
chaaaaz hilary wa bbc akikupa vitu laivu toka uwanja wa milenia huko kadiff ile juzi asenoo ilipolala 2-1 kwa chalsii fainali za kombe la carling kap. huyu bwana pamoja na kupromoti sana macharanga hapa bongo pia anasifika kwa vikolombwezo vya 'majalo', 'namna gani pale', 'vituuuz' na kadhalika. hakika wabongo twatembea vifua mbele kwa umahiri wa hawa jamaa. tumshukuru mtu wa pale nyumba ya kichaka landani aliyezua wazo la kututangazia mipira ya ukerewe laivu kwa kimatumbi...
Umenikumbusha mbali sana kuhusu huyu Chaaz... hasa utangazaji wake.
ReplyDeleteNakumbuka hiyo slogan ya "hatumwi mtoto dukani...." aliitoa siku ya Simba v. Stella Abidjan dakika 3 kabla ya goli la kwanza la Boli Zozo, alipoisema hii slogan ilikuwa dk ya 15 goli likaja dk ya 18! Alianza da Jua ni kali sana saa 9 alasiri... hatumwi mtoto dukani na akitumwa soda anakunywa hukohuko...
Na ni siku hiyohiyo slogan ya "uzalendo umenishinda.." iliimbwa na mashabiki wa yanga baada ya Simba kufungwa goli la pili kwenye dk ya 32 kipindi cha pili...Sekioni Kitojo alikuwa kwenye 'maiki'. Yanga waliombwa kuwa na uzalendo siku hiyo ili kuishabikia Simba, lakini baada ya goli la 2 Yanga wakaimba ... uzalendo...umenishinda!
Kwa kweli, huyu jamaa pamoja na Dunstan Tido Muhando ni watangazaji wa kujivunia kabisa Tanzania. Charles Hilary kwa hakika pamoja na kwamba ana kipaji cha utangazaji, lakini pia ni rafiki mzuri wa kila mtu. Nyota yake iko juuu sana na inawaka sana! Kila la kheri baba
ReplyDeleteKwa hakika wadau naungana nanyi,Charles amejaliwa kipaji cha kutangaza soka,maana mimi alinifanya hadi niwe namuigiza primary enzi miaka ya 90/91 wkati wa fainali za kombe la africa mashariki na kati,nakumbuka ilikuwa mechi kati ya simba na sport club villa ya uganda,na simba walishinda goli 3 sifuri kama sikosei, goli la tatu likufungwa na zamoyoni mogella,charles alimsifia zomoyoni akisema ni goli la sita tangu mashindano haya yaanze kwa zamoyoni mogella -golden boy,aisee nakumbuka nilikuwa darasa la sita, na wachezaji wa simba walikuwa Iddi pazi,Rafael Paul,Twaha hamidu,Jamhuri kiwhelo,Frank kassanga bwalia, Method mogella,Issa kihange,Hassan hafif-kocha mchezaji, Bakari iddi,Gebo peter,Itutu kigi, na Zamoyoni mogella,wengine Hassan banda, Makenzi ramadhani,Hamis gaga,Mavumbi omari na wengineo, hapa soka ilikuwa tamu sana bongo,namimi nilikuwa darasa la nne enzi hizi,da hatari kweli,big up charles.
ReplyDeletemambo si hayo bwana
ReplyDeletesio RADIO 1 kule weeee hakuna kutoka wala nini JIBABA ULIKUWA UMECHOKA ILE MBAYA maneno BBC bwana!
Halafu tazama raha ya ulayahakuna kwenda kupata kilauri kwenye baa za uwani au kwenye vumbi kule sinza...maneno ukitoka the strand basi unajichanganya JDWEATHERSPOON nje ya Holbon station
ukitoka hapo unachukua gazeti lako la THE LONDON PAPER kisha unajimwaga kwenye Central LIne Mpaka Mile end
Ulaya kuzuri na nakushauri undelee hivyo hivyo nyundo zako 20 ndio unarudi bongo
safi sana
Bwana Charles mimi ananikumbusha zile za 'wapenzi wasikilizaji, hapa uwanja wa taifa watu ni wengi, wengi, wengi kwelikweli'!!!
ReplyDelete