Home
Unlabelled
BREKING NYUUUZZZZZZZZZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Michu,
ReplyDeleteSafari imeanza, waachie na wengine jamani. Au ndo kajiuzulu apewe uwaziri? Maana Tz kwa kubebana hatujambo. Mtoto akivunja sahani anapewa chungu abebe
Kazi imemshinda, kashindwa kukusanya madeni anakimbilia kupandisha bei kwa 40% na 280% kuunganisha line mpya. Jamani, umeme nao umekuwa anasa?
ReplyDeleteNinavyomfahamu huyu mzee ni mtendaji mzuri sana na anajua anachokifanya. Inawezekana wanasiasa uchwara walitaka kuingilia kazi zake akaamua kuanza mbele. Kama kweli amejiuzulu kwa ajili ya manufaa ya Taifa basi ninampa pongezi na ni mfano wa kuigwa.
ReplyDeleteHuu ni mfano wa kuigwa kwani bongo ina viongozi wengi wanaotakiwa kujiuzulu!Sababu hazijajulikana lakini nafikili ni mfano kama mambo hayaendi unawaachia wengine waongoze.Hii tabia ya watu kung`ang`ania madaraka sio nzuri.Nampongeza huyo mheshimiwa kwa uamuzi kama huo maana baadhi ya viongozi bongo hawajui kitu kama hiyo ni nini na wanafikili kung`ang`ania madaraka ndio njia pekee. Kama unachemsha chomoka
ReplyDeleteNakubaliana na wewe Anonymous wa 11:36 PM. Huyu Bwana ni mchapakazi mzuri tangu akiwa BoT. Yawezekana ame-rub shoulders na wakubwa wa nji!
ReplyDeleteNashangaa kuwa Anonymous 11:36:00 anampongeza huyu bwana!!!!! Huyu bwana ni failure: alipotoka BOT akaenda Akiba Commercial Bank akamess, baadaye akaenda VODACOM aka-blunder, akagombea kituo cha mafuta Kimara na jamaa mmoja akapewa lakini hatimaye kikamshinda. Hapo TANESCO, ulizeni habari zake, mtashangaa!! Sasa anakimbia challenge za EWURA! Kiongozi husimama na kutetea hoja na sio kumangamanga kama huyu. Wenye akili walijua kuwa hatadumu TANESCO, kwa kuwa hapendi/hamudu challenge.
ReplyDeletekisha Fisadi sasa anaanza mbele. Lakini afadhali maana bongo watu hawajiuzulu wala nini....
ReplyDeleteHuyu si ndiyo baba yake Muhamed alikuwa Marekani na Amina pia? Sasa sijui kitaeleweka maana huku U.K inajulikana hao watoto wake waliamua kurudi Bongo ili dad awape mkwanja wa nguvu? Michuzi tupe habari zao kama ni masupa stars pia ama Dingi alikuwa anaimba nyimbo tuuuuu hakieleweki!
ReplyDeletemzee mtendaji huyo itakuwa wanasiasa wanataka kumuingilia au JK anamrudisha kuwa Gavana pale BOT
ReplyDeleteRichmond hiyooo ndio imeanza khabari zake na akina lowasa sasa hivbi utawaona matumbo joto wee ngoja weee........ kudadadadeki
ReplyDeleteNi kweli huyu Mzee Idris Rashid(PhD)ni msomi na hataki mchezo, sasa wanasiasa wa CCM walitaka kuleta Siasa zao katika uendeshaji wa Tanesco basi akaona bora aachie ngazi aachane na upumbavu wao. Tunahitaji wasomi wengi kama yeye wasiokubali kuburuzwa na hawa wanasiasa vihiyo malimbukeni.
ReplyDeleteKi msingi, ameshindwa kazi, na ndio maana daima umeme unapanda juu kila kukicha na wachache wanakula hela badala ya kuendeleza vyanzo vya umeme, kujali maslahi ya wafanyakazi, kufanya maintanance ya vifaa, kutoa huduma bora kwa wananchi nk, sasa acha mambo yawatokee puani,Hongera Dr.Idrisa kwa kukubali yaishe,Tunataka na KARAMAGI afuate mkondo huo, sii kusubiri hadi atolewe kwa reki...
