NA MPIRA UMEKWIIISSSHAAAAAAAAAAA.....

MSUMBIJI 1 TAIFA STAAZ 0

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Msife moyo wadau,
    haya mambo yanachukua muda kuzaa matunda. Nafikiri huu moto uendelezwe kwa ajili ya mechi zijazo.

    ReplyDelete
  2. Afadhali maana kelele za JK, hivi JK vile zingetuziba masikio na kutusahaulisha jinsi anavyoboronga katika kuendesha nchi.

    ReplyDelete
  3. Ndo mambo ya soka. Tulikuwa tunapimana nguvu na mojawapo ya vigogo wa soka afrika, wametuzidi nguvu, cha msingi tusikate tamaa kwani ndo kwanza tunaanza kusimama dede wakati wenzetu wa msumbiji walishatambaa. Hata kwa FIFA rankings (ambazo zitabadilika kwa matokeo ya mechi za leo) msumbiji wako nafasi ya 86 wakati Tanzania iko nafasi ya 102. Hivyo kimpira ni kaka zetu, huo ndo ukweli. Tujizatiti kwa siku za usoni na maandalizi yaanze mara moja.

    ReplyDelete
  4. Haya matokeo yanapendeza kiasi maana Msumbiji hawaendi kokote, na sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye matatizo yetu ya Buzwagi na Richmond, hatuwezi yasahau sasa.
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  5. basi hakuna noma wamejitahidi mungu yupo

    ReplyDelete
  6. Haya matokeo yanapendeza kiasi maana Msumbiji hawaendi kokote, na sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye matatizo yetu ya Buzwagi na Richmond, hatuwezi yasahau sasa.
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  7. POLE SANA WATANZANIA WENZANGU!!

    HUU NDIO WAKATI MWAFAKA WA KUONYESHA MSHIKAMANO.


    TUPO PAMOJA,HONGERA STARS,TUNAWAPENDA NA TUNAWATHAMINI.

    PONGEZI MAXIMO TUPO NA WEWE.
    TUKUBALI MATOKEO NA TUWE NA UMOJA.

    ReplyDelete
  8. Du kweli ng'ombe wa masikini hazai na hakizaa ndama anakuwa mgonjwa na hatimaye kufa.Hata hivyo tusikate tamaa.Sio majungu yanaanza na kumfukuza kocha.

    ReplyDelete
  9. kama kawa holaa...Taifa stars poleni sanaaaa
    mungu atawasaidia, hopefully soon!!

    ReplyDelete
  10. Acha tufungwe ili tuendelee kuyakumbuka mabuzwagi yetu

    ReplyDelete
  11. TUMEPATA HAKI YETU.

    ReplyDelete
  12. NA SIMBA WA TERANGA KAMPA MTU 5-1. TUMEJITANGAZA SANA NA NILIWAAMBIA TUNANUNUA NEPI MTOTO BADO HAJAZALIWA. MATOKEO YAKE HATA ZILE NAFASI TATU ZA BURE TUMEAMBULIA PATUPU. SHEREHE SHEREHE NYINGI NA NILIJUA YATAWAKUTA KAMA YALE YALIYOWAKUTA SIMBA VS STELLA ARTOIS YA CODE VOIRE. WATU WAMEKALIA KUUZA TIKETI ZA WIZI KWA KUSINGIZIA TAIFA STARS, TAIFA STARS. SASA KIPO WAPI. KAENI SASA MLE UWANJA WENU MPYA. MASHINDANO MENGINE-2010 WAKATI HUO WANJA LITAKUWA MDEBWEDO. WACHEZAJI WAMEZIDISHA UBISHOLOLO NA KUSAHAU KWAMBA SOKA NI KAZI. KWAO WAO SOKA NI KUONYESHA VIBALOON VYAO FEKI. SASA WAKATI UMEFIKA, TENGA NA WENZAKO TIMUENI WEZI NA MMESABABISHA TIMU HII KUFUNGWA. JK, JK, JK, MALIZIENI BASI-JKT.

    ReplyDelete
  13. Afadhali tumetolewa mapema, maana kwa kiwango cha timu yetu huko Ghana ingekuwa aibu. Tuanze kusuka kikosi kwaajili ya 2010.

