitangaza Ngorongoro, chezeni kwa nguvu zenu zote Ila mkumbuke michezo ni furaha na amani na muwe tayari kupokea aina yoyote ya matokeo,”alisema Dkt.Badru.
Afisa Michezo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Yotham Gitige alimshukuru kamishna kwa ziara hiyo na kusema kuwa imewatia moyo katika ushiriki wao kwenye michezo hiyo.










.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