ReplyDeletemimi nadhani tuangalie historia ya shirika ilikotoka, shirika ni tegemezi kwa serikali linajiendesha kwa hasara manake faida yote inalipwa ipt, actually last year losses were around bilion 656 na kwa sasa hasara ni about 65 bilion, mzalendo ameomba application ya kuongeza tarrif kunusuru shirika, na wananchi kulipia haswaa wanachokitumia, na si kwamba ni lazima ni public application wadau wote wanachangia, kwa hiyo muache maneno ya ajabu ajabu ya kusema ooh imemshinda, were u following his track record? amefanikiwa kuvunja makundi kazini na kuwawekea perfomance contract managers and above, mimi nadhani anahitaji muda to change the place, vilevile bill mpya ya umeme ikipita bungeni, watu wengine watakaribishwa kuja kuzalisha, watakapokuja kuzalisha umeme ndio mtaona mtauziwa kwa bei ya hasara ya shirika au kwa bei yao ya kutaka faida, naombeni msome kabla hamjaanza kuropoka, electricity generation is easy but transmission na distribution ndio issue, utagenerate lakini utamuuzia nani ??? unagenerate megawatt 400 mtu anataka kuwasha taa na tv utaishia kumuuzia tanesco apitishe kwenye gridi yake, so acheni longolongo hapa. mzalendo
ReplyDeleteHuyu ni mchapa kazi, na anajua anachokifanya. Walimwambia kuwa TANESCO iendeshwe kibiashara, sasa wanasiasa wakataka kuleta siasa zao ambazo kwenye Balance sheet hazina nafasi. Kaamua kuwaachia Tanesco yenu. I Salute you Dr Idris. OC-Sinza.
ReplyDeleteNI MTENDAJI MZURI NDIO LAKINI AME-RESOLT TO SIMPLEST FINANCIAL SOURCE; PRICE HIKE. WATANZANIA KWA SASA WANA MAISHA MAGUMU KUTOKANA NA MFUMUKO WA BEI SASA KUONGEZA BEI YA UMEME NI KAMA KUWAUA KABISA.NAKUMBUKA MABENKI YALIIKOPESHA TANESCO MABILIONI SIJUI YALIFANYIWA NINI MPAKA BEI ZA UMEME ZIPANDISHWE NDIO SHIRIKA LIPATE PESA!
ReplyDeleteMtoa maoni wa 11.36 pm uko sawa kabisa na waliotangulia hawajui ukweli ulivyo. Dr. Idris hakubali hata mara moja kuingiliwa na siasa ktk utendaji wa kazi, yeye ametoa uchambuzi wa gharama zote ambapo ni wazi bila kuongeza bei shirika haliwezi kuendelea kutoa huduma kwa hiyo ilikuwa serikali iamue kati ya bei kuongezwa, au huduma ipunguzwe au serikali itoe ruzuku ya kutosha na wananchi waendelee na bei nafuu. Yanayosemwa na EURA na bodi ya TANESCO ni siasa ambazo hazina analysis yoyote. EURA wanaendelea na midahalo kwa wananchi ili waeleze kama bei ipande au hapana, hapa jibu la mwananchi linajulikana hata bila mdahalo hakuna anayetaka kulipa zaidi. Ni sawa na kuweka mdahalo kama TRA ipandishe kodi au la. Kuna kiwanda cha saruji kimekatiwa umeme kwa kutolipa na bodi ikaamua urudishwe hizo ni siasa ambazo CEO yeyote aliye makini na hana njaa hawezi kukubali. Inabidi tuamue kama siasa zituongoze au tuwaachie wataalamu wafanye kazi zao. Dr. Idris ni mchapa kazi ambaye hayumbishwi na ninampongeza kwa kukataa kutawaliwa na siasa, ni ziongozi wachache sana Tanzania wa aina yake.
ReplyDeleteHongera sana DR Rashid,tunahitaji wanaume kama wewe katika nchi hii ya wadanganyika.Imekuwa kila kitu nchi hii ni siasa hata kama kinahitaji utaalam.Jamani tufike mahali tukubali mawazo ya wataalamu wetu ili taifa lisonge mbele.KEEP IT UP DR IDRISSA!
ReplyDeleteMUACHE AENDE HATUHITAJI KUFAHAMISHWA ZAIDI, MBONA UMEME HUKATIKAKATIKA NA HATUFAHAMISHWI SABABU ZAKE? NDIO TUSEME HUYO NI MUHIMU KULIKO UMEME? SAFARI NJEMA USIJALI HUENDE UTAUKWAA UWAZIRI SIKU ZIJAZO.
ReplyDeleteNi mmoja kati ya watu makini sana, ni watendaji mzuri na sisi wabongo tulijua kwamba tumepata mtu. Kwa kweli alipoingia kwenye hiyo nafasi alionesha kabisa nia ya kusaidia shirika lipige hatua. Hata alipozungumza alionesha kabisa nia ya ndani kwamba anataka kufanya mambo mazuri.