    ReplyDelete
  14. NIMEFURAHI SANA WATU WENGI SANA WAMEKUWA POSITIVE KWELI WA TZ TUNAPENDA NCHI YETU YAANI HATA WATU WANAKAA NJE YA NCHI NI KWASABABU YA SHIDA SISI WOTE BABA YETU MMOJA YAANI NYERERE MIMI SIJAKATA TAMAAA HAWA JAMAA SASA HIVI WANAIVA SANA
    IDUMU TAIFA STARS

    ReplyDelete
  15. Haya matokeo niliyategemea ndo maana sikuweka maoni yangu,my bruv NDAKi aliwa over- rate sana hawa vijana wa Taifa Stars lakini ukweli ni kwamba mpira wetu bado sana,hii baada ya kuona live ya 4-0 dhidi ya Senegal.
    LA MUHIMU turudi tujipange upya tuweke mikakati ya World cup,TUKUBALI MATOKEO KWANI "asiyekubali kushindwa si mshindani" na"kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi",tusikate tamaa one day YES.
    CHA CHANDU

    ReplyDelete
  16. Ni muda muafaka sasa kurudi Buzwagi mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  17. Hay mpira umeisha tumefungwa na tumeumia BUT life has to go on. Haya twendeni sasa tukalicheze Twangapepeta manake tumelikosa siku nyingi, na wengine wa Ngwasuma kama kawa na wale wa mambo ya CLubing haya tena

    ReplyDelete
  18. kwa masikitiko makubwa tumeyapokea matokeo ya mechi na msumbiji na kama tungeshinda naona tungevunja jungu kwa kufuru sasa ni wakati muafaka wa kuelekeza matarajio yetu kwenye sekta nyingine za kiuchumi na kijamii mpira basi maana tumefungwa nyumbani ndani ya uwanja wetu mpya ambao tungeweza kutumia fedha hizo kwenye shughuli nyingine haswa mashule na huduma za afya kwa wanawake na watoto ambao ndo taifa la kesho .

    ReplyDelete
  19. Stars mbofumbofu,magazeti andikeni msimwogope kikwete.

    ReplyDelete
  20. Nuksi ilianza tarehe 1 mwezi huu, walipomchagua miss Mhindi, mi nikajua tu huu mwaka basi, tumeshachemsha kila kitu, mambo mazuri tungojee mwakani tena,,hii miezi ilobakia ya 2007 ni BALAA TUPU.....yote ni nuksi aliyoleta Lundega na shoga yake Richa.

    ReplyDelete
  21. Motokeo ni sawa kusema ukweli, nilikua sijawahi kuangalia mechi ya Starz kabla ya leo na kusema ukweli kiwango chetu ni kidogo sana, yaani ilikua ni kubutua mpira ili mradi uende mbele, hakuna build-up play yenye akili.
    I hope watamfukuzu huyo kocha ili pesa zitumike vizuri kwenye shughuli za maendeleo.

    Na pia tujaribu kulijenga soka kuanzia utotoni kwa kuwa na ligi za miaka tofauti (under 16, 18 etc) na hata labda academy za michezo kama wenzetu wanavyofanya.

    Mungu ibariki TZ!!!

    ReplyDelete
  22. Sasa ni muda muafaka wa kurudi kwenye masuala muhimu yanayohusu taifa letu! Buzwagi, richmond nk.. Muda wa kuzugana umekwisha. Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  23. Mtoa Mada wa mwisho Madiba boy, acha ushamba ndugu yangu, sasa wewe unafikiri kumfukuza kocha ndiyo itasaidia? naugana nawe kwenye hoja yako ya kuandaa vijana, pia soka kuwa bado hipo chini, lakini hata kidogo siungani na wewe juu ya suala la kumfukuza kocha.
    Leons, USA

    ReplyDelete
  24. Wanaostahili lawama kufungwa Taifa Stars si wachezaji wala kocha bali ni kamati ya ufundi ya Taifa Stars.Inabidi itimuliwe.

    Michuzi BLOGU HII TAREHE 6 SEPT 2007 illeta taarifa ya nini kifanyike ili tuifunge msumbiji mabao mbili bila na mshauri akaeleza kuwa tusipofanya hivyo magoli mawili bila yataingia goli la Tanzania.

    Kweli mabao mawili bila yameingia goli la Tanzania moja likakakubaliwa moja likakataliwa.Mtabiri alikuwa sahihi.

