Home
Unlabelled
miss dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
MTOTO UMEKAMILIKA,Ningependa ukaiingia miss Tanzania
ReplyDeleteHuyu ni Miss Tanzania au Miss India?
ReplyDeleteTuwekee basi hizi picha zake tumfagilie zaidi kaka michuzi kwa hapo bado sana mkuu wangu!!Lakini mbona kanaonekana kama KADOSI vile huyu mtoto!!!
ReplyDeleteacheni hizo twendeni na wakati ili mradi anawakilisha nchi yetu Tanzania anastahili sifa alipofika.HONGERA MREMBO
ReplyDeletemimi nakaona kama kahindi hindi vile, sijui wanzangu mnasemaje?
ReplyDeleteHata kama ni mdosi tatizo liko wapi? Mtanzania ni mtanzania tu.
ReplyDeleteSamahanini huyo ni miss dunia au miss Earth(mazingira) kwa jinsi wanavyomtambulisha
ReplyDeletemichuzi hakuna ubishi kwamba tanzania imeaaliwa walimbwende kama huyu, mashaallah.
ReplyDeletelakini bila umeme watang'ara kweli?hebu tusaidie kuchechea mijadala itakayowafanya wahusika watuletee maendeleo.
tunatamani umeme wa uhakika na maji yatiririke kila kibanda, kila kasri na kila kitinga!
Angekuwa mweusi kama Mbantu afadhali...ndo kuwakilisha huko!!
ReplyDeleteMdosi gania anaitwa Rachel? Acheni mambo ya ajabu jana.Hata UK iliwahi wakilishwa with one of this mashindanos na mtoto from east, tena Muisliamu. Pamoja na yooote wanayofanya,hawakupiga kelele. Uache sisi ambao Jamal alikuwa mjomba na mlezi shule tulizosoma kibao? Tuangalie mbali jama, tusiropoke tu!!!!
ReplyDeleteAHENI UBAGUZI,KAMA MTANZANIA NI MTANZANIA TU,HONGERA DADA!
ReplyDeleteDada anakula pilipili huyuuuu! sijawahi kuona, halafu anashushia na maziwa ya mgando
ReplyDeleteJamani kuweni na akili. Hata kama ni mhindi anaiwakilisha nchi yetu. Ingelikua hivyo basi marekani si kila miss wao angetakiwa kuwa Red Indians?Open your mind guys. GOOD JOB GAL.
ReplyDeleteMimi kama Mtanzania mwenye asili ya Kihindi na nikiwa mzaliwa wa kizazi cha tatu hapa Afrika, naalaani wale Wazawa wanaopenda kututukana na kutufanya kama kwamba Tanzania sio kwetu, ila tu ni nchi ya Wazawa na sisi tusiokuwa Wazawa ni wageni tu. Napenda kuwakumbusha wazawa wabaguzi kuwa Wahindi na Waarabu wa Kitanzania wanawapa kazi Watanzania kwa maelfu na wanasaidia kuendesha uchumi wa nchi kama Wazawa. Kuniita "Mdosi" ni sawasawa na kumwiita Mzawa "nigger". Mara nyingi Wazawa wanakuja juu sana kama wakibaguliwa na Wazungu ulaya au marekani lakini hawaoni kitu chochote kama wakiwabagua Watanzania wenzao walio na rangi tofauti na wao. Napenda pia kutoa shukrani kwa wale waliotupa mkono hapa kwa kutuona sisi Watanzania kwanza, na asili na rangi yetu pili. Ubaguzi upo upande wote, lakini kama tutakuwa na busara na kutunga sheria za kuthibiti ubaguzi wa aina yoye kwa wananchi wote, basi itakuwa jambo la busara na la kimaendeleo kwa jumuiya yote. Mimi nimechoka kuitwa "Mdosi" na "Mgeni" hapa nchini wakati nachapa kazi na nasaidia kujenga nchi na kulipa kodi kama Watanzania wengine. Wabaguzi wanatakiwa kwenda TRA kuona kiasi kani tunalipa kodi, Wazawa wangapi wanatutegemea sisi kuwavisha na kuwalisha. Kuna msemo wa Kiingereza " Treat others like the way you want to be treated". Kwa wale wanaotuheshimu hapa, natoa heshima kwao. Ahsante kwa muda wenu.
