WADAU WA BONGO NAOMBA MTULIZE MZUKA. ZAWADI YA $500 TUTAKE TUSITAKE INABIDI IENDE KWA BRIAN MARIKI WA HOUSTON, TEXAS, MAREKANI, KWA KUWA YEYE NDIYE MSHINDI HALALI BAADA YA KUIBUKA PASINA SHAKA YOYOTE KUWA MDAU WA MILIONI 2 WA GLOBU YETU HII YA JAMII, NA ZAWADI HIYO ATAIPATA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

KATIKA KUTULIZA HUO MZUKA, WADAU WA BONGO MSIKONDE. SPONSA WA HII ZAWADI AMBAYE SI MWINGINE ILA ANKO RODRICK B. MWAMBENE MKURUGENZI MKUU WA COMPUTERCONSULT LTD. AMESIKIA KILIO CHETU KWAMBA BONGO SIO TAMBARARE KIIVYO KWANI HAKUNA NYENZO ZA KUWEZA KUSHINDANA NA WADAU WA UGHAIBUNI, AMBAO WANA INTANETI NYUMBANI NA ISITOSHE ZINA SPIDI KUBWA, NA AMEAMUA YAISHE KWA KUTOA $500 INGINE KWA MAHUSUSI KWA AJILI YA WADAU WA BONGO UFIKAPO MUDA WA KUMZWADIA MDAU WA MILIONI 3.


YAANI SAFARI HII MDAU WA MILIONI 3 ITABIDI AWE KUTOKA BONGO HIVYO KAENI MKAO WA KULA NA ACHENI LALAMU.


PICHANI NI ANKO MWAMBENE AKINIKABIDHI $500 KWA AJILI YA BRIAN MARIKI NA $500 ZINGINE KWA AJILI YA MDAU WA BONGO ATAKAYEIBUKA WA MILIONI 3. SHEREHE HII ILIFANYIKA LEO KWENYE KIOTA CHA MARAHA CHA BREAK POINT, KIJITONYAMA, NA KUSHUHUDIWA NA WADAU MBALIMBALI WAKIWEPO FRIENDS OF SIMBA. HIYO MSIWE NA WASIWASI NA WALA MSIMSAKAME BURE BRIAN WA WATU KWANI SIO KOSA LAKE KUWA UGHAIBUNI NA KUJISHINDIA $500 KWA KUWA MDAU WA MILIONI 2.


MJADALA WA TASHTITI HILO NAUFUNGA RASMI HII SASA NA NAMTAKA BRIAN ASUBIRI MKWANJA WAKE. NA PIA NACHUKUA NAFASI HII KUMPA HONGERA TENA BRIAN KWA USHINDI NA KUWASHUKURU WADAU WOTE DUNIANI KOTE KWA KUENDELEZA LIBENEKE.
VILE ILE NATOA ASANTE KWA RODRICK B. MWAMBENE BOSI WA COMPUTERCONSULT LTD. KWA UELEWA WAKE NA MOYO WA KUJITOLEA UNAOFAA KUIGWA NA WADAU WENGINE WENYE UWEZO NA NIA NJEMA KWA WADAU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Michuzi, kuna tajiri mwingine wa ComputerConsult hajatokea kwenye picha, ni Yanga mkubwa, mwambie Rodrick ampe salamu zake.

    ReplyDelete
  2. Issa umeonesha jinsi gani usivyo na msimamo kwa hiki kitendo cha kujiuliza eti kama Mshindi apewe zawadi yake au la!

    Na kumbuka blog yako haina mipaka kwa hiyo kelele za wadau wa Bongo achana nazo, wakikua wataacha

    ReplyDelete
  3. aliyepata kapata,,hongera brian.....leo michu liverpool lazima tuwachape kama 6 ivi, kwahiyo kaa mkao wa kula na hizo zawadi zako unaweza kuanza kujiliwaza nazo mwenyewe....

    ReplyDelete
  4. Michuzi naona sasa unapoteza maana halisi ya shindano lako. Unaposema mdau wa milioni 3 LAZIMA atoke Bongo, una uhakika gani kwamba atatoka Bongo? Au ikitokea mdau wa milioni 3 ametoka nje ya Bongo basi itabidi umruke ili usubiri wabongo waamke ndipo uwape hiyo zawadi?

    Hii naona ni sawa na mtu kuanzisha mashindano ya mbio halafu unasema bingwa wa hizo mbio lazima awe mtanzania na wakati washiriki wapo wa kutoka nchi nyingi tofauti. Kimsingi utakuwa umewafukuza wanaotoka nje ya Tanzania wasishiriki hayo mashindano. Kwa kifupi ni kwamba kwenye shidano lako la MDAU WA MILIONI 3 hutaki washiriki walio ughaibuni, which is not fair and makes your competition meaningless, tafuta jina jingine na siyo useme SHINDANO LA MDAU WA MILIONI 3. Haina maana niwe mdau wa milioni 3 halafu uniruke umpe ushindi mdau wa 3000520, bado utaendelea kuliita hilo shindano la mdau wa milioni 3?

