gwiji wa mashairi ya kiswahili mzee andenenga ama 'sauti ya kiza' akiongozwa na mjukuu wake kwenda kupanda daladala baada ya kughani redio ya taifa. mzee huyu haoni, lakini ukimwondoa mtu kama mathias mnyampala, shaaban robert ama juma akida, hakuna anayemgusa kwa ufasaha wa lugha ya kiswahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mambo ya aibu sana haya, huyu mzee tunamsikia tangu tukiwa wanafunzi, serikali haiwezi kuthamini kazi za mtu kama huyu na kumpa walau usafiri tu??

    ReplyDelete
  2. usanii bongo mgogoro tuuu........... ndo maana woote wanaishia njiani kwani hamna msaada wa kutosha kuendelea au kuendeleza fani... na pia kuishia kuibiwa kazi zao....

    ReplyDelete
  3. Tuachane na serikali, tujiulize mimi na wewe pamoja na wadau wengine tunaweza kufanya nini kumuondolea adha huyu mzee. Tuanze then tunaweza kuiambia serikali isaidie sehemu nyingine. Kwa mfano, tukichanga kununua gari basi tuiombe serikali imsamehe kodi. Tusingoje kuilaumu serikali kwa njia hiyo huyu mzee atendelea kuadhirika na sisi tutabaki tunapiga kelele tu. Nina imani ukitoa 10,000 na mimi 20,000 na wengine, kama vile tunachangia harusi huyu mzee tutakuwa tumeuthamini mchango wake. Let us show the way and the government to follow.

    ReplyDelete
  4. Huyu mzee anatoka kughani shairi redio ya taifa na si redio ya binafsi!! Aibu gani hii kwa watu wa MEDIA? Hii redio haiwezi kutoa usafiri kwa mtu ambaye anatoa kitu aghalabu kwa ajili ya jamii wakati magari hayo hayo utayakuta Kimanzihana yakisomba majani ya ng'ombe?

    ReplyDelete
  5. Wazee kama hawa wanastahili heshima yao wakati bado wako hai

    ReplyDelete
  6. Hao redio ya taifa ni wapumbavu au? Kwanini wasimpe usafiri baada ya hapo? Mijitu ina roho mbaya sana, ingekuwa vimada wao wamekuja kujuchukua matumizi ya nyumba ndogo ungeona inakabidhiwa land cruiser kuwarudisha nyumbani!

    ReplyDelete
  7. Bongo ukisha retire unatupwa pembeni kama ganda la muwa!

    ReplyDelete
  8. Ama kweli ndiyo mambo ya Tz haya,Baraza la mitihani kutumia Elimu katika kutungua na kutumia kitabu cha huyu mzee katika mitihani na elimu ya kiiswahili kwa ujumla bado tuu mpka leo huyu mzee hana hata baiskeli jamani

    Kweli tusiwanyonye watanzania elimu zao jamani inatia huzuni kabisa,kwanza haoni napenda sana kitabu cha cha MALENGA WAPYA kwa kweli maishir yake yameenda shule kabisa mungu atakukhafu mzeee wangu,mwisho wa dhuluma ipo!

    ReplyDelete
  9. Wanangojea afe kwanza, halafu tusikie "ameacha pengo lisilozibika"

    ReplyDelete
  10. Jamani hii ni aibu gani--huyu mzee ananiuma utafikiri baba yangu mzazi au babu yangu.Mmmhh Tanzania yetu hii.Michuzi mimi niko radhi kuanza kumchangia huyu mzee kwa ajili ya usafiri wake na serikali walau japo huo usafiri iusamehe kodi.Angalia possibility then wakilisha ujumbe humu humu kwenye Bulogu yako tutaanza kumchangia mpaka atapata usafiri wa kwake mwenyewe.

    Tunachotaka ni Benki akaunti na routing number ya hiyo benki na sisi tutajikakamua tu.Huyu mzee mchango wake mimi nameukubali katika kutujenga sisi Watanzania.

    ReplyDelete
  11. Michuzi, sema hakuna anamuweza kwenye ushairi wa Kiswahili, sio ufasaha wa Kiswahili. Unamlinganisha mtu mmoja na wengine milioni 40 ambao hujawasikia wote wakizungumza Kiswahili?

    Sijui hata kama unanielewa!

    ReplyDelete
  12. Michuzi yuko sawa kuhusu ufasaha wa huyu mzee. Hao watu milioni 40 wamejitokeza kudhihirisha vipaji vyao ktk jamii? huyu mzee mchango wake unaonekana. Mtu anaweza akawa na Phd ya lugha na asiwe fasaha. Tusipinge tu mradi tunapinga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

    ReplyDelete
  13. Suala si kumpa gari. Ingepasa baada ya huyu Mzee kufanya kazi yake huko RTD, angepewa usafiri wa kumrudisha nyumbani. Ninaamini kuwa RTD ina magari kadhaa ambayo yanaweza kufanya shughuli hiyo!! Bongo bwana...we acha tu!!