ReplyDeleteUnaona sasa? Hata hujui kwanini WAZAWA wanakerwa na wadosi. Maneno yako uliyoongea yalikuwa na mantiki mwanzoni, lakini baadae hali ya udosi ikajitokeza katika maneno ya arrogance kuwa "mnatuwaisha na kuwalisha" Wazawa. Je ni kweli kuwa Wazawa wanapiga foleni kwenu kuomba chakula na nguo, na sio kama mnawatumikisha na kuwanyonya ndio wapate riziki yao? Katika jibu lako unajidai kuwa wewe ni Mtanzania halisi, lakini hapo hapo umejigawa katika kundi kuwa kuna 'sisi' na 'ninyi'. Hata hivyo tunaweza kukusamehe kwa kusema hujui unalolisema, maana hali hiyo imejengeka katika undani wako (subconscious). Fikiria kwanza maneno yako kabla ya kuandika ama sivyo utaharibu badala ya kujenga!!
ReplyDeleteMimi ni anony wa 3:39:54 na namjibu anony 5:15:00. Kwanza, sijaandika kumtukana Mzawa yoyote hapa, na sijataka kujigawa kama anony anavyodai, bali kutoa point kuwa sisi kama "wageni" au "wadosi" tunaajiri, tunalipa kodi, na tunasaidia maendeleo na uchumi wa Tanzania. Suala la kuwavisha na kuwalisha Wazawa sio maana yake ni ya kutowaheshimu wafanyakazi bali ajira wanayoipata kwetu kama "wadosi" inawalisha na kuwavisha. Pointi yangu ni kwamba tunategemewa kiuchumi na maelfu ya Watanzania.
ReplyDeleteJapokuwa sijajigamba mwanzo, lakini napenda kumfahamisha anony hapo juu kwamba nina elimu ya juu ya Kiuchumi (Master's) na nimerudi kwetu kuwajibika. Undani mwangu ni clear, kweupe, ninatoa ajira kwa yule anayeweza kufanya kazi siangalii rangi wala kabila ya Mtanzania. Pia, sijaona wafanyakazi wengi wa nyumbani wanaolipwa kima cha chini na Wazawa, wengi wao wananyanyaswa na kulipwa mshahara mdogo kwa kuwa wanatoka shamba. Kama kuna mdau anabisha kwamba hamna mfanyakazi wa nyumbani anaolipwa mshahara mdogo na Mzawa mwenzake naomba ajitokeze.
Wazawa wameshindwa kuendesha uchumi wa Tanzania, ndio maana bado asilimia 40 ya bajeti tunawaomba wazungu watusaidie, miaka 40 baada ya uhuru. Wagonjwa wetu wa moyo tunawapeleka udosini kuwatibu, barabara zetu zinajengwa na Wajapani. Tukitaka elimu ya juu, lazima tuwaombe nchi mbalimbali kama India, Uingereza, Japan na Marekani lakini hatuna hata elimu ya kimataifa ya biashara katika chuo chetu kikuu cha Dar, hapo Mlimani.
Kama anony bado anakerwa nasi basi afanye kampeni ya kuwafukuza "wageni" na "wadosi" wote Tanzania ili aweze kuiendesha Tanzania anavyopenda. Ninasubiri fikra zake na elimu atakayetumia kuleta maendeleo Tanzania kwa kutimia nguvu moja ya Wazawa. Historia imeonyesha kwamba inawezekana , lakini huenda ikachukua miaka 200 kufikia maendeleo ya nchi zilizoendelea. Itakuwa jambo la busara kuanza na umeme na maji safi, kwa kuwa bado hatuna baada ya miaka 40 ya uhuru na maendeleo.
