
dk asha-rose migiro na waziri mwenzie wa mambo ya nje wa brazil wakitia saini mkataba wa ushirikiano wa kudumu wa nchi zao leo hapa brasilia. ushirikiano huo ni katika nyanja za uchumi, utamaduni na tekinolojia. tumeambiuwa leo kwamba jina na tarehe ya kuwasili kwa kocha wa timu ya taifa toka hapa vitatajwa wiki hii... ikiwa ni mojawapo ya matunda ya mkataba huo, na ahadi ya jk kutimia....


Michuzi kama wachezaji wenyewe bongo magoigoi,TFF na wizara husika wababaishaji na uozo umejaa tele hata kocha atoke mbinguni hatatufika mbali.Kocha atakuja tutamboa halafu anachukua mshiko wake na kuondoka.Lakini tukiwa makini kwenye wajibu kuanzia viongozi mpaka wachezaji basi hapo itakuwa ni kanyaga twende na hata raha ya kuwa na kocha mzuri tutaiona.
ReplyDeleteMMESOMA HIYO MIKATABA KWA UNDANI NA KUONA WATANZANIA WATAFAIDIKA NAYO AU NDO KUPIGA SAINI TU NA MLALAHOI WA KIBONGO KUENDELEA KUTESEKA NA MAISHA. TUNABIDI TUANGALIE HILI KWASABABU HAWA WATU KILA KUKICHA WANAPIGA SAINI TU NA MAFANIKIO HAYAPATIKANI NA KILA SIKU WATU WANABAKI KUWA MASIKINI.
ReplyDeletekwa hiyo Serikali imeamua kumwajiri Ceasar Leal kuwa kocha wa Taifa Staaz?
ReplyDeleteJamani kama sio kumuonea mama Migiro ni nini? mnamsainisha mikataba ya kabumbu?
ReplyDeleteHatutashinda footboli kwa kuemda kubembeleza kupewa kocha, tunatakiwa sisi wenyewe tumtafute kocha ambaye tunaona anatufaa na pale tutakapo ona hafai tunataka tuwe na uwezo wa kumunyesha mlango vile vile.
Mie naona ingekuwa rahisi kama tungeenda kumuuliza Joseph Kabila, au Angola kama wanafanyaje wao kufanikiwa ktk soka wakati sie tumelala. Mind you kabila ni kijana wetu kakulia Dar na Mbeya atatupa insider information.
Congo-Kinshasa pamoja na vita zao zoooote bado wanaenda Nations cup na sisi na amani yetu tumekalisha tu!
Zemarcopolo, unauliza eti uelezwe kilichomo kwenye mikataba! we hujui kuwa kwenye nchi yetu mikataba unaambiwa ni siri? sasa unashangaa siri kati ya nani na nani? wanakwambia kati ya serikali na serikali! sasa serikali ni nani? inamfanyia kazi nani? imepewa dhamana na nani? hapo ndio inakuja kazi kweli kweli.. sikatai kuna masuala ambayo yanaweza kuwa siri wakidai kuwa ni kulinda maslahi ya taifa. kama hivyo ndivyo sawa, lakini mara nyingi kwetu ni kwa kulinda maslahi ya viongozi.. tusijue wamekubaliana mambo yapi ambayo yanaweza kuwa na athari kwenye maendeleo. Nami nina hofu iwapo kweli hata waandishi wa habari wanaozunguka ziarani na mheshimiwa migiro wanafahamu kwa kina mkataba huo! sidhani! naamini watakuwa wameelezwa tu na viongozi walio nao ziarani halafu wao wakaandika... Sasa hivi bei ya mafuta duniani imepanda kutoka dola 20 na kitu hivi mwaka 2002 hadi dola 60 na kitu hivi sasa. BRazil na JApan wameamua kushirikiana katika uzalishaji wa miwa ili kuzalisha ETHANOL, nishati mbadala, badala ya kutumia petroli.. sasa sijui sisi tumewahi kuwaza hilo, au ndio mashamba ya miwa yanagombea soko la sukari na sukari ya magendo na ya ubora wa chini inayoingizwa nchini kimagendo kutoka nje! kazi kweli kweli... Tutafika siku moja!
ReplyDeleteA:SASA MICHUZI MUWAAMBIE WATANZANIA WAMWACHIE KOCHA AFANYE KAZI,ILE TABIA YA KILA SHABIKI KUWA KOCHA NA KUPANGA TIMU AHHNHA!
ReplyDeleteB;-1:NA WACHEZAJI NAO WAZINGATIE MAFUNDISHO NA WAKUBALI KUFUNDISHIKA,KALE KASIFA KA BONGO KASIWAFANYE WAMDHARAU KOCHA.
