kitoweo kikipelekwa kuliwa. jamani nakaribisha tena picha zenu za matukio enyi wa ughaibuni na hata wa hapa bongo. nileteeni kupitia issamichuzi@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi

    Hii ni picha baab kubwa maana wale wanaharakati wa kutetea haki za wanyama wakiiona hii, lazima waje juu sana na au watoe zawadi kwa ukereketwa wako hu dhidi ya haki za wanyama.

    Huyu jamaa nadhani akiwafikisha huko anakokkwenda tayari kuku watakuwa wamesha kufa na au kulemaa kabisa. Hii ndiyo staili ya wauza kuku wengi bongo na au walaji.

    ReplyDelete
  2. Ama kwa hakika huu ni ukatili dhidi ya ndege, watetezi wa haki za wanyama Bongo mko wapi?

    ReplyDelete
  3. Ukatili dhidi ya wanyama...
    Haki za wanyama...
    Bado na matatizo na hii dhana. Japo utamchinja mnyama na kula nyama, kwani ni lazima kumlea kama vile hautamchinja shingo, nadhani ukatili ni kumchinja.
    Haki za wanyama zizuie kuchinja kabisaa...

    ReplyDelete
  4. hivi kweli na sisi wabongo tumeshafikia hatua ya kutetea haki za wanyama?
    Binafsi nafikiria tuko mbali sana na hilo, isipokuwa kama tunataka kufungua NGO's ya kutetea haki ya wanyama kwa minajili ya kupata pesa za 'donors'.
    Inatubidi kwa sasa tutetee haki za binadamu wetu ambao wanaishi chini ya haki hizo kwa kipimo chochote kile. Angalia mashuleni, makazini, mabarabarani na kwenye familia, huko serikalini ndio usiseme.
    Embu tuyaacheni haya mambo tuongelee mambo ya kweli kweli.

    ReplyDelete
  5. Jamani!

    Haki za wanyama Bongo zilikuwa zinatetewa mpaka mwanzoni mwa miaka ya 80. Kwa wakazi wa Dar mtakuwa mnakumbuka jengo la ofisi ya Idara ya Kutetea Haki za Wanyama Tanzania, TSPCA (Tanzania Society for Prevention of Cruelity to Animals). Ofisi hizo zilikuwa Mtaa wa Morogoro kwenye kona na Mtaa wa Alikhan, nyuma ya jela ya watoto, jengo la pili kutoka jengo la Umoja wa Vijana na jengo moja kabla ya Technical College. Ofisi hizi baadaye zilikuja kuwa ofisi Agriconsult na za ofisi za Marehemu Dr Aleksi Khalid wa Makondeko Investments na Shikamoo Jazz.

    Mimi binafsi nilikuwa nikienda ofisi hizo kuogesha mbwa kila Jumatano, kuwapigisha sindano mara moja kwa mwaka, na kuwaangalia afya zao. Huduma zote hizi zilikuwa bure mpaka mwishoni mwa miaka ya sabini zikaanza kuwa za kulipia.

    Kwa hiyo suala la kutetea haki za wanyama siyo jipya kabisa nchini Tanzania. Na ninadhani kuna sheria kali sana zinazolinda wanyama wa kufungwa, wasio wa kufungwa, na wa porini lakini sheria hizi hazitiliwi mkazo.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  6. Kuku hao wakifika sehemu waendayo wamechanganyikiwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2006

    KWELI KUTOJUA SHERIA SIO KINGA YA KUTOHUKUMIWA!
    LAKINI ELIMU HII WENGI WA WATANZANIA HAWAIJUI,NANI ATAWAELIMISHA?
    MAADIU HAWA BADO TUNAO:-
    1.UJINGA

    2.MARADHI

    3.UMASIKINI

    UTATUZI WA HAYO BADO UPO MBALI MNO!KUJITUMA KWA ZIADA KUNATAKIWA KWA WATANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...