TAARIFA KWA UMMA
Sisi Chama cha wanasheria Tanzania Bara tumepokea kwa masikitiko nakala ya barua kutoka kwa Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu Mh. Addy Lyamuya kwenda kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu kuhusu malalamiko dhidi ya Wakili Msomi wa kujitegemea Fatma Karume kwenye shauri la ndoa kati ya Bwana Sadiq Ahmed Walji (Petitioner) na Bibi Saeeda Hassan (Respondent) leo tarehe 22/11/2007.
Barua hii ilieleza malalamiko dhidi ya Wakili Msomi Fatma Karume ambaye ni mwanachama wa chama cha Wanasheria Tanzania Bara ambaye anatuhumiwa kusumbua mahakama na kuchelewesha kesi kwa vurugu ambazo hazikuwa za lazima tarehe 21/11/2007 katika mahakama ya Kisutu wakati shughuli za mahakama zinaendelea.
Tumeijibu barua ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu na kumhimiza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama wa Kisutu, Mheshimiwa Mwangesi, ayasikilize malalamiko haya ili kuthibitisha ukweli wa tukio hilo kwa haraka. Sisi kama Chama wa Wanasheria tuna wajibu wa kutetea wanachama wetu pale wanapoonewa na pia tuna wajibu wa kuwachukulia hatua kuendana na sheria na kanuni zetu pale inapothibitika kwamba mwenendo wao umekiuka maadili ya taaluma yetu.
Tuko tayari kushirikiana na Mahakama kufikia maamuzi ya kweli na haki. Endapo itathibitika kwamba Wakili Msomi Fatma Karume aliyafanya hayo yanayodaiwa itakuwa ni kitendo ambacho kitastahili kukemewa/kukaripiwa na kutolewa adhabu kwa mujibu wa kanuni za sheria kwa sababu ni kinyume na maadili ya Mawakili ambao wana majukumu kama maafisa wa Mahakama kulinda uhuru, kuiheshimu na kuisaidia Mahakama kufikia maamuzi huru na haki.
Joaquine De-Mello
Rais,
Tanganyika Law Society
22 Novemba 2007
Sisi Chama cha wanasheria Tanzania Bara tumepokea kwa masikitiko nakala ya barua kutoka kwa Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu Mh. Addy Lyamuya kwenda kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu kuhusu malalamiko dhidi ya Wakili Msomi wa kujitegemea Fatma Karume kwenye shauri la ndoa kati ya Bwana Sadiq Ahmed Walji (Petitioner) na Bibi Saeeda Hassan (Respondent) leo tarehe 22/11/2007.
Barua hii ilieleza malalamiko dhidi ya Wakili Msomi Fatma Karume ambaye ni mwanachama wa chama cha Wanasheria Tanzania Bara ambaye anatuhumiwa kusumbua mahakama na kuchelewesha kesi kwa vurugu ambazo hazikuwa za lazima tarehe 21/11/2007 katika mahakama ya Kisutu wakati shughuli za mahakama zinaendelea.
Tumeijibu barua ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu na kumhimiza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama wa Kisutu, Mheshimiwa Mwangesi, ayasikilize malalamiko haya ili kuthibitisha ukweli wa tukio hilo kwa haraka. Sisi kama Chama wa Wanasheria tuna wajibu wa kutetea wanachama wetu pale wanapoonewa na pia tuna wajibu wa kuwachukulia hatua kuendana na sheria na kanuni zetu pale inapothibitika kwamba mwenendo wao umekiuka maadili ya taaluma yetu.
Tuko tayari kushirikiana na Mahakama kufikia maamuzi ya kweli na haki. Endapo itathibitika kwamba Wakili Msomi Fatma Karume aliyafanya hayo yanayodaiwa itakuwa ni kitendo ambacho kitastahili kukemewa/kukaripiwa na kutolewa adhabu kwa mujibu wa kanuni za sheria kwa sababu ni kinyume na maadili ya Mawakili ambao wana majukumu kama maafisa wa Mahakama kulinda uhuru, kuiheshimu na kuisaidia Mahakama kufikia maamuzi huru na haki.
Joaquine De-Mello
Rais,
Tanganyika Law Society
22 Novemba 2007


Habari za huyu wakili Fatma Karume nimezisoma leo kama ilivyoripotiwa na Happiness Katabazi na zimeniskitisha sana!
ReplyDeleteKama watoto wa vigogo (maana huyu ni binti wa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar) watakuwa wana tabia kama hizi mpaka mahakamani wanaonyesha ni kiasi gani walivyolelewa.
Naipongeza Tanganyika Lawa Society kama kweli wameliona hilo na ningependa vile vile watuambie kwenye mtandao ni hatua gani wamechukua!
Wataalam wanasema tabia nyingi anazokuwa nazo mtoto mara nyingi sana, kwa bahati mbaya au nzuri, zinaakisi tabia za wazazi wake wote.
Naomba kutoa onyo kuwa suala la Wakili Fatma Karume lisichanganywe na siasa au kumhusisha Baba yake.
ReplyDeleteHili ni Suala lake binafsi Fatma kama Wakili.