ReplyDeleteTatizo ni nalijua wengi waliomzunguka sio watu makini na watendaji wazuri. Kwa kifupi TANESCO imejaa watu wasio na elimu, waliofoji vyeti na wenye uchu wa hela!! Mzee wa watu kama ni hela anazo za kumtosha.
Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar
ReplyDeleteHabari Zinazoshabihiana
• Karume: Sifikirii kugombea urais 2010 19.07.2006 [Soma]
• Mfaransa mbaroni kwa kutaka kulawiti msichana 31.12.2006 [Soma]
• Karume ampongeza Chissano 25.10.2007 [Soma]
*Amfokea Hakimu Kisutu wakati akiendesha kesi
*Ainuka kumvaa, wasikiliza kesi, karani wamzuia
Na Rabia Bakari
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, binti wa Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, Bi Fatma Karume, amemtishia kwa maneno makali huku akitaka kumshambulia Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bibi Addy Lyamuya.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mahakamani hapo jana, wakati Hakimu Lyamuya akisikiliza kesi ya madai ya mtoto kati ya Bw. Sadiq Walju na Bi Saeda Hassam ambapo Bi. Fatma alikuwa akimtetea Bw. Walju.
Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo namba 60 ya mwaka jana, ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Bw. Adolf Mahay, lakini baada ya kutokea kutokuelewana na wakili huyo (Fatma), hakimu Mahay alijitoa kusikiliza .
Septemba 20 mwaka huu, kesi hiyo ilipangwa kwa Hakimu Mkazi, Bibi Euphemia Mingi na ilipofika Oktoba 8 mwaka huu, Hakimu Mingi alijitoa kusikiliza kwa kile kilichoelezwa kufokewa mahakamani na wakili Bi Fatma na kushinikizwa kujitoa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoiendesha ipasavyo.
Jana kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa na Hakimu Mkazi, Bibi Lyamuya lakini kutokana na sababu za kimahakama aliiahirisha hadi Januari 13 mwakani.
Baada ya Hakimu Lyamuya kupanga tarehe hiyo, Bi. Fatma aliipinga na kumwambia anataka kesi hiyo isikilizwe Novemba 23 mwaka huu.
Karani alimwambia Hakimu kuwa tarehe iliyopendekezwa na wakili Fatma, imejaa hivyo hakutakuwa na nafasi, ndipo wakili huyo alipopendekeza isogezwe na kusikilizwa Januari 2 mwakani.
Baada ya pendekezo hilo, Hakimu Lyamuya alimwambia wakili huyo kwamba hatakuwa na nafasi tarehe anazolamizisha, hivyo anaomba kujitoa kusikiliza kesi hiyo na badala yake apangiwe hakimu mwingine, mwenye nafasi katika siku hizo.
Kutokana na kauli hiyo, ndipo, Bi. Fatma alianza kufoka mahakamani hapo kwa sauti hali iliyozua tafrani na watu waliokuwapo kubaki wameduwaa kwa kilichokuwa kikiendelea.
"Umeniona kwa mara ya kwanza, hunijui mimi ni nani, nitakuonesha kwanza hujui kazi, nitaandika barua kwa wakuu wako wa kazi," wakili huyo alifoka kwa jazba huku akimnyooshea kidole Hakimu Lyamuya na kumfuata alipokuwa amekaa.
Hata hivyo, Bi. Fatma alizuiwa na karani wa mahakama pamoja na watu waliokuwamo mahakamani hapo, ambao walifanikiwa kudhibiti mtafaruku huo.
Akizungumzia tukio hilo, Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi alisema amepata taarifa ya tukio hilo na atalifanyia uchunguzi.
"Nimepata malalamiko ya wote wawili, yaani wakili Bi. Fatma na Hakimu Lyamuya, nitafanya uchunguzi kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria, zogo wala ugomvi haviruhusiwi mahakamani, hata kama umegombana na mtu msubiri nje ya mahakama si kuleta vurugu ndani ya mahakama," alisema Bw. Mwangesi.
Aidha, Hakimu Lyamuya alisema awali wakati Bi. Fatma akimtolea maneno ya vitisho, alidhani ni utani, lakini alipomwambia kuwa ataandika barua kwa wakuu wake wa kazi, ilibidi awe makini zaidi na jambo hilo.
"Nina mashahidi, maana nimejua kwamba hafanyi mzaha, shahidi wangu wa kwanza ni Bw. Jerome Msemwa, Bw. Jabiri Mkongo, Bw. Juma Magota, Bw. Derick Ngoro na watu waliokuwa mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea," alisema Hakimu huyo.
