Ukimuona kwa sura, ni msichana mzuri mwenye macho ya kuvutia, lakini masikini hana raha ya maisha!
Mtoto Sofia James Mwiga (17) mkazi wa Manispaa ya Tabora nchini Tanzania anaishi kwa mateso kufuatia ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu hali iliyomfanya ajione mpweke machoni mwa jamii huku akishindwa kuanza shule.
Licha ya baba yake kumtafutia matibabu kwa zaidi ya miaka 10 bado hajafanikiwa kwani kila Daktari anayemfanyia uchunguzi hutoa maelezo kuwa hapa Tanzania hawezi kufanyiwa oparesheni isipo kuwa nje ya nchi ambako kuna Wataalam na vyombo vya kitabibu vya kisasa..
Kutokana na umasikini alionao baba mtu ameshindwa kumsaidia badala yake amebaki akisubiri miujiza ya mungu ishuke pengine atapata mfadhili atakaye weza kumsaidia kupata matibabu hivyo anawaomba wasamaria wema popote duniani waweze kumsaidia kuokoa maisha ya mtoto wake huyo.
Hivi sasa mtoto huyu yupo katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar es salaam akisubiri atakayeweza kujitokeza na kumsadia kupata matibabu sahihi nje ya nchi, kwa mujibu wa mdaktari, anahitaji operation ya kuondoa nyama hizo zilizozidi.
Mungu kama amekupa, basi kumbuka na wenye shida….naamini kuna mtu hapo anaweza kubadili maisha ya msichana huyu kwa uwezo wake mola!
namba ya simu ya baba mzazi wa msichana huyu ni +255 753 916 690

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. pole sana sophia, mwenyenzi mungu akusaidie inshallah. na kumbuka mwenyenzi mungu yuko na wewe na atakulipa malipo mema mbeleni. Ni mtihani tu mshukuru mungu na uzidi kumuomba. kuna siku mwenyenzi mungu anaweza kuleta miujiza yake ukakuta uko kwenye furaha tele.

    ReplyDelete
  2. Pole sana, tafadhari tafuteni hospitali India na gharama zote ziandikwe humu kwenye blog. tumieni taarifa za hao madakitari wa mwanzo kuwapa taarifa wenzao wa India na leteni hapa tuzione.

    ReplyDelete
  3. JAMANI KWELI KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA. POLE SANA MDOGO WANGU.

    KUSEMA KWELI SIJUI KUHUSU TIBA NA NJE MADOCTOR WA BONGO WANAPOSEMA NI WAPI. MIMI NIPO UK NA SI MUDA MREFU NILIONA DOCUMENTARY KWENYE TV KUHUSU MWANADADA AMBAYE ANA UNGONJWA HUO NA AMEISHI HIVYO KWA MIAKA MINGI NA KUWA HAKUNA TIBA. ANYWAY LABDA AJARIBU... POLE ZAKE

    ReplyDelete
  4. Oh my god this is very sad.Yeah watu inabidi tufanye harambee aisee tumsaidie huyu binti.

    Mwanakijiji,Dues!!....where is your vyombo vya habari?

    ReplyDelete
  5. vile vile naomba bandikieni picha moja ya kifamilia na mgonjwa akiwepo ili tuweke katika blog mabali mbali na kutengeneza matangazo ya kuomba msaada hapa Marekani. wekeni account no yenu au Mwakilishi wenu huku Marekani. si mbaya kama mtaniteuwa mimi ili niwawakilishe. Nitafanya niwezalo hata kusimama bara barani kuomba pesa. Cha msingi kwanza tafuteni gharama za matibu na jina la hospitali na anuani yake. Nitumieni email kwa kutumia MWAKI66@YAHOO.COM.(mwaki66@yahoo.com) ANDIKENI KWA KUTUMIA HERUFI KUBWA. hilo jina la Nyakyusa ni kwa ajili ya Blog tu baadaye nitawapa jina langu kamili. mimi nina isha Marekani.
    Nyakyusa.

    ReplyDelete
  6. Pole Sana Dada Sofia, tunafundishwa kumshukuru M/Mungu Kwa Kila Jambo Linalotufika!...Jaribuni Kuwasiliana Na Taasisi Hii ya Facing The World kwa # +442073520052 website www.facingtheworld.net au e-mail info@facingtheworld.net waelezeni kuhusu ungojwa huo mkiambatanisha na picha na watamsaidia Sofia.