Nimeshaona kuwa suala hili linachukuliwa kama ni suala la kisiasa, kutokana commets zilizokwisha tolewa kwa njia mbalimbali.
Haki itendeke kwa Wakili na Hakimu pia.
Tusiwahukumu wazazi wake kama vile ndio waliomtuma avurunde kazi, na kunyea kitumbua chake mwenyewe.
ReplyDeleteNa wala asiadhibiwe vikali au kidogo eti kwa sababu baba yake ni rais. Sheria, taratibu na kanuni zichukue mkondo wake.
Kama ni kweli amefanya yaliyosimuliwa na amekuwa na kawaida hiyo mpaka anatishia Mawakili / Mahakimu wengine
1.Basi asimamishwe kwa muda (kama atakiri makosa na kuomba msamaha) au anyang'anywe kabisa leseni ya kufanya hiyo biashara yake ya kukaripia wenzake na kutamba chini ya kivuli cha uanasheria uchwara!!
2. Hakimu / Mahakimu wengine wowote waliohusika kutomkemea au kumshauri siku zote hizo mpaka akawa tishio au sugu wapewe maonyo ya maandishi (reprimand) ili wawajibike ipaswavyo bila kujali nasaba wala hali ya familia ya Mtendaji anayekiuka maadili ya kazi yake.
Advocate Nyakarungu
Naomba mtu anisaidie hili la Wakili Msomi...... naona limetumika sana Je ina maana ninayofikiri au kwa kiingereza ina maana nyingine?
ReplyDeleteJamani heri ya JINI MAKATA anayekuja kuchukua roho na kuishia nayo......cha kuogopa hapa duniani ni kulilea hili PEPO LA HASIRA.....hili ni la kulikemea kwa nguvu zote ulizopewa duniani ili lisikutawale....Leo hii yuko wapi DITOPILE....yaani namsikitikia huyu binti jamani...(PEPO LA HASIRA HALINA SUBIRA WALA SIMILE.....VERY RIGID)....haya mwenzetu...soma yote hiyo!!!...YANI UELEWE UMEMDHALILISHA HATA BABA YAKO NA BABU YAKO MZEE KARUME.....POLE SANA.....tuzidi kuomba kupambana na PEPO LA HASIRA
ReplyDeletePoor girl......usijali....zidi kuomba na mwenyezi mungu atakisikia kilio chako....Hao watakaokukashifu ni MAPEPO vilevile...na yana matatizo kuliko wewe.....hivyo tulia usali na umuombe mwenyezi mungu alifukuzie mbali hilo PEPO LA HASIRA.....yaani hapa kinachoonekana cha wazi wazi mdogo wangu...UMEUA PROFFESSION YAKO....Pole lakini usijali
ReplyDeleteWakili Fatma Karume ameongea na radio clouds leo asubuhi kuhusu sakata hili, kwa maoni yangu hakupaswa kwenda ktk radio wakati tayari amelalamika kwa hakimu mkuu mkazi naona kama anatafuta public support & sympathy sijui kwa wanasheria kama jambo alilofanya la kwenda ktk radio ni sahihi na hata anavyojieleza ktk radio ni wazi anaonyesha ni mtu wa namna gani. Ngoja tuone sheria zinasemaje kwa masuala haya!!
ReplyDeleteashughulikiwe ipasavyo, sheria ichukue mkondo wake, kuwa mtoto wa Rais isiwe sababu. Wamepita watoto wa marais wangapi hatujasikia wakifanya vituko kama vyake. Ashughulkiiwe ipasavyo.
ReplyDeletelabda mnisaidie wadau wenzangu kwanini huyo Fatma alizua hilo tafrani mahakani tukishajua hilo ndio tunaweza kujua moja kwa moja why did she do that.
ReplyDeleteHuyu dada nafikiri kama si kiburi basi nafikiri
ReplyDeleteakili yake si nzuri!!!!Nafikiri pia hata mawakili wenzangu wanachama wa TLS tunatambua hili! Ni mara ngapi amekuwa akitukana mawakili mahakamani pale wanapomshinda kesi? She is NOT professional! Isitoshe, ni mara ngapi tumeshuhudia akiwaonyesha dharau ya dhahiri Ma-Judges wetu? Imefika hatua ambapo hata Judges hawataki kusikiliza mashauri yanayosimamiwa naye. Mawakili wote tunalifahamu hilo. Amekuwa pia akionyesha utovu wa nidhamu na dharau ya hali ya juu mahakamani na ni mtunzi mzuri wa uongo. Nafikiri tunakumbuka kuna wakati alishawahi kutunga UONGO mkubwa dhidi ya Judge mmoja bahati nzuri jambo hilo lilikuwa wazi na wote waliuona uongo wake. Nafikiri kwa sasa itakuwa vizuri aadhibiwe na chama cha Wanasheria (TLS). Siombei afukuzwe ila angalau awe suspended nafikiri akirudi atakuwa na nidhamu.
Fatma maezungumza kwenye radio clouds asubuhi ya leo,tumemsikia!
