uzalendo haukumshinda mtu jana staz ilipocheza na kuibanjua bukina faso 2-1 neshno jana. huu ni upande wetu...oops! samahani...huu ni upande wa yanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. michuzi..
    naomba kama una picha ulizopiga ndani ya uwanja,namaanisha za wachezaji na special moments za hiyo mechi.
    Namiss sana na ningekuwa bongo lazima nienda kucheki hiyo mechi!
    thanks!

    ReplyDelete
  2. kuna jamaa wabongo wapo london wameanzisha hii web siku za karibuni inaandika mambo ya sports tu, Michezonet huenda wakawa seriuos

    ReplyDelete
  3. Bila shaka jana hakukuwa na kurushiana chupa za mkojo, maana jukwaa hilo wanakaa watu ambao ustaarabu bado kama miaka 2000 hivi iliwaufikie.

    ReplyDelete
  4. Mhhh wewe mtoa maoni hapo juu uliyegusia chupa za mkojo inaelekea hujawai kufika uwanja wa taifa kabisa hilo jukwaa hapo ni main standa kunakurushwa mikojo ni jukwaa la kijani sasa kama hujui si ukae kimya tu kwa nini kila wakati mnapenda kudandia vitu msivyojua, Mugo hawa ndio walewale wasiojua lakini wanajifanya kujua, jamani sio lazima kuchangia kila kitu na kakitka kuchangia sio lazima tutafute vitu hasi tu, tuchangie hata pale kwenye kutoa pongezi na kusifia.

    ReplyDelete
  5. Zedi,
    Nimekupata. Ni kweli Mtoa Maoni:Anonymous wa September 04, 2006 2:41 AM inaonyesha hajawahi kukanyaga uwanja wa taifa. Kama anaogopa kutoa kiingilio kwenda kuangalia mechi, basi hata ajitahidi kuhudhuria wakati wa gwaride ambako panakuwa hakuna kiingilio.
    Tujaribu kuchangia na kutoa maoni chanya! Watanzania tuache kuangalia kila kitu katika mtazamo hasi! Tubadilike sasa ili tuweze kupata maendeleo ya kweli.
    Ndugu Michuzi, tunashukuru sana kwa jitihada zako na kwa picha safi za matukio mbalimbali. Tafadhali tunakuomba uendelee na moyo huo.

    ReplyDelete
  6. ni kweli huyo aliyeongelea masuala ya mikojo inaelekea hajawahi kufika uwanjani. Lakini tumsamehe kwa vile hajui kwamba hajui.

    ReplyDelete
  7. Michuzi hii picha kweli imeonyesha hali ya uzalendo iliokuwepo uwanjani. Tanzania juu, polepole na pamoja tutafika tuu.

    ReplyDelete
  8. Huyo jamaa wa juu inaonekana kweli hajakanyaga taifa ni wale wanasikiliza stori za maskani halafu wanadandia, kaka au dada kwa taarifa yako, jukwaa hilo ndio watoto wa mjini wote hukaa, na karibu watu ni wale wale siku zote na wanajuana, na hupokezana matani kutokea pande zote mbili, hamna hata siku moja imewahi kutokea fujo pale na siku ikiwa hivyo basi ujue atakayeanza atakuwa mgeni kama wewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...