2:NA MAKOCHA WETU WA KITANZANIA HUU SIO WAKATI WA KUCHOMEKEA ILI KOCHA MGENI ASHINDWE KWA KIGEZO CHA KUTAFUTA UMAARUFU WAO BINAFSI,PIA NI FURSA KWAO KUJIFUNZA.
3:SERIKALI IMEAGIZA ALIPWE MSHAHARA,SASA ISIJE KUTOKEA WATENDAJI
WANAANZA NYODO;OOH!PESA KALIKWENDA,KAKARUDI!NO!
michuzi anayoandika mwenzetu hapo juu ni kweli?huu mkataba mmeona umeandikwa nini?
ReplyDeletehaa hivi kocha anakuja kwa mkata wa kuwekeana serikali na serikali. Hii tayari siasa, siasa na footbal vitu viwili tofauti. Kweli TFF watakuwa na sauti na huyu kocha kama anakuja kwa mikataba ya kisiasa. Mie yangu macho.
ReplyDeletembona mihogo haina afya?
ReplyDeletemkataba uliotiwa sahihi jumatatu si wa kocha bali ni kuundwa kwa kamisheni ya kudumu ya ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchumi, utamaduni na teknolojia.
ReplyDeletedr migiro hakuja hapa kutia saini mkataba wa kocha, bali katika kufanya hivyo, kupitia mkataba wa ushirikiano wa utamaduni (unaojumuisha michezo, tamaduni mbalimbali) ndipo njia imefunguliwa kwa kocha na wataalamu wa michezo mingine kupatikana.
naomba niseme tena. jumla ya mikataba miwili iliwekwa. wa kwanza ulikuwa ni kuzindua hiyo kamisheni ya kudumu ya ushirikiano baina ya brazil na tanzania, na wa pili ni mkataba wa ushirikiano kwenye uchumi, elimu, utamaduni na teknolojia.
soma hapa chini kwa ufafanuzi zaidi:
From Muhidin Issa Michuzi in Brasilia, Monday May 15, 2006
Tanzania and Brazil today launched a Joint Permanent Commission of cooperation (JPC) here, with both countries assuring the other of their political commitment to consolidating and further expanding the existing cordial relations.
Two agreements were signed at a colorful ceremony held in this Brazilian capital, the first being the formal establishment of the JPC, and the second was the Agreement on Technical Cooperation.
Major highlights of the two agreements include the promotion of economic, trade, cultural, technical, scientific and technological cooperation.
The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr. Asha-Rose Migiro and the Minister for External Relations of the Federative Republic of Brazil, Mr Celso Amorim, signed the agreements on behalf of their respective Governments.
Dr Migiro expressed the hope that the areas in the JPC would serve as a catalyst for cooperation in the various social, cultural and economic spheres.
“The enhanced cooperation between Tanzania and Brazil will not only be beneficial to these two countries but also it will build a solid foundation for continued south-south cooperation.
“The framework of cooperation is there what is needed now is to put a firm mechanism in place which is, indeed, the Tanzania-Brazil Joint Permanent Commission of cooperation we have signed today”, Dr Migiro underscored.
She assured her Brazilian counterpart of Tanzania’s political commitment at the highest level, and at the same time forecasted rising economic ties and steady cooperation growth as was the case in the 1980s up till the early 1990.
The Minister also guaranteed her Brazilian counterpart that Tanzania would open her embassy in this country in the near future, and that the processes towards that end were in high gear.
The idea of establishing the JPC was the brainchild of Mr Amorim during his visit to Tanzania in March, last year.
Initially it was agreed by both sides that the launching of the Commission take place in August 2005 but since Tanzania was heading for general elections, it was pushed forward to this year.
To show its commitment towards the landmark initiative, Brazil re-opened its embassy in Tanzania in August 2005 after it was officially closed in the early 1990s due to economic difficulties.
Meanwhile, envoys from SADC countries accredited to Brazil have hailed Tanzania’s decision to re-establish diplomatic ties with this South American Federative Republic, saying that the move was both a step towards the right direction and timely.
They have also committed themselves to assist Tanzania in opening up her embassy here as soon as the necessary arrangements were in place.
“The Brazilian are in the process of expanding relations with Africa and are looking forward to do more for the continent”, Mr Patrick Nandago, the Dean of African Diplomats here who is also the Namibian Ambassador to Brazil, said yesterday
Speaking at a dinner hosted last night by the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Dr. Asha-Rose Migiro, Mr Nandago said that Brazil was one country that Africa needed to look up as far as international politics were concerned.