    Izz Wa

    ReplyDelete
  7. Pole sana dada yangu, yaani kweli dunia hujafa hujaumbika, mungu atakusaidia tu, hii inanikumbusha pale usagara sec kulikuwa na dada mmoja tunasoma nae alikuwa mzuri kupita wanafunzi wote wa kike (nganya), ila alikuja pata ugonjwa wa matende, japo watu wanasema alichukua mume wa mtu lakini mengi yatasemwa. Hapa kilichopo ni kumsaidia sophie matibabu ya kisayansi najua mpaka kajitokeza hapa wazazi watakuwa wameshamaliza njia zote za kijadi na kizungu kwa bongo kilichopo hapa ni kupata matibabu nje ya nchi. Kama watu wanaweza kubadili sura na maumbile yako basi hata sophie ana matumaini makubwa ya kuishi maisha ya raha na furaha, jamani shime shime. Ila kama wadau walivyosema hapo juu ni kwamba ifunguliwe special Bank Acc. iwekwe hapa kwenye blog na vyombo vya habari.

    ReplyDelete
  8. Baadhi ya madawa ni kama ifuatavyo:
    Suramin (Antrypol)

    Diethylcarbamazine yenye majina mengi: DEC, Heterazan, Banocide, and Notezine.
    Ivermectin (Mectizan)
    Metrifonate (Trichlorphon), Mebendazole
    na Levamisole

    ReplyDelete
  9. Pole sana sofia...nafikiri cha muhimu zaidi ni kujua ni kiasi gani cha pesa kinahitajika, wapi matibabu yanapatikana na awepo mtu atakayesimamia kukusanya chochote kitakacho patikana. Mungu akusaidie....

    ReplyDelete
  10. Pamoja na pole nawatumia anuani za webusaiti hizi ili wahisani waweze kuchangia kwa matibabu au gharama:
    www.comicrelief.org
    www.christian.org.uk
    www.amref.org
    www.actsa.org

    wasalaam
    London.

    ReplyDelete
  11. naomba nirekebishe na kutoa anuani sahihi ya webusaiti ya comic relief:
    www.comirelief.com

    Wasalaam
    London

    ReplyDelete
  12. Kuna mdau hapo juu ametoa namba ya simu na website ya NGO moja huko London iitwayo facing the world. Ni NGO nzuri sana inaweza kumsaidia, kwa kweli kaka Michuzi unaweza kumsaidia kuwasiliana nao maana wanasaidia watoto wenye matatizo kama hayo. Kuna watotowengi toka Ethiopia na Kenya wamesaidiwa.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  13. pole sana dada mungu atakusaidia kwani yeye ni muweza wa yote, jamani muheshimiwa kikwete embu litilie manani jambo la dada uyu dada wewe unauwezo kabisa wakutafuta wadau nje na ndani ya nchi, na sisi watanzania tuliopo uk tumsaidie uyu ndugu yetu kila mtu akitoa pound kumi jamani inatosha, tutoe kwani mungu atatuzidishia mara dufu.

    ReplyDelete
  14. Sipingi kinachosemwa na picha lilvyo.siku hizi pia compyuta inaweza kuigiza picha za namna hiyo.Usiamini kila unachoona hata mimi nina huruma sana lakini najiuliza ni kweli hii?!

    Ikiwa nchini hakuna matibabu madaktari wamechukua hatua gani kwa kesi kama hii au wizara kuifanya hii kuwa kesi ya kitaifa ili kesho ikitokea wanfahamu msaaada unapatikana wapi kuliko kusema nje nje nag`ambo.

    Nitawachapa viboko woye wailiko idara ya afya.

    ReplyDelete
  15. Sophia Pole sana kwa matatizo ya ugonjwa unao kusumbua. Endelea kumuomba mungu bila shaka atakusaidia.

    Michuzi Tafadhali tunaomba umtembelee huyo dada kama kweli yuko Lugalo army hospital manake bwana huwezi jua anaeza kuwa mtu tapeli kabandua hii picha mahala fulani sasa anaitumia ili kuwatapeli watu ili apate fedha za kulewea.

    Aidha, ugonjwa kama huu nilishaona mtu anafanyiwa upasuaje katika televisheni chaneli ya discovery kwa wale wa USA watakuwa wanaijua kwa hiyo basi tukipata habari za uhakika kama kweli huyu binti ana exist na yupo lugaluga then wandugu wapedwa tujaribu kufanya kila liwezekanalo kuisambaza picha atakazopiga Michuzi hadi kieleweke. Pi ana Michango tutatoa as long as tuna uhakika zitamfikia mlengwa kwa makusudio ya kumsaidia matibabu au azawaizi

    ReplyDelete
  16. Michuzi,

    Ktk mchango wa kununua kamera ya mdau mmoja ulijitolea 50,000/=.
    Ktk hili la huyu mtoto umebaki bubu! Ina maana kati ya kamera na huyu mgonjwa kwako bora kamera au ...