    Labda nikukumbushe kuwa Michuzi tarehe 6 sept 2007 ulibandika kueleza breaking news za kifo cha mchezaji wa msumbiji Matola kwenye blog hii.

    Mmoja wa wachangiaji akajibu hivi:

    "Msumbiji hao kwa uchawi ndio wenyewe wameshamtoa kafara mwenzao kwa uchawi ili wawafunge watanzania.

    Watanzania mtafungwa tu wenzenu wameshawawahi tayari.

    Taifa Stars itafungwa tu.

    Hamna mjanja aweza tegua uchawi waliofanya wachawi wa Msumbiji kwa uchawi.Taifa Stars itafungwa magoli mawili bila.

    Labda mpeleke walokole wakemee kwa jina la Yesu wakizunguka huo uwanja wa Taifa ndipo mtawafunga mabao mawili bila.Wachezaji wa Tanzania wakiingia uwanjani waseme Yesu,Yesu,Yesu mara tatu ili kufukuza majini waliyokuja nayo wachezaji wa Msumbiji.

    Bila hivyo mjiandae kufungwa mabao mawili bila mbele ya Raisi Kikwete." Mwisho wa kunukuu.

    Na kweli tumefungwa.Kamati ya ufundi ingefuata huo ushauri tusingefungwa.
    Lawama zote za Taifa stars ziende kwa kamati ya ufundi.Wamewekwa wahuni wasiojua ufundi.

    Kocha na wachezaji safii tu.Kamati ya ufundi hawajui kitu wale.

    ReplyDelete
  25. Yaani hatujapata bado nafasi ya kupumua na pigo la Miss India kuwa Miss Tanzania, na sasa hili pigo la Kufungwa na Msumbiji! Kudadadeeki! Tanzania tuna sifa ya kuwa wastahamilivu sana, najua tutasongambele mwakani tutampata Miss Tanzania asili, na Mechi dhidi ya Msubiji next time tutashinda 3 - 0.

    God bless Tanzania!

    ReplyDelete
  26. tumejitahidi

    ReplyDelete
  27. kujitahidi wamejitahidi stars ila mambo ya soka yapo hivyo ila ktk blog hii kunawatu darasa la saba wengi niwatu wa kukurupuka ipo siku tutafika huo ni mwanzo tu nani alitegemea kama stars ingetoa challeng kiasi hicho.Mmejitahidi stars mshikamano muhimu.

    ReplyDelete
  28. MAKOCHA WA BRAZIL HAWAZIFAI TEAM ZA AFRICA.. WANAWEZA KUFUNDISHA WACHEZAJI AMBAO NI VERY TALENTED TUU, SISI TUNAOHITAJI DARASA HAWAWEZI.SASA HIVI SOUTH AFRICA KESHAPIGWA 3-0 NA ZAMBIA PAMOJA NA KUWA NA CARLOS ALBERTO PERREIRA. PIA MAKOCHA WA BRAZIL HAWAWEZI KUWAFANYA AU KUWATAFUTIA WACHEZAJI WETU TEAM ULAYA KITU KINACHOWETA LETA REVOLUTION HAPA KWETU. NDIO MAANA WACAMERON NA NIGERIA (SOCCER POWERHOSES IN AFRICA) HATA SIKU MOJA HAWACHUKUI MAKOCHA WA BRAZIL. NASEMA KAMA TUNATAKA MAFANIKIO BASI TUWE NA KOCHA WA ULAYA HASA HASA UFARANSA.SISI TUNAPENDA MAMBO CHEAP NDIO MAANA TUTAISHI KWA MATUMAINI TUU ILA REKODI YA AKINA PETER TINO ITAKUWA NDOTO KUIFIKIA.

    ReplyDelete
  29. SASA TUNA SERIKALI INAYOJUA UMUHIMU WA MICHEZO, TUNA UWANJA ULIOJENGWA NA MKAPA (SIYO JK) INGAWA JAMAA KAPIGA BAO MALI ZETU KIBAO. TUNA KOCHA NA TUNA WASHABIKI LAKINI HATUNA WACHEZAJI, INGEKUWA ENZI ZILE ZA AKINA MASATU, MASHA, IDD SELEMANI, LENNY, KASONGO, MWAMEJA, JUMA AMIR, LUNYAMILA, KIDISHI, RIFFAT, TUNGEKWENDA MBALI. HAWA SI WACHEZAJI JAMANI.

