wadau, msanii juma nature ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka video bora ya muziki wa hip hop na anaomba mumpigie kura kwa kubonfya linki hiyo hapo chini. shime wadau na tumbembe kijana wetu huyu anayejitahidi katika gemu. kupiga kura kunaanza leo hadi oktoba 4, 2007...
http://www.mnet.co.za/ChannelO/shows/nomination-artist.asp?ID=11

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Issa bro kwa nini unaogopa kudai haki zako??? Inawezekana unaacha pesa mezani bwana. Kukupa mfano watengenezaji wa filamu ya vikaragosi ya "The Lion King" yaani Walt Disney ya Marekani walitumia wimbo mmoja uliokuwa umetungwa na Mwafrika Kusini. Bila shaka watengenezaji hawakujua mmiliki hasa wa huo wimbo ni nani manaake wabunifu wa kiafrika Marekani huwa hawafahamiki sana. Yule Mwafrika Kusini baada ya kuisikia tune yake akatafuta msaada wa Kisheria na kufungua kesi ya Madai Marekani. Alishinda na kupewa donge nono kwa kazi yake. Sasa inabidi umtathmini huyu mwizi wako anaingiza mapato kiasi gani, na ni mtu wa aina gani (yaani ni corporate guy ambaye asingependa kashfa, au ni muhuni tu). Kama ni corporate guy au ni mtu anayependa kulinda jina lake tafuta mwanasheria akusaidie kumfungulia kesi. Kama jamaa anaingiza mshiko mzuri unaweza ukaambulia vidola elfu kadhaa.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli inakera sana brother Michu. Kwa hili niko tayari kukutetea na kukupa ushauri. Ila tujiulize kwa nini mtu asione aibu kujipatia credit ambayo siyo yake?? Why?? Ubunifu katika nchi yetu utakuwa lini if the status quo is left unchallenged?? Copy copy copy!!! Hii inanichefua kabisa. Wadau wengine kemeeni hii tabia. Last time mliwatetea wale wa sait gani sijui, I weighed the arguments nikaona kweli kuna ka element ka "fair use" maana wote wana ihabarisha jamii. Lakini kuweka alama kabisa??? Ahhhh!!! Someone should stop this!!

    ReplyDelete
  3. TAFUTA LAWYER HARAKA SANA MICHUZI.

    ReplyDelete
  4. Na wewe kaka Michuzi tulishakuchoka na malalamiko yako. Wadau tumekuwa tukikushauri kwamba watu kama hao inatakiwa uwashitaki ili hati miliki ifanye kazi yake, lakini wewe unasisitiza kwamba huna noma. Sasa kama wewe muhusika huna noma na wizi huo unafikiri tukushauri nini wakati jibu umetupa kwamba huna noma na wezi wako. Mara nyingi inakuwa hivyo, leo anaiba kidogo ukimuachia kesho anaongeza and then mwishowe anahamisha kabisa na kudai ni chake, wewe si ulikuwa huna noma naye.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  5. Tuseme nini Bruv Michu,acha unafiki,juzi umetuomba ushauri kuhusu another website ukakubaliana nao then ukatuambia hamna noma wala nini.Kwa hiyo watafute hao nao ili mmalize udhia kama wale wengine au vipi.Kwa hili hatuna ushauri ....

    ReplyDelete
  6. mi nadhani imefika wakati maharamia wanajiamini kwako hadi wanakushika sharubu we unabaki kushangaashangaa tu,ukinung'unikia pembeni haikusaidii tutakuona mzushi tu,chukua hatua za kisheria ili iwe mfano na hawa wameshajianika tofauti na wanigeria ooh haya we,mchelea mwana kulia hulia yeye,ukimchekea nyani utavuna mabua na sisi tutakuchekaa ,si yetu macho tu.