ReplyDeletebado nashangazwa na fatma akiwa kama mwanasheria approach aliyotumia kutatua tatizo lilokuwa likimkabili mteja wake.
anazungumzia kuwa mteja wake aliombwa rushwa,kwanini akuarrange(mtego) na PCCB wamkamate huyo hakimu?
inaonekana fatma alifanya aliyoyafanya kwakuwa tu alijua kuwa hatofanywa lolote na na vyombo vya dola kwa kuwa yeye ni binti wa kigogo!
wewe na mimi hatuwezi kufanya hivyo.
kwenda kwenye radio ya clouds na kutoa tape recorder ya hakimu akiomba rushwa hilo nalo kisheria sijui limekaa aje!?
binafsi nahisi yeye mwenyewe fatma analichukulia swala hili kisiasa zaidi badala ya kulishughulikia kwa mujibu wa taaluma yake ambayo ndiyo njia muafaka,na lazima taratibu zifuatwe,siyo kwakuwa wewe ni mtoto wa rais kosa la rushwa unaenda kushitaki kwa waziri hatashindwa kukusaidia!
Huyu Fatma Karume ndio zake...Very rude woman. Hata akiwaanaongea kwenye maongezi yake lazima atasema mara kwa mara you know we Karume's.... Kusema kweli nimekilaani kitendo chake cha kumtukana na kutaka kumpiga wakili. Tabia gani hii jamani. Shame on her
ReplyDeleteKwa kweli huyu dada ashughulikiwe kabisaaa. Kwanza leo asubuhi kwenye kipindi cha Clouds ameonyesha jinsi asivyo na ETHICS. Suala lake tayari lilikuwa linashughulikiwa, sasa clouds ndiyo waamuzi? Tena alikuwa anajisifia jinsi alivyo na mdomo wa kuongea. Haki itendeke, asionewe ila asiachwe aendelee na tabia hiyo
ReplyDeleteJAMANI MBONA HAPA MNAMUONGELEA FATMA TU? TENA MBONA AMEKUWA NA SUBRA SANA? ME MTU AKINIONYESHA KIDOLE KUWA SINA AKILI NAMTIA KIBAO ILI ATIE AKILI, NA MBONA HAMUONGELEI HIZO RUSHWA ALIZOKUWA AKIZICHUKUA KWA MTEJA WA FATMA?
ReplyDeleteME NINA MIKASA MINGI YA MAHAKAMANI JAMANI, SIMLAUMU HUYU DADA, KUNA ULASIMU SANA, YANI USIKUTE NA YEYE ALISHACHOSHWA NA MAMBO YA MAJAJI, FATMA KAZA BUTI, ONGEA HATA UKITAKA WEKA MHADHALA JANGWANI UTANGAZE, HAYA MAZEE YAMECHELEWA KUJENGA NYUMBA HUKO ZAMANI SIKU HIZI YANATATUFA KUJENGA KWA NGUVU KAZI KULA HELA TU ZA WATU..KUDADADEKI!!!
NA MSIMTAJE BABAKE HAPO, WALA HAKUWEPO MZEE WA WATU, NYIE MTAJENI FATMA TU, MAMBO YA MTOTO WA RAISI ONDOENI!! HAYO YOTE MADONGE TU, NA NYIE BABA ZENU WAWE MARAISI BASI
MKELEKETWA!!!
muacheni dada wa watu, bongo mtu akishasema ukweli tu mnamjia juu, kuficha mambo ndo kunasababisha hata watu wanapoteza maisha yao, ni sawa na wale waliopasuliwa vichwa na miguu, mnaogopa kusema ukweli kuwa madaktari wanapokea rushwa matokeo yake ndo hayo, Fatma sema tu!!! tuko nyuma yako sie mawakili wasomi!!!
ReplyDeletehapo huyo hakimu alikuwa anabania hiyo tarehe ili apewe chochote aweze kuichomeka kwenye tarehe za karibu, sasa kaona kashikiwa bango ndo mana kaja juu!!
Wala hajaua professional yake popote, sana sana waaandishi wamempa jina na kumtangazia business, safi sana, nimempenda huyu dada yuko fit!!
ReplyDeleteMwenye kulia na alie, binti kajitaidi kajiimarisha na kajitoa kimasomaso ili kutetea haki!!! sisi kama wazazi tunamuunga mkono, fikiria usiweze kumuona mwanao kwa muda mrefu halafu eti hakimu kwa sababu zake tu anasema haiwezekani mpaka tarehe anayotaka yeye, ingekuwa yeye ndo mwenye kutamani kumuona mwanae angeweza?
Hovyoooo!!!
Michuzi unanionea. tafadhali toa Komenti yangu niliyokuandikia.
ReplyDeleteNilijitahidi sana ku-control hasira zangu ili nitoe lugha ya matusi na kwa kweli sikutukana. sasa mbona hujaitoa?
Tafadhali usinionee. Itoe
yeye ni mdogo sana kwenye hio fani ya uwakili comparéd to the people aliowatolea lugha mbaya yaani majaji. ni kosa liĺilokuwa wazi, ni kitu kidogo sana kuomba samahani kwa aliotumia lugha chafu kwao, akÃrà makosa yake na jamii itamuona mtu mwenye busara, kuliko kukimbilia vyombo vya habari, na