    ReplyDelete
  30. PONDA MALI KUFA KWAJA, WABONGO TUNAJIVUNIA MISS INDIATANZANIA NA WANJA LETU LA TAIFA.NANI KASEMA TUNAJIVUNIA SOKA.

    ReplyDelete
  31. WATANZANIA WENGI WANAFIKI NA WATU WA OVYO KABISA,YAANI KABLA YA MECHI WALIKUWA NA TAIFA STARS BAADA YA KUFUNGWA WANATOA MAONI YA AJABU AJABU,KWELI WATU WANAFIKI NA SISHANGAI NCHI NI YA OVYO OVYO!

    ReplyDelete
  32. narudia kocha afukuzwe!! Kocha analipwa kufikia malengo fulani hata kama hayapo realistic, na hayu bwana amefeli, kiwango cha wachezaji bado ni kibovu, pamoja kuwa watu wanasema kimeimprove bado ni kibovu sana, yaani tumebadili level za ubovu tu ndo tulichofanya.

    Pia naamini kua hakuna alichofanya huyo kocha ambacho kocha wa kibongo au wa kiafrika ambaye angelipwa much less angeshindwa kufanya. tatizo tukiweka makocha wa kibongo serikali haiwapi support, lakini akija mbrazil team inasafiri nje daily inapata experience then tunasema kocha bora wakati vitu havifanani.

    ReplyDelete
  33. tatizo mazoezi wanayofanya mdebwedo. Wanafanya mazoezo marahisi mno. Wenzetu Ulaya wanafanya mazoezi magumu sana. Achilia mbali vipaji, kipaji bila kuendeleza kwa bidii haiwezi kuonekana. Mazoezi wanayofanya akina Rooney, Ronaldo na wenzao siyo lelemama kama hawa jamaa zetu, hawana stamina kabisa.

    Halafu hakuna anayecontrol diet wanakula ovyoovyo tu wanavyoweza. Wanakunywa hovyo, na si ajabu wanakunywa laga, na wanawake wengi kama kawa. Kwa mtindo huu wa maisha ambao hauna nidhamu wala control kutoka mtalaam wa afya watakuwa midebwedo tu.

    Mpira wa kimtaifa si lelemama unahitaji nidhamu katika vitu vingi na mazoezi ya nguvu. Bila hivyo ni kichwa cha mwendawazimu tu. serikali yenyewe kupitia wizara husika unakuta haina sera yoyote inayoeleweka ya kisasa kuhusu michezo, kila mtu kajichokea tu huko ofisini. Jamani ni kwamba tumelogwa bongo? Au ni nini? Mbona kila kitu mdebwedo? Tukumbuke tu michezo ya Osaka juzi. Majirani zetu tu hapo Kenya jiulize wamerudi na medali ngapi za dhahabu. Na sisi tumerudi na nini. Hii nchi baada ya muda kama si mapinduzi tutaanza kuikana. Nchi gani hatuna pa kutokea hata kitu kimoja? Kila mtu kajichokea inakera. Unaweza kuamini huu Mungai alifuta michezo shuleni unategemea nini? Siku moja hapa Uingereza nilienda uwanjani nilikuta timu ya watoto wa miaka kuanzi minne mpaka mitano wakizi sita na si zaidi ya hapo wanacheza wamevaa jezi wako kamili kumi na moja. Naombeni mnielewe sitii chumvi wala nini ndio hali halisi, na walimu wao wako pembeni mwa uwanja wanatoa maelekezo na watoto wanafuatilia kwa umakini, sisi tunafuta michezo sekondari. Kwanini
    hawa viongozi wakifa siku moja tusiwapime bongo zao. Inakera kuona katika nchi viongozi hawana hata plan ya miezi mitatu ijayo. utafikiri tumeambiwa na kibwetere siku zimeisha tunaenda kufa. Lawama
    zote kwa Serikali.

    ReplyDelete
  34. Tico tico tico tico tico tocooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo! Hamna kitu TZ sound tu!

    ReplyDelete
  35. Tico tico tico tico tico tocooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo! Hamna kitu TZ sound tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...