    ReplyDelete
  7. mimi bado najiuliza ni vipi mbona utitiri wa video za kitanzania za bongoflava ulivyojaa hapa mbona sielewi ? yaani kweli video moja tuu ya juma nature ndio imeonekana bora?
    Hebu angalia nchi jirani hapo Kenya sina uhakika unspecified sources zinasema wamepata nominations saba(7) aparently.
    kwa upande mwingine hii this single nomination ya watanzania it's a wakeup call kwa watengenezji video nyumbani hapa ,pia it defies ule sheria yatu inayotokana na utamaduni mashuhuri wa tanzania yaani UNAFIKI wa KUJISIFIA ooh! video zimetulia,ooh!,bongoflava bwana bab kubwa! mara aah video za bongoflava zinaviwango bab kubwa na tunatesa saana huko nje ya nchi
    Nimeshawahi sema mara kadhaa ktk ukumbi huu na kushambauliwa sana na watoa maoni wengine!
    sisi wabongo tunapenda na tunaona fahari kujipa MISIFA ya uongo men! tunapenda saana kujisifia sifia na japo hatuna uwezo unaotakikana il mtu asifiwe.
    nilishasema before kwamba ni vema tuasubiri sifa kutoka kwa competitor wetu,wadau watumiaji wa kazi zetu za sanaa

    Hivi wenzangu mnaonaje ,mnafikiri MNet wametuonea? au hawana wataalamu wa kusort na ku-pick great videos ?

    Video za muziki kuonekana kwenye tv especially hapa sio kwamba video hizo basi ndo zitakuwa na viwango vya kuonyeshwa ktka ma Net work Tv yale makubwa hii ukiachia mbali SUBSTANCE ya video husika,lakini kwa uzoefu wangu kwa kawaida NETWOKS kubwa kama Mnet nafikiri wanapima visual quality ya video pia na wanzingatia saana hilo ukiachia substance na suala zima la composition na kiwango cha mziki husika,yaani audial qualityu

    Hapa nyumbani huonueshwa saana tuu kwenye tv domestic nafikiri (sina uhakika) ni kwa sababu ni lazima kupromoti na kucheza local materials any way irrespective of quality kwa sababu that's what is available
    sasa basi inapokuja tv networks za nje viwango hua ni vya juu sana

    sasa basi kwa maoni yangu mimi nawaomab wabongo wenzangu tuache huu urithi wa utamaduni wa kujisifia sifia uongo,tena sio tuu kwenye kazi za sanaa bali hata kwenye soccer siku hizi na japo hatauna na wala hatustaili misifa hiyo

    Kazi ya ku produce video inataka kwamza kipaji cha usanii kama ilivyo sanaa nyingine,lakini hivi sasa kila mwenye camcorder na computer basi utasikia eti anajiita .... production,..... films works Inc nk majina makubwa lakini ubora leaves a lot to be desired!

    Ukiacha mambo na vigezo vingine vingi tuu ni vema watengenezaji,directors na producers ofcourse bila kuwaacha artists wenyewe muanze kuangalia pia ubora unaotakiwa ktk video sio tuu kwa kuagalia soko hapa nyumbani pia soko la nje
    Mfano hivi sasa networks nyingi kubwa wancheza na wanpendelea kucheza video zilikuwa shot kwa fils iwe ni 16mm,super16 au best ni 35 mm,ofcourse zinakuwa transfered ktk video format for final release mfano wa stations hizo ni Mnet na MTV nk

    pia hupendelazaidi video zilizoshut kwa high End pro video camera na siyo mambo ya high def prosumer gears .
    any way nomination hii ya video moja ni blow on the face ! kutokana na tabia ya kependa kujisifia tusikate tamaa tuitumie kama changamoto la kutsukuma zaidi ili tufanye kazi ilyobora ktk viwango (vya ukweli na siyo blah blah)

    JUma nature bwana hongera saana
    na hasa director na wahusika woote walishiriki ktk kufanaya video hiyo
    tuko nyuma yako
    great job!

    Raceznobar

    ReplyDelete
  8. Mh, jamani mbona hayo maoni hapo juu mi naona ni Ndivyo sivyo, au mawenge yangu? Picha na kichwa cha habari ni Juma nature anaomba kura zetu, maoni naona mambo ya wizi duh!
    Au Misoup alilalamika kuibiwa tena na baada ya kupewa dau lake kama last tyme akaondoa malalamiko na kuweka hii habari ya Juma nature akasahau kufuta maoni nini?
    Haijaniingia akilini jamani, nielewesheni mwenzenu, isijekuwa PC ninayotumia ina kizungu zungu jamani!, vijijini huku tabu tupu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...