wanafunzi wa chuo kikuu sehemu ya mlimani leo wamegoma masomo na kuandamana wakidai malipo ya kujikimu ambayo hawajapewa kwa siku kibao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hivi wanafunzi wakigoma kusoma huwa wanagoma kumsomea nani?kaka michuzi unaweza kuwa na statistics za migoma iliyotokea mwaka jana,just to see how many migomo/kunjis we have every year.kama kuna sheria inayoiwajibisha bodi kuwapa wanafunzi hawa mkopo,je ni kwa nini wasitoe taarifa kwa chombo husika(mahakama)kuwa bodi aifuati sheria.na kama bodi ailazimiki kukopesha ni kwa nini wanafunzi hawa wailazimishe?tujifunze kueshimu sheria na taratibu......zemarcopolo!

    ReplyDelete
  2. Huyu mwenye hilo koti ndio kiongozi wa mgomo?

    ReplyDelete
  3. Kunji,
    Hata enzi zetu... tulidhani "kunji" ndio njia fanisi zadi ya kuleta mabadiliko. Kidogo umri sasa umesonga - na naweza kusema, nimegundua kuna njia nyingine nyingi tu; ambazo mtu unaweza kutumia kuwakilisha hoja zako kwa ufanisi zaidi kuliko "kunji" - tatizo ni kuwa wakati tulipokuwa chuoni - hatukuwa tunajua hizo njia nyingine - so ilikuwa ni "kunji" mtindo mmoja.
    Viswali vya msingi hapa ni Je.
    - vijana wetu wanazifahamu hizo njia?
    - Viongozi wa chuo - (viongozi wote kwa jumla) wanaziheshimu hizo njia nyingine za amani?
    - Ni kwa kiasi gani viongozi wa chuo wamejaribu kuwaelimisha vijana wetu, sababu zinazobabisha hali kutokuwa ya kuridhisha? Au ndio mtindo wa "hawa watoto tu... ni lazima wafuate amri..." Iwapo hii ndio attitude ya viongozi - hakuna cha ajabu kuona "kunji" zinaendelea kama kazi!
    * Yes, penda wasipende, ukweil ni kuwa; mzigo na uwezo wa kuzuia vitu kama "kunji" vipo mikononi mwa viongozi - in this case - viongozi wa chuo!
    Ned

    ReplyDelete
  4. Kwa mtindo huu tutaendelea kuwa tegemezi wa utaalamu siku zote. Mwanachuo atapata wapi muda wa kuwa creative wakati anafikiria atakula nini? Fedha yenyewe ni ndogo, halafu inachelewesha. Kwanini hawa watu waliopo madarakani wanashindwa kujifunza nchi zingine zinafanyaje? Inaniuma sana kuona matatizo ya wanachuo hayapatiwi ufumbuzi, wao wanadai sh 1,200,000 hazitoshi mbunge kwa mwezi halafu mwanachuo hata laki moja hazifiki

    ReplyDelete
  5. huyo jamaa wa juu yangu kaongea kweli.....huyo aliyesema viongozi wazuie migomo hajui maana ya mtu kuwa na njaa.....
    emergencypoison

    ReplyDelete
  6. Anonymous,
    Sina uhakika kama ulikuwa ukijibu hoja yangu hapo juu. Nitachechemea kujaribu kujitetea.
    Sikuwa na maana ya viongozi watumie "nguvu" kuzuia mgomo. In fact That will ONLY make the situation worse! Iwapo utasoma hoja yangu vizuri utaona kuwa nilichokuwa nasema ni kuwa... hawa wenzetu waliogoma huenda wamefika mahali ambapo kwao "kunji" ndio njia pekee iliyobaki kujaribu ku-focus attention ya viongozi wao kwenye matatizo yao! _ swali ni kama kweli ilikuwa ni lazima ifikie hapo. Wakati ambapo huenda kwa wanafunzi - that is their best hope; viongozi walikuwa na nafasi, na nadhani bado wana wanafasi ya kuweza kukutana na wanafunzi ili wasikilize na kujaribu kuelewa shida zao. Kwa wakati wetu... All we wanted ni kwa viongozi kuonyesha kujali! kwani kila kitu kiliikuwa kinaashiria kutokujaliwa... inakuwa kama vile wanafunzi si watu! Kwa mtaji huo... hata ng'ombe asiye na meno anaweza kukuuma! - simply in response to a natural desire to survive! Ukiwa hutaki kuumwa na asiye na meno... usijaribu kummbana kwenye kona - na usifanye kitu kitakachotishia uwezekano wake ku-survive!
    Kwa sababu ya hii nadharia, si ajabu then kuona kuwa: katika jamii yoyote... ukiona sehemu ya jumuia au kikundi fulani cha jamii kinaamua kufanya uasi - basi ujue kuna uwezekano mkubwa kuwa chanzo zha matatizo ni kushindwa kwa uongozi kuongoza vizuri na kwa haki. Kazi ya kiongozi ni kuongoza njia, kutoa mwanga wa tunakoelekea, kuonyesha na kutahadharisha uwepo wa mashimo, vikwazo na mitego iliyopo njiani n.k.

    Afrika kwa ujumla... shida inayotukabili si watu, si ardhi... na mara chache sana ni siasa mbovu. Shida kubwa ni viongozi wabovu!
    Kiini cha kuwa kiongozi bora ni nia na utayari wa kuwa mtumishi wa wote. Hii ni ngumu sana kuiona miongoni mwetu. Wengi ya viongozi waliopo Africa sasa hivi hawana hiyo. Kwa walio wengi kuwa kiongozi ni kama kupata hati ya kuwa miungu wadogo! Kwa wengi, uongozi ni kama tiketi ya kujichumia matumbo yao na kunyanyasa wanaotakiwa kuwaongoza. Wengi wapo busy kujichumia matumbo binafsi kiasi kuwa wanasahau kabisa kujaribu kufahamu kinachoendelea huko mitaani kwa wasaka nyoka. Matokeo ni kutokuwa makini na yale yanayotokea miongoni mwa wanaoongozwa, na kutegemea kuwa "wataelewa tu".
    Once one lose touch.. there is no way wataweza kutatua matatizo yaliyopo - that is if they will even be aware kama kuna matatizo! Kitu kama "kunji" as bad as it may be - inaweza kuwanjia pekee ya kuweza kuonekana! Now - ni lazima iwe hivyo? Jibu ni hapana!
    Nilipoandika.. nilikuwa naweka mzigo mkubwa zaidi wa lawama kwa uongozi wa UDSM! Kwa nini?... kwa sababu wao ndio wenye mzigo wa kuonyesha na kutoa majibu ya matatizo yanayowakabili wanafunzi wao. Kunji ni reaction against what is perceived as an oppression of some sort!
    Ned

    ReplyDelete
  7. Njaa sio tatizo, inabidi serikali inunue vitabu kwanza na kuvijaza maktaba, harafu baada ya hapo ndio iangalie uwezekano wa kushughurikia njaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...