    Tafuta shindano la jina tofauti ambalo litawahusisha watu walio Bongo tu. May be useme kwamba lengo ni kumpata mdau kutoka Bongo lakini yeyote atakayekuwa wa kwanza after 2,999,999.

    Kwa kumalizia, GLOBU yako ni ya jamii, jamii haibagui uwe Tanzania au ughaibuni bado ni mwanajamii na tena mtanzania. Acha ubaguzi endesha mashindano na mshindi apewe zawadi bila kujali yuko Bongo ama nje ya Bongo.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana mdau wa milioni 2 !

    ReplyDelete
  6. MICHUZI HUYO WA KUSHOTO MWENYE KOFIA KAKAKO NINI? MAANA HILO DOMA KAMA WEWE.. NA MUSTACHE..

    MZOZAJI

    ReplyDelete
  7. "Wadau wa bongo"!!!Ni akina nani hao?Mbona sijasoma popote pale ambapo "wadau" hao wamewalalamikia wenzao wa ughaibuni?Anyway,cha muhimu sasa ni kutekeleza ahadi yako.

    ReplyDelete
  8. Michuzi hata sikuelewi au hueleweki. Ina maaa mshindi ni lazima atok Bongo ..kwa kukaza libene au akitoka nje ya bongo zawadi hapati?

    Kuwa honesty na sio kuwaridhisha watu wa home. Hata kama unaonyesha upnd o na huruma zao lakini kama akitokea tena nje ya nchi hutampa.


    Mimi ningekushauri zawadi hiyo itoke kwa mtu yeyote ila huyo mtu ni lazima wagawane hiyo hela na mtu wa Tanzania. Upeleke hiyo hela kwenye charity orgnization yeyote atakayochagua mshindi na jila lake litajwe kuwa yeye ndio amesema hela zisaidie hapo.

    Hiyo ndio uzalendo. Lakini mambo ya kusema ni lazima mshindi atoke bongo haina sence. Na sio kuwa tunadanganya lakini majority ya watu wanasoma blog yako wako nje ya nchi sas ni kama unawashika mikono.

    Mimi ni hayo tu yangu kwa leo

    ReplyDelete
  9. Michuzi namfagilia sana huyu brother Rodrick kwa hatua kubwa ya kimaendeleo aliyokuwa nayo...Jamaa alikuwa anacheza sana soccer sijawahi kuona.tokea katika shule ya msingi Mlimani(UDSM), Azania Sec School, Tambaza na hata Proffessional football in India....Nimefurahi sana kumuona kwenye picha ila kanenepa sana.Kwa upande wangu sijawahi kuona mchezaji kama yeye, labda kina Ronaldinho au Okocha..His game ws intertaining

    ReplyDelete
  10. HALAFU NA HIZO COMPUTER ZAO ZA LONG
    NAINTIN KWEUSI ZA PENTIUM MOJA AU
    MBILI SIJUI KAMA WATAWEZA KUINGIA
    WEB SIKU HIYO.MAANA TUTAINGIA KWA
    WINGI HUKU UGHAIBUNI WATAKOMA NA
    WATALIA SANA SAFARI HII WAKISIKIA
    MTU WA MILIONI TATU ANATOKA MAJUU
    HUKU TUNA MADUDE AMD ATHLON,AMD SEMPRON,INTEL CORE 2 DUO PRO.
    MAMBO YA CELERON TUSHATUPA ZAMAN
    HIZO ZIJE HUKO KWENU.MICHUZI LAPTOP
    YAKO UNATAKA ANTIVIRUS YA NGUVU
    AMBAYO HACKERS HAWATAINGIA? IF YES
    SEMA TUKUTUMIE ANTI-HACKERS KAKA
    REGARDS

    ReplyDelete
  11. "MAANA TUTAINGIA KWA
    WINGI HUKU UGHAIBUNI WATAKOMA NA
    WATALIA SANA SAFARI HII
    WAKISIKIA
    MTU WA MILIONI TATU ANATOKA MAJUU"

    Damn ok,here we go lol

    ReplyDelete
  12. Hongera Brian,
    Ilikuwa kidogo tu nikamate mshiko.
    BofyaHAPA

    ReplyDelete
  13. Michuzi, Blogu yako ni ya kimataifa. Wasomaji wako wengi wajo nje ya Tanzania. Hivyo mtu anayeishi nje ya Tanzania akishinda ni sawa.

    ReplyDelete
  14. Whyyyyyyyyyy kwa niniiiiii!! Huko maisha si mazuri wenzetu ila bado tunanyang'anyana hako kadola 500!!!! Mmmmmmmm kazi ipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...