HABARI ZINASEMA HUKO KOROGWE GARI LA TVT JANA LILIPINDUKA NA ABIRIA WAKE AMBAO NI WAFANYAKAZI WA TV HIYO YA TAIFA AKIWEMO DADA ESHE MUHIDIN WAMEJERUHIWA NA WALIKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA WA TANGA YA BOMBO KWA MATIBABU.
HABARI ZA AWALI ZINASEMA DEREVA WA GARI HILO AMBALO LILIKUWA LIKIELEKEA MOSHI KUKAVA MAZISHI YA HAYATI SALOME MBATIA LAIVU ALILAZIMIKA KULILENGESHA GARI NJE YA BARABARA KUKWEPA KIZUIZI CHA POLISI CHA BARABARANI SEHEMU ZA KOROGWE, NA GARI LIKAPINDUKA. HABARI ZINASEMA NDANI YA HILO GARI MLIKUWA NA WAPIGA PICHA WAWILI NA MARIPOTA WAWILI
MUME WA ESHE MUHIDIN, MAULIDI KITENGE, AMETHIBITISHA SASA HIVI KUHUSU AJALI HIYO NA ANASEMA AMEONGEA NA MKEWE MUDA MFUPI ULIOPITA NA KAMWAMBIA KWAMBA ANA MAUMIVU UBAVUNI NA ANANGOJA MATOKEO YA X-RAY ALIYOPIGWA KUJUA MADHARA ALIYOPATA.
ABIRIA WENGINE AMBAO MAJINA YAO BADO KUPATIKANA MARA MOJA WAMEPATA MAJERAHA KIASI NA WANAENDELEA VIZURI


Poleni sana. Mbona naona kama ajali za barabarani zinazidi kuwa nyingi.
ReplyDeleteebwana, pole kwa majeruhi, pole sana,,i hope wengine watatumwa haraka wakachukue video huko msibani Kilimanjaro,,
ReplyDeleteBongo kuna nini jamani, viongozi wetu tilieni mkazo usalama wa barabarani, waziri wa usafiri...?? sina uhakika kama anaitwa hivyo, naamanisha anayeshughulikia maswala ya usalama wa barabarani, yuko wapi? mbona hatumsikii? CHUKUA HATUA, HII SASA KARAHA..AJALI ZINAFUATANA KAMA MAZINGAOMBWE BWANA.
du hii sasa kali kila kukicha jamani poleni sana majeruhi uzembe siyo wa madereva ila wa wale wanaotoa leseni mtu hata ajui uendeshaji na sheria za barabara ni mawazo tu wadau
ReplyDeleteDuh!! Poleni sana mlioumia katika Ajali hiyo... Mimi kama kawaida napenda kutoa RAI kwa jeshi la police hayo Ma-gate yao wanayaweka mahali ambapo sio rahisi kuyaona usiku taa ya Chemli nyekundu isiyo na mwanga wa kutosha,Al manusura tuivae juzijuzi tukitokea Moshi tatizo ni hawana Reflectors hawana chochote kichoonyesha kuwa kuna Gate... Karibu... Ma-gate yooote yapo katika mkoa wa Tanga... Kamanda Sirro do something pleaseeeee!!!
ReplyDelete