    ReplyDelete
  17. MICHUZI MJENGWA ALIPODAI ANATAKA MCHANGO WA KAMERA ULIJITOA MBELE NA KUCHANGA SH 50,000 HARAKA SANA HUKU UKIOMBA WADAU WENGINE WAJITOKEZE KUMCHANGIA.
    JAMAA ALIPOPATA FEDHA, TIKETI YA NDEGE HUYOOOO SWEDEN WIKI MOJA KARUDI YUPO BONGO.
    LA DADA YETU SOPHIA HATUJASIKIA UHAMASISHAJI WOWOTE HATA KAMA KUDAI UMECHANGIA SH.500 TOKA MFUKONI MWAKO KAMA CHANGAMOTO, HAKUNA.
    NDIYO KUSEMA ILIKUWA GIA KUBWA ILI UWANGIZE WADAU KICHWA KICHWA NA KUMFANYA MJENGWA MTU WA MAANA NA MAARUFU SANA AU?
    SIYO KAMA NAOSHA KINYWA LAKINI UKWELI WA MAMBO NDIYO HUO NA UKIKASIRIKA UKAFICHA UJUMBE HUU, SHAURI YAKO, LAKINI UKWELI UTAKUA UMEUPATA NA KAMA LITAKUINGIA AKILINI, UTAONYESHA MFANO!! POLE SANA SOPHIA MUNGU ATAKUONDELEA MARADHA HAYO.

    ReplyDelete
  18. Hakuna cha comic relief wala nini!Tuambiwe gharama,tupewe ac no tutarusha hayo mawe binti akatibiwe.Nyie mnaojidai mko ugaibu,mnajidaigi mnapinga bakuli na umaskini kwa jumla,leo mmetuonyesha mnajua hadi website za kupeleka mabakuli!

    ReplyDelete
  19. Pole binti Sophia. Michuzi mi naona watu wapo hapa na wana moyo wa kusaidia. Tunaomba wewe binafsi ufanye bidii uende kumuona na ikibidi utumie nondo zako kumpiga picha manake hiyo picha kama imekatwa gazetini vile! Alafu jua gharama na kila kitu na ni nchi gani anakwenda alafu utumwagie issue watu tujikune tutakapofikia tumsaidie. Asante

    ReplyDelete
  20. Dear Michuzi
    Let’s help this little girl, Please take close pictures and Send them to the following contacts as soon as possible send them by UPS or DHL or FEDX after you do so let me know ad I will follow up

    Be well, do good work, and keep in touch,

    Regards,

    ============================
    Johns Hopkins International Patient Services
    JHOC, Suite 1080
    601 North Caroline Street
    Baltimore, Maryland 21287 USA
    E-mail: jhis@jhmi.edu
    http://www.hopkinsmedicine.org
    Vice President: Harris Benny, Phone 1-410-614-6734/Fax: 1-410-614-0955
    Associate Director: Rafaella Molteni, Phone 1-410-614-4405/Fax: 1-410-502-7397

    ============================
    UCLA Medical Center, Los Angeles.
    International Relations Office
    10920 Wilshire Blvd, Suite 1800
    Los Angeles, CA 90024
    E-mail: international@mednet.ucla.edu
    Phone: + (310) 794-8759 Fax: + (310) 267

    President: Dr. David T. Feinberg

    ReplyDelete
  21. I am happy to see wachangiaji wamekuwa-serious na issue ya dada Sophia. Michuzi kwa njia moja ama nyingine kama utataka kuratibu maoni ya wachangiaji unaweza kuugusa moyo wa Sophia na wasamaria wema wengine na kuleta mabadiliko.
    Kumbuka mkusanyiko bila ya uratibu hakuna kitakachoeleweka.
    Au wadau mnasemaje?

    ReplyDelete
  22. JAMANI MBONA HAKUNA GAZETI HATA MOJA LA TANZANIA LIMEANDIKA HABARI ZA HUYU DADA NA KAMA NI KAPUYA KWELI ALIMLETA HUYU DADA TOKA TABORA INGEJULIKA MAANA NI MBUNGE WA UKO ANGALIENI KWANZA MTU WA MUHIMU KAMA MICHUZI AFANYE UTAFITI NA WASIWASI KIDOGO NA HII PICHA PLS DONT TAKE ME WRONG LAKINI TUHAKIKISHE KWANZA SI MMEONA UTAPELI WA WA NAIJA JUZI JUZI KWA MICHUZI

    ReplyDelete
  23. kaka michuzi.mbona hujarudi kutupa picha uliyopiga wewe ya huyu Dada sophia ili watao hoja waweze kuchangia pesa maana wengi wanadhani huenda ni mambo ya technology huenda sio kweli.pia kama kuna Ac imefunguliwa kwa ajili ya matibabu yake naomba tujulishwe na tupewe Ac watu wachangie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...