KWA KWELI KWA MTU YEYOTE MUELEWA ANAEWEZA KUTOFAUTISHA SIASA NA UTAALAM ATAMUUNGA MKONO DR IDRISA. MIMI NAMUUNGA MKONO SANA DR AMEONYESHA JINSI GANI ALIKUA PALE KWA AJILI YA KUTENGENEZA SHIRIKA LIENDE KWENYE MSTARI UNAOTAKIWA NA HAKUA PALE KWA AJILI YA UKURUGENZI YUKOO SAWA HANA NJAA NJAA! HII ITOE FUNDISHO KWA WAKURUGENZI WENGINE WANAOBURUZWA NA WANASIASA. BIG UP DR!
ReplyDeleteHABARI ZA KUAMINIKA ZINASEMA KUWA HAJAJIUZULU NA AMEKANUSHA VIKALI 'UVUMI' HUO
ReplyDeleteLet put it simple and clear, the guy had is own strategic plan, he propose to the stakeholders and they denied it,so he resigned. You can't rise price by 40% while salary rised at 3% annual. You said this guy have a brain? This antique strategic plans which does not have chance in 21 century. You know how to fix TANESCO? Just brake that company into peaces and create competition between themselves, that is how you kill monopoly. This guy was expecting JK to babysit his startegy, no way. You know waht is the effect of rise price by 40%? Iflation. I wounder he was in BOT, and he doesn't care about effect of price change in economy. Bye BYe DR Idrisa, see you.
ReplyDeletePoleni nyie mnaomwelezea huyu Dr Idrisa vibaya maana hakupita kwenu na nadhani hammfahamu utendaji wake wa ndani. Na yawezekana mkawa wale wa kada ambazo aliwabana makoo akiwa kwenye maeneo yenu. Waulizeni wadau wapenda haki, wapenda kazi na wenye uchungu wa nchi kote alikopita, kama hawatawaambia tunaomba arudi kwetu tena!!. Huo ndio uzalendo Hongera Dr Idrisa
ReplyDeleteAMEGUNDUA KWAMBA DENI LA IPTL HALILIPIKI BILA KUONGEZA BEI. OLE WENU WABONGO, MTALIA NA KUSAGA MENO NA IPTL
ReplyDeleteJamani kilichotokea pale hata kama ningekuwa mimi ningejiuzulu. Tanga Cement walikuwa wanaiba umeme! Ilipogundulika hilo ikabidi ibandikwe faini kwa kanuni za Tanesco. Jamaa walikatiwa umeme. Tanga Cement ikafunga kiwanda. M/kiti wa Board ya Tanesco (Kichwa cha siasa) akawa anamsindikiza Dr. kurudisha umeme, Dr. akadai ni heri wachukue cheo chao kulikoni kufanya hivyo . Kwa mantiki hiyo Naungana na Dr kwa 100%, kwani kwa uzoefu wangu wa siku nyingi kama mwl. wa power eng. TZ, viwanda vingi viliwatumia wafanyakazi wa Tanesco wenye tamaa ya pesa kuiba umeme (by pass). Na hii ndo sababu kubwa ya Tanesco kushindwa kupata kipato sahihi.
ReplyDeleteHivi mnaosema kazi imemshinda ukipewa wewe Tanesco utaiweza?
ReplyDeleteNi mafisadi tu ndio wanaoweza kufurahia kujiuzulu kwake na si wengineo. Shirika lilijaa na bado limejaa ufisadi wa kila aina. Wafanyakazi wanaliibia shirika muda wa kazi (badala ya kufanya kazi wanafanya mambo yao), wako wanaliibia kwa kuwauzia watu umeme wa bure, na kuna watu mtaani pia wanalibia shirika hawalipi billi za umeme na wanafanya mambo ya ujanja ujanja wakisaidiwa na na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco. Kuna viongozi wa Tanesco humo ndani ambao wamechangia kulifikisha shirika hapo lilipo.
Hizo ni baadhi ya internal challenges.
Bado kuna external challenges kibao kama kupanda kwa bei ya mafuta, inflation, unapozungumzia inflation kumbuka bei ya vifaa nayo inapanda. Kupanda kwa bei ya gesi, bado kuna Independenty Power Producers ambao wakizalisha ama wasizalishe wanalipwa bili zao kama kawaida na wafanyakazi wao wanalipwa mishahara.
Mizigo yote hii ni kwa kampuni moja Tanesco! Sidhani kama bila ya ruzuku ya serikali hili shirika litasurvive.
Sasa unamwambia mtu hebu jaribu kulisukuma hili dudu angalau lijiendeshe lenyewe kwa kutumia utaalamu wako. Sasa anapoanza kutumia principle za kiuchumi watu wanapiga kelele, wangempa Mganga wa kienyeji labda.
