hapa ni jiji klabu ambacho ni kijiwe kipya kwa wasiotaka vurugu. hapo unatia timu kwa mwaliko tu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi sasa mbona hutuambii hiyo "JIJI KLABU" iko wapi/maeneo gani?

    ReplyDelete
  2. Michuzi .. eti Aunti Shenazi kafa?

    ReplyDelete
  3. Ukisikia UBAGUZI ndio huu.....

    na sitoshangaa nikisikia kuwa wanaompinga richa ndio wa kwanza kwenda huko!

    Sina haja hata ya kujua hii club iko wapi. Maana kwangu mimi naona inaturudisha kwenye enzi za ubaguzi ambazo zimeshapitwa na wakati.

    A public place is a public place, ukitaka kuwa na issue zako aidha kodi sehemu ufanye party yako au fnaya party yako kwako.....

    ReplyDelete
  4. kweli shenaz kafa,apumzike ktk amani.kazikwa jana kisutu.na mwenzi wake ana hali mbaya sana yuko hospitali.

    ReplyDelete
  5. Eti ni kweli Shenaz amefariki?

    ReplyDelete
  6. JIBU: Anon 12:38:00 Ni kweli Aunt Shenaz kafariki kwa ajali ya gari.Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  7. Taratibu tunaeleakea, sasa tupe taarifa kamili iko wapi na tunapataje hiyo mialiko.

    ReplyDelete
  8. hebu tupe lokasheni ya hiyo klabu ili tuwapo bongo kukajivinjari kwa usalama kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    kc,ks

    ReplyDelete
  9. Anny hapo juu ni kweli Shenaz hatunaye duniani baada ya kufa ktk ajali ya SABCO....

    ReplyDelete
  10. JE NI KWA NINI SERIKALI ISIMFILISI MMLIKI WA SABCO AND KUWAPA FIDIA FAMILIA YA WALIOPOTEZA NDUGU PAMOJA NA WALE WALIONUSURIKA? PIA KUWACHUKULIA VIKALI HATUA YA SHERIA..HII ITAKUWA NI FUNDISHO KWA WAMILIKI NA MADEREVA WOTE KWA UJUMLA...

    ReplyDelete
  11. Michuizi sijakuelewa vizuri.....HAPO NI WAPI KWANI.......mambo ya utani utani mahali pengine sio mazuri.....ELEZA KITU KILICHOTULIA...HAPO NI WAPI???....kama unaona jibu lake ni DILI basi usiwe unaropoka

    ReplyDelete
  12. WADAU NA WAPENZI WA SHENAZ.TAARIFA NILIZOSOMA KWENYE VYOMBA VYA HABARI NI KWELI KAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA AJALI YA BASI LA SABCO ILIYOTOKEA JUMAMOSI KULE MBEYA.

    ALIKUWA ANATOKA KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KIKAZI HUKO TUNDUMA MBEYA.

    KWA MAELEZO ZAIDI UNAWEZA KUBOFYA HAPA HIYO LINK KUPATA MAELEZO ZAIDI.

    http://www.darhotwire.com/maisha.php

    MWENYEZI MUNGU ALIZA ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.AMINA

    ReplyDelete
  13. Wanawani bongo hakuna ubaguzi wa rangi ila kuna matabaka katika jamii yetu ambayo kwangu mimi ndio aina mbaya kabisa ya ubaguzi. Hii wabongo wenye nazo wanaishabikia lakini ndio haohao wanakimbilia kuzungumzia ubaguzi wa rangi. Mbona aina hii ya ubaguzi wanaifurahia?

    habari kutoka Morogoro mji kasoro bahari zinasema ABOOD Azizi ampiga chini Mh. waziri wetu Dr. Juma Ngasongwa, sasa hapa kuna ubaguzi wa rangi? Au tuseme hawa wananchi wa Moro wote mdebwedo?

    ReplyDelete
  14. Sasa ubaguzi gani uko hapa. mtu kama kaamua kufungua ukumbui wake wa starehe na kualika washikaji wake, na mashoga zake, tatizo liko wapi? Ni sawa tu na mtu amwe na nyumba yake na aalike marafiki zake kila wikiendi, sasa nyie mwatakaje? Mnapend a kuzamia vya watu , fanyenyi zenu wajameni.

    ReplyDelete
  15. Tulipiga vita "apartheid"! Sasa yaturudia mlango wa nyuma!

    Ubaguzi ni ubaguzi tu...wa rangi, matabaka, jinsia, dini, itikadi, vyama vya mipira, vyama vya siasa!

    Kulikuwa na Klabu moja hapo pwani karibu na Kilimanjaro Hoteli...ikiitwa Dar es Salaam Club...ya wazubgu na wahindi (kidogo).

    Kambarage kaifunga! Ikawa kwa wote!

    ReplyDelete
  16. Michuzi maeneo kama haya ni muhimu sana hususani kwa jiji la DSM ambalo mara nyingi ukienda hizi baa za kawaida unajikuta kwenye risk ya kuvamiwa na hawa "WAZEE WA UCHAKAVU"........wateja mnalazimishwa kulala chini na kuporwa kila mlicho nacho...si ajabu siku moja tutaporwa mpaka na nguo tulizovaa

    ReplyDelete
  17. Nadhani wale wanaokimbilia kueleza kuwa ni ubaguzi au siyo ubaguzi wanakosea na hawana haki ya ya kufanya hivyo.
    Cha msingi pata kujua ni utaratibu gani unatumika ili uwe kuwa mmjoja kati ya hao wanaoalikwa. Utaratibu wa klub kama hizi upo kila sehemu ulimwenguni. Zipo sehemu fulanifulani huweka utaratibu kwa ajili ya wateja wake.
    Wakati mwingine huwa inasaidia kwani kila anayekwenda pale hulazimika kujiandikisha kwa yupo hapo kwa muda ule. Endapo kama kunatokea jambo kla hatari au vinginevyo taarifa zake hupatikana tofauti na sehemu nyingine huhitajiki kufanya hivyo.
    Kwa hiyo usalama wako huangaliwa kwanza nadhani hata sight mirror ya gari lako ukitoka baada ya burudani utaikuta salama.
    Kwa mfano hapo Dar zipo klub ambazo huwezi kwenda bila ya kualikwa na zipo kwa miaka mingi tu na huenda hata wengi hawajazaliwa km Dar Gym Khana, hukatazwi kwenda, lakini ni lazima uandamane na mwanachama pale ambaye ndiye atakayekuwa amekualika, simple!!!!
    Huwezi kwenda katika Lions Club au Rotary Club bila ya kualikwa, ni lazima uandamane na mwanachama ambaye ndiye mwenyeji wako, simple just like that!!!!
    Ninashauri tupate kujua utaratibu uko vipi then mnaweza kusema kadri ya hali halisi ilivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...