    ReplyDelete
  14. Mzee Andanenga alikuwa jirani yangu Kinondoni Shamba miaka hiyo ya zamani na ninaamini kabisa bado anaishi pale pale Kinondoni Shamba katika mazingira magumu ya maisha wakati akiendelea kulitumikia taifa kila kukicha bila kuchoka.
    Naungana na wanablog hapo juu kwamba lawama ni lazima na pengine ingekuwa vyema kumuenzi mzee wetu wakati akiwa hai na hakutakuwa na maana hata kidogo uhai wake utakapotoweka ndio watu waanze kusema pengo lake halitazibika.
    Pengine ni vyema sisi wenyewe kama wananchi kuipa serikali fundisho la kuenzi "hazina ya nchi yetu" kama mzee wetu Andanenga!
    Mimi nina imani kubwa kabisa kwamba sisi kama wanablog tunaweza kumchangia babu "Sauti ya kiza" si lazima kwa suala la gari lakini hata katika suala la kukidhi mahitaji yatakayomuwezesha au kumrahisishia kazi zake za uandishi wa tungo za mashairi na pia usomaji wake.
    Tukumbuke mzee huyu ni kipofu, upofu alioupata akiwa mtu mzima mwenye mke na watoto. Nahisi mbali ya uandishi hana kazi yoyote inayomletea kipato,basi hima hima tukubaliane kumsaidia mzee wetu!

    ReplyDelete
  15. Nyie kweli mliotoa wazo la kumchangia apate usafiri mnanichekesha.. hivi kweli mzee huyo mkimuangalia hata pa kulala panaeleweka kweli... na hata akipata usafiri si utaishiwa tumiwa na wanawe au wajukuu cha msingi ni MICHUZI afuatilie kwanza anapoishi ni pa hadhi aliyompa hapo juu???? Na jee wananchi sisi wenye usongo tunawezaje kumkomboa walao aishi kwa kiwango kinachoeleweka kwa maisha yake yaliyobaki??? SWALA LA USAFIRI LITABAKI HAPOHAPO HAO WANAOMKARIBISHA KUIMBA HUKO STUDIO WAWE RESPONSIBLE KUMCHUKUA NA KUMRUDISHA NYUMBANI KWAKE SIO KUSINDIKIZWA NA MJUKUU NA BAHASHA MKONONI.... KWANZA SI AJABU HATA HAWAMLIPI KITU MZEE WA WATU ANAENDELEA KUJITOLEA.... KWELI TANZANIA EEEEEEEEEEEEEEEEE YAPENDEZAAAAAAAAAAAAAA MJE MUONEEEEEEEEEE TUNAVYONYANYASANAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  16. Maoni ya wana-blog hapo juu (japo mengine ni ya jazba) yanaonyesha moyo walionao watanzania wa undugu, ambao wakati huu wa soko huria undugu unaliwa kilauchao.

    Nakubaliana kabisa na wale wanasema haki za wasanii zilindwe na pia wazo la kupata akaunti ya Sauti ya Kiza ilitutoe vimchango vyetu.

    ReplyDelete
  17. Michuzi nimerudi tena kuendelea kuboresha hoja ndani ya blogu. Kitu kikubwa na cha msingi ni TUACHE KUPIGA KELELE KWA KUILAUMU SERIKALI INAMFANYIA NINI JUU YA MCHANGO WAKE KWA TAIFA BADALA YAKE TUJIANGALIE SISI TUNAMUENZI VIPI HUYU KWA KUJUA NA KUUTHAMINI MCHANGO WAKE. Kwa umoja wetu tukiunganisha nguvu tuna weza kuonyesha tuna weza badala ya kuishia kulalamika wakati wote. Hebu chukua sekunde 30 fikiria katika watu 100 kila mtu akichanga wastani wa TShs. 10,000.00 je hudhani nyumba yake kama ilikuwa inavuja tutaweza kuirekebisha? Haya shime tuamke tuongee kwa vitendo na wala si maneno. Nilitoa mfano tu wa kumchangia kupata usafiri kwa vile ujumbe uliotufikia ulikuwa unatuonyesha picha halisi na tatizo tuliloliona na vilevile jinsi gani ya kuishirikisha serikali. Nina imani matatizo aliyokuwa nayo ni mengi na wala hatuwezi kummalizia yote. Tunaangalia nini kina weza kufikiwa kwa wakati uliopo kutokana na ujumbe tulioupata. Haina maana sana baadae tukajitoa kumchangia baada ya yeye kuwa ameitwa mbele ya haki. Tufanye mambo sasa hivi kumpunguzia adha anazozikabili, kwani PAMOJA NA SHIDA ZOTE ANAONA MCHANGO WAKE KWA JAMII UNAHITAJIKA NDIYO MAANA ANAPIGANIA DALADALA AFIKE KUITUMIKIA JAMII NA WALA SI SERIKALI.

    ReplyDelete
  18. Kaka michuzi huyu mzee anakwenda Radioni kutoa mashairi ili watanzania tuweze kusikia sababu ni kwamba anajua watanzania tutapata ujumbe kupitia radio na sio mchango kwa serikali wala Radio Tanzania hii ni kwa wananchi, Kwa hiyo naungana na wadau waliopita tunakuomba bwana Michuzi umtafute tena huyu mzee afunguliw akaunti yake ili tuweze kuwasilisha michango yetu mara moja, Fanya juu chili ili ionekane amesaidiwa kweli na sio maneno matupu ndugu zangu

    ReplyDelete
  19. JAMANI HUYU NDIYE SHAKESPARES WETU WA TZ.KWANINI SERIKALI HAIFANYI JUHUDI YA KUWATUMIA WATU KAMA HAWA ATA KAMA WAMESTAAFU WAWE KWENYE BARAZA LA USANII TZ.KAMA WATOAJI WA USHAURI...ANDANENGA AU DIWANI YA USTADH IT WAS ONE OF THE DIFFICULT BOOKS I READ IN MY OLEVELS..NA UNAJUA KWAMBA KISWAHILI NI LUGHA NGUMU SANA I WAS ONE OF THE SMARTEST STUDENTS IN MY CLASS I MANAGED A C GRADE IN MY OLEVEL FINALS..KWELI HII NI AIBU KUONA KITU KAMA HICHI KINATOKEA!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...