Mr Nandago said that it was a blessing to have Tanzania as a diplomatic ally in Brazil, adding that this would further solidify SADC’s common objectives towards the region’s economic and cultural cooperation initiatives.
He said that more African countries have shown interest in forging diplomatic ties with Brazil, explaining that so far six of them were expected to open their embassies in this South American Federative Republic before the end of the year.
His Zimbabwean counterpart, Mr Thomas Bvuma, seconded him and offered whatever assistance Tanzania might need when the process of setting up an embassy here starts.
“The embassy of Zimbabwe opens its doors and extends a warm welcome to Tanzanian officials who will be here to set in motion the opening Tanzania’s embassy here”, said Mr Bvuma.
Their solidarity and that of other African envoys accredited to Brazil was obvious since the arrival of Dr Migiro, as most ambassadors of the 21 countries that have offices here were at the Brasilia International Airport to receive her.
African envoys here appreciate that despite the profile of Brazil in terms of its economic, political and social attributes is as a Third World Country, but its economy, which is highly industrialized when compared to other Third World Countries, qualifies it to be a member of the Developed Nations.
This soccer-crazy Federative Republic is composed of 26 states and one Federal District where Brasilia, the capital of the country, is situated.
Brazil is among the largest economy in the third world. Characterized by large and well-developed agriculture, mining, manufacturing and services, its economy outweighs that of all other South American countries and is expanding its presence in the world markets.
According to statistics, from 2001-2003 Brazil’s economy grew on average only 2.2% per year, as the country absorbed a series of domestic and international economic shocks.
That Brazil absorbed these shocks without financial collapse is a tribute to the resiliency of the Brazilian economy and the economic program put in place by former President Cardoso and strengthened by the current President Lula Da Silva.
The statistics also show that in 2004 Brazil enjoyed more robust growth that yielded increases in employment and real wages.
The three pillars of the economic program are the floating exchange rates, an inflation-targeting regime, and tight fiscal policy, all reinforced by a series of IMF programs.
However, the currency depreciated sharply in 2001 and 2002, which contributed to a dramatic current account adjustment; in 2003 to 2005.
The country ran record trade surpluses and recorded its first current account surpluses since 1992. Productivity gains, particularly in agriculture, also contributed to the surge in exports and in 2005.
Brazil surpasses the previous year’s record export level.
hiyo mikataba sio michezo tu yaani ni kila kitu kuhusu tanzania na brazil. je hiyo mikataba tunaisoma na kuilewa kwa undani? na je ina wasaidiaje watanzania kwa ujumla? sababu kila kukicha life ni ile ile hakuna mafanikio sasa sijui hiyo mikataba ni ya kwao (brazil) na viongozi wetu tu au sijui nini maana ni viongozi tu ndio wanazidi kuwa matajiri na wananchi wanazidi kuwa masikini.
ReplyDeletehapa UK au kule America kuna kitu kinaitwa freedom of information act ambacho kinampa uwezo raia kuiuliza serikali swali lolote na kuomba kuiona mikataba kama hiyo au kuona chochote kile sasa sijui tanzania kuna kitu kama hicho? mfano ninacho sema umetokea US ambapo raia wameomba serikali kuonesha video inayo onesha pentagon ikilipuliwa na magaidi na pia ilitumika ktk kuonesha mazungumzo ya mwisho mwisho ya abiria ktk ndege zile za 9/11 zilipo lipuliwa.
Wakati umefika kuweza kujua kila kitu wanacho saini maana ni miaka 45 sasa wanapiga saini tu na maisha ya mtanzania yanazidi kuwa masikini ambapo nilikuwa nadhani ya kwamba hiyo mikataba ingeondoa umasikini wa watanzania kwa muda huo wote.
Ni mimi mtu wa 1:16 AM
Ni kweli kabisa umefika wakati sasa hiyo mikataba iwe inawekwa wazi maana hata hatujui kinacho sainiwa katika hiyo mikataba tumekuwa tukiambiwa mkataba wa ushirikiano umesainiwa lakini details zinakuwa za serikali tu hii iishe na iwe inawekwa wazi si mmeshuhudia tunavyoumia kwenye madini.....
ReplyDeleteAta mimi nimeona katika suala la madini kwasababu mimi natokea maeneo ya huko huko utaona maisha ya wana kijiji bado duni sana. wakati umefika kwa hii mikataba kuwekwa wazi. Ongera Anonymous wa saa 1:16 AM na saa 5:07 PM kwa kuanzisha mjadala na tuuendeleze.
ReplyDelete