Ifike mahali watu tuwe realistic kuanzia serikali yetu na wengine wote. Iwalipe watu mishahara kulingana na hali ya maisha ili watu waache wizi na watu nao waache bla blah wafanye kazi kuongeza tija ili ipatikane hiyo mishahara mizuri.
Kwa wafanyakazi wa Tanesco, badilikeni shirika hilo likifa ni nyie ambao mtakosa kazi na kuanza kuhangaika kwenye soko la ajira, baadhi yenu mnalihujumu shirika nyie wenyewe kwa kusaidiana na watu wengine kuiba mafuta kwenye transforma, kuwauzia watu umeme kinyemela mkienda kufanya ukaguzi mnawapigia simu "tunakuja kukagua leo usifungue mlango". Wengine madeal kwenye manunuzi ya vifaa na tenda. Mnamkomoa nani?
Na nyie sasa (pamoja na board members wenu) muanze kulipia umeme mnaotumia angalau basi nusu ya bei. Hata muletewe malaika msipobadilika shirika litakufa tu.
EWURA go and learn what other utilities company are doing in other countries. Hao IPP wanapata faida na kuzipeleka makwao tena faida kubwa tu wakati Tanesco ambayo ndio inauza huo umeme inaishia kupata hasara ya mabilioni. Bora hiyo bill huko bungeni ipite sasa sijui mtaifanyaje ile mikataba mliyoiingizia Tanesco ya kununua umeme kwa 20 years mtaivunja au?
Kama kweli amejiuzulu Hongera DR. LAKUVUNDA HALINA UBANI, WAACHIE WENYEWE WAHANGAIKE NALO!
Ameonyesha high moral standards na pi a kwa kukataa political interference
ReplyDeleteNadhani kwa hili anahitaji pongezi
Ni wachache ambao wanajiuzulu katika mazingira kama aliyokuwa nayo Bw huyu.Kudos!
Huo ni mwanzo tu hakika wengi utafuata kwani Bwana lazma asimame na kuonekana maana Tanzania inabidi kumuona maombi ya watakatifu lazma yajibiwe.Huo ni mwanzo tu JK anajua ukweli but anaogopa.
ReplyDeleteWanasiasa wanaharibu nchi kwani wanaangalia masilahi yao binafsi. Ni wanasiasa hao waliingia mikataba ya kizushi kwa Songas na IPTL.
ReplyDeleteAngalia Mtanzania akifanya kitu wanasiasa wanakuja juu walikuwepo makaburu hapa wamekatia wizara na serikali ya zanzibar ikawa ni sawa kwani wazungu wamefanya. Sasa mswahili mwenzetu amefanya wa nasiasa wamekuja juu tunakimbiza wawekezaji jee tutafika kweli kwa kutegemea wazungu wafanye?
Ili tanesco isipandishe bei, kwanza JK abatilishe mikataba ya songas na IPTL kwani haina faida kwa taifa.
Kama Sudani inaua watu Dafur na hakuna umoja wa mataifa itakuwa sisi kuvunja mikataba ya kizushi inayotia hasara nchi yetu?
Hongera sana DR. tupo pamoja
simpongezi huyu jamaa wala nini alipokuwa gavana uchumi ulikuwa mbaya ,ana benki yake na mambo kama hayo INAWEZEKANA KUNA ISSUE NDO MAANA AMEJITOA MAPEMA JK AUENDE KAMATI .hana jipya kwa heli mzee endelea kucheki the comedi
ReplyDeleteAaaaaaaargh!
ReplyDeleteMi nilifikiri Karamagi kajiuzulu kumbe ni Dk Rashid? Naona kashindwa kupandisha bei ya umeme kama alivyotarajia.
Karamagi, Mungai na Msola wamuige.
Bravo DK Rashid
Hongera sana kwa uwamuzi wa busara, ushauri wangu zianzishwe kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme wa uwakika hata kwa bei kubwa wenye uwezo waunganishiwe kwani tumechoka na ubabaishaji wa Tanesco,
ReplyDeleteAh! Tanzania inaudhi! Viongozi hawabadiliki? Majina ya viongozi na sura ni zile zile na kama sio zile ni watoto wao, wajukuu, ndugu au home-boys/men or girls/women it is very stupid!
ReplyDeleteHuyo Idris sijui kwa nini ameresign, lakini ni bora kwake aresign tu. Kwani amekula kashiba!! Nitashangaa sana Rais wetu akimpa cheo kingine! Kwani watu wengine wamekwisha jamani! We need changes we are tired na huo undugunization.