aliekuwa mwanasheria mkuu wa kenya na waziri saa chalez njonjo na mkwewa wakiwa na rafiki zao wakubwa jaji mark bomani na mkwewe siku ya harusi ya heri bomani na binti ottaru. njonjo alikuwa 'mtu bora' kwenye harusi ya bomani miaka ya sitini, na kabla ya hapo walienda kusoma sheria pamoja nchini uingereza na kuchaguliwa kuwa wanasheria wakuu wa nchi zao muda mmoja. jaji bomani sasa ni wakili wa kujitegemea, njonjo amestaafu na ni mzee wa kanisa nairobi. ila juzi alizua zogo aliposema jumuiya ya afrika mashariki ni nguvu ya soda na si chochote zaidi ya kuwa tembo mweupe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Unabii wa Njonjo kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki ulinikera. Kero ya unabii wake inakuja pale ambapo unaambiwa ni mtu huyu huyu alihusika sana kuiangusha ile ya mwanzo iliyokufa kifo kibaya mwaka 1977.

    Viongozi wa Afrika Mashariki, nashauri wampuuze.

    ReplyDelete
  2. Unaweza kuwa ulikereka na unabii wa Njonjo, lakini ukweli ndio huo hakuna kitu hapo. Huwezi kuunda shirikisho mahali ambapo kuna watu wanataka Urais wa maisha. Kama mnata shirikisho kwa jina sawa, lakini kama Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tu umewashinda na hali nyie ni ndugu mmeoa na kuoleana mtaweza kweli na Wakenya na Waganda wasowajua?
    Huku ni kukurupuka na kutaka sifa. Hayo mambo tunayodai tumeshasawazisha sijui ushuru wa forodha sijui nini tuwapi sasa? Mbona Kenya waligoma kuacha kutoza kodi ya asilimia kumi dawa zitokazo nje? Tuachane na Mentality ya kuamini mambo yatajipa tu, inahitajika kazi kweli. Afrika Mashariki haijawa tayari kwa shirikisho kamwe. Shirikisho linataka demokrasia ya kweli ambayo Afrika Mashariki haipo. Jambo muhimu kwa jumuia yoyote ni "Vibrant" Civil Society (Kiswahili cha Civil Society sikumbuki), ambayo hatuna. Tutabaki na viongozi wanaoipigia debe kwa sababu ya ulaji tu wakikutana kwenye mikutano.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa. Itachukua muda mrefu saaaaaana mpaka hizi nchi ziungane. Sidhani hata haya maongezi na so-called targets walizoweka wako serious nazo, mengi yatabaki tu kama symbol kwa muda mrefu. Hamna kuaminiana na huo ndiyo msingi wa muungano wowote. Hizi nchi zinatofauti sana kisiasa, na hata kiutamaduni. Tulidrop the ball tuliposhindwa kupata uhuru kama nchi moja.

    Mimi ningependelea kuona muungano unatokea hata kesho lakini hali halisi ndiyo hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...