Aluta continua.
hawezi kuwa mnyakyusa huyo au muha?noooo
ReplyDeletentuyabaliwe mlisema mrundi kama si mnyarwanda hapo je????
ReplyDeleteWewe mdosi hapo juu saa hizi unachemsha mwanzioni nilikuona unapoint laiki ssaa basi. Don't bring up your stupic education. Why don't you take your education to your mother land. Huko India nimefika na ninajua yote ndio maan hata hamtaki kurudi kwenu. Umerudi nyumbani wapi ni nyumbani? Unazania basi wewe ndio tunakutegemea sanaaaaaaa. jinga tu. Mbona basi hamkai TZ mnataka passport zetu halafu mnaishia Canad, USa and Europe. Yeah! Kila muhindi nchi za nje ni mkenya au mtanzania...sasa kama mnapenda sana nchizetu basi mkae hapo hapo tu mara mnapokua raia... Kumbe mnatafuta njia ya kuwaingiza hizi nchi ambazo haziwataki tena. Kwasababu ukiomba visa kwenda nchi hizo hapo juu waiting list ni more than 12 months lakini kwa nchi zetu poaa tu. Kwa hiyo manishi tusitanuliane bwana. Heshima ya wazawa weka mbele. nimeishi nchi za watu na nilikua naheshimu wazawa pia....Thanks
ReplyDeleteWahindi wasilaumiwe.Waswahili na ninyi mmezidi kila mnaposoma mnawaza kuajiriwa ndio maana mnaangukia mikononi mwa watesi wa kihindi.Mhindi hapendi kuajiriwa na mtu.Hapendi kupangiwa mshahara au bei.Waswahili mnapenda kwa sababu kujiajiri ni wavivu na si wabunifu kwenye stadi za maisha.Bila wahindi nchi hii haiendi ndio wanaongoza kwa kulipa kodi wakifuatiwa na waarabu na wapemba.Hata hiyo elimu ya bure mnayosoma na hospitali mnakotibiwa asilimia kubwa ya pesa zinatoka kwa wahindi na waarabu kwa njia ya kodi.Nyie waswahili koko mtukome wahindi tukiondoka mtavaa magome ya miti na kula mizizi pori.
ReplyDeleteMimi ni Anony 6:16:22. Kwanza nalaani maneno ya kutukanana, yawe kutoka kwa mzawa au mhindi mwenzangu. Msomi yoyote anaongea kwa pointi sio kwa kutumia hasira au chuki lasivyo watu hawatamwelewa, ataonekana tu kama mwehu. Anany hapo juu anadai nisijidai na elimu yangu wakati naambiwa sijui ninaloongea. Lakini sipingwi na point yoyote kuhusu hali mbaya ya uchumi Tanzania kutokana na viongozi wabovu. Mimi siwezi kuenda India kwa kuwa napata riziki yangu hapa Tanzania, nyumbani kwangu. Sasa kama huyu Anony anataka kunifukuza, basi afanye hivyo kama nilivyosema mwanzo. Lakini pia awaambie Wazawa wenzake wanaofanya kazi Ulaya , Marekani, India na nchi nyingine warudi makwao kwa kuwa wanafaidi maisha huko kuliko yeye. Nadhani mnaona upuuzi wa pointi yake ya kudai najigandisha Tanzania kwa manufaa ya pasipoti ya Kibongo, kitu ambacho ni haki yangu kama mzaliwa. Pili Anony hapo juu hajasoma kutosha kujua kuwa dunia siku hizi hazina pasipoti wala upendo wa nchi kwa wafanyabiashara wa kitaifa. Nikitaka kesho ninaweza kuenda Kanada au Marekani au nchi yoyote ninayopenda kwa kuwa nina elimu na fedha za kutosha. Ndio maana Wazawa wengi hasa madaktari na manesi wanakimbilia Uingereza na Afrika Kusini kutafuta riziki. Kanada inachukua mtu yeyote mwenye elimu ya chuo kikuu na elfu 10 dola. Mbona hasumbululiki kuona Mzawa anadandia nchi ya watu lakini ana hasira kali Mtanzania wa Kihindi akiajiri au akiishi Tanzania? Je, huu ni wivu au ameathirika akili hajui analolisema? Pia, nitamwoomba sana anony asome uchumi wa India, nchi bado ni masikini lakini ipo mbele mara 100 dhidi ya Tanzania. India inalima mazao yake na inatoa misaada kwa nchi nyingine za kimasikini kama Tanzania. Anony ukipata ugonjwa wa moyo usistuke ukipelekwa India na serikali kutibiwa. Kama ameishi huko angejua hayo nayosema. Umasikini upo lakini pia kuna watu milioni 300 wenye uwezo mkubwa wa kifedha na ndio wanaoendesha uchumi kuwa juu. Maprofesa wa kihindi na madaktari wao ni maarufu duniani kote. Kwa nini nisirudi huko? Kwa sababu nina biashara ya maana nchini kwangu na nimeridhishwa kimaisha kama Watanzania wengine walioaamua kukaa kwao, kwa hali na mali.
ReplyDeleteAnony, nchi changa na masikini kama Tanzania inategemea watu kama mimi. Nina elimu na fedha ya kuendesha biashara na kuwapa watu ajira na kuwapa serikali kodi. Kama kosa ni rangi yangu na tabia yangu basi unifungulie mashitaka ya kuvunja sheria, au ya kubagua, au ya kutolipa kodi. Lakini huwezi ukaropoka tu kama mwandawazimu kwa kutumia asili yangu kama kisingizio cha umaskini wa Tanzania au kwa watu kunyonywa katika biashara za wahindi. Kama kuna wanyonyaji wa haki za binadamu ni viongozi wetu walioshindwa kutupa maji safi, elimu na umeme, viongozi wanaonuka rushwa, viongozi wasiojali maisha ya wenzao. Namshauri Anony hapo juu asiwe na tabia ya ubaguzi na chuki.Viongozi wake wako Kanada kuomba misaada na vitega uchumi wiki hii. Tanzania bado inadaiwa dola bilioni 8 mpaka leo. Je, ana mpamgo wowote wa kusaidia kulipa hiyo deni au atakaa tu domo wazi katika internet ya mhindi akitukana mlipa kodi wa Kihindi huku nchi yake inazidi kudidimia kiuchumi? Aluta continua.
Anony wa Dec.5, 8:35 acha matusi. Tunawategemea Wahindi? nenda India kama utawakuta watanzania wamejaa kama mlivyojaa nyinyi hapa. Wahindi ndo mnaongoza kwa rushwa. Mnatumwa uarabuni kama manamba. Ndio maana Idi Amini aliwatimua baada ya kuona madhambi yenu, alafu hamkwenda kwenu India mkakimbilia Uingereza kuwa wakimbizi. Hivi mnaogopa nini kwenu? Wahindi wabaguzi na mna roho mbaya. Kuwa na masters umejiona umesoma saaana mwizi we, watu tuna Phd.
ReplyDeleteHongera kwa Ph.D yako anony hapo juu, nadhani hii itakuwa jibu langu la mwisho hapa, sioni mtu anatoa pointi bali kutukanana tu. Kuna Watanzania zaidi ya 10,000 wengi wao ni wakimbizi feki kanada, pia wengi wapo Uingereza. Mbona huambii hawa wazawa warudi makwao? Je, unafikiri hawa Watanzania hawateseki kama wahindi wanaofanya kazi uarabuni? kwa taarifa yako, kuna wabongo chumgumzima wanafanya kazi arabuni pia. So pointi yako ni nini? Swala ni uzaliwa.... hapa unasema niende kwetu, sioni jibu la maana ila ubaguzi na chuki dhidi yangu. Pili, Kama umefika Uganda au unafuatilia siasa ya Uganda utajua kwamba Museveni kawaomba msamaha Wahindi na kuwaomba warudi kutega uchumi Uganda. nyumba na biashara zao zimerudushwa kwao. Pia, hawa wahindi walikimbia uingereza kwa kuwa walikuwa raia wa Kiingereza. Sasa, kama wewe ukifukuzwa Tanzania ukiwa na uraia wa Uingereza, ni common sense kuwa utarudishwa Uingereza, sijui hiyo Ph.D yako ni ya kwenye subject gani, naona tu wewe ni sawa na wagabuzi wengine hapa, huna pointi bali chuki. Sisi Wahindi toko hapa milele, wabaguzi mpende au msipende.
ReplyDeleteSi tunajua Canada wako Wahindi wengi na si watanzania. Tanzania ni nchi ya Amani kwa hiyo haina wakimbizi kiasi hicho nje ya nchi. Labda hao watakuwa Wasomali, Warundi,Wanyarwanda, n.k. wanajipakazia tu utanzania kama wanavyojipakazia wahindi.
ReplyDeleteKwa nini msiukubali ukweli Kuwa sis wahindi ni wa maana.Elimu ya bure alikuwa akitoa Nyerere pesa zilikuwa za Wahindi maana wakati huo waswahili walikuwa wamejaa kwenye siasa na ajira,Wahindi wakiwa wamejikita kwenye viwanda na biashara wakilipa kodi kubwa.Hata nyumba za National Housing mnazosema wahindi wamejaa wakipanga hazikujengwa na waswahili. Ni wahindi tulijenga kwa pesa zetu mkazitaifisha.Hivyo tuna haki ya kuzikaa sababu jasho za babu zetu zimo humo wakati jasho za babu zenu hazipo sababu walikuwa vijijini wanatega mitego ya panya pori wa kula.Bila wahindi hizo PHD mtakuwa hamna pa kuzifanyia kazi sababu serikali haitakuwa na uwezo wa kulipa mishahara yenu.Na sababu ninyi si wabunifu mtakufa njaa na PHD zenu msipoajiriwa na serikali au wahindi. Ndio maana kutwa ni kupiga kelele serikali iwaongeze mishahara.Kwa mhindi mwenye PHD huwezi sikia anapigia kelele mshahara upande he knows what to do.It is a shame for PHD holder to behave like a junior na kukosa kuwa innovative na kuandamana barabarani eti anadai aongezwe mshahara.Waswahili wengi ni wajinga tu hata wawe na PHD.
ReplyDeleteDuh, we muhindi unadharau sana.Halafu unaonekana una muda kweli wa kujibu, maana majibu yako ni gazeti.Mi nakushauri uende ITV upeleke machungu yako taifa zima wakuone. Sidhani kama wewe ni director wa kampuni yako utakuwa na muda wa kuandika vyote hivyo kwenye blog. We ni kachero tu, wale wahindi wachafu wa kariakoo.Wale wanaokula dengu kila siku. Upende usipende ubaguzi upo dunia nzima hata ujieleze vipi hauwezi kuisha. Mradi unanywele za kuteleza wewe ni muhindi tu hata kama babu zako walijenga nyumba za NHC. Huwezi kuwa mTZ hata sikumoja. Na nyie mnabaguliwa kwa sababu ndani yenu tu kuna ubaguzi, utasikia ooh mimi suni,or mimi hindu. Wapi na wapi bwana? Kama nyie watanzania mbona hamuoani na watanzania asilia? tena mko radhi mtu awe na demu mzungu au jamaa la kizungu kuliko mbongo. Halafu mkiitwa wahindi mnakasirika. Saga chupa unywe kama una hasira. Hatukatai kama michongo yote mnayo nyie, sawa lakini sio kihiivyo. Kwa hiyo acha dharau dogo. Ohooo.
ReplyDeletewewe unajiita muhindi hapo juu unamapungufu mengi ktk maandishi yako!moja hakuna nchi haina ubaguzi wa rangi kama tanzania pili hakuna msingi wowote unaozongumzia hapo kama wahindi kubaguliwa basi ni arabuni munabaguliwa lakini sio hapa Tanzania.kwa hio nakuomba kijana uwe unaangalia nini onachozungumza
ReplyDeleteni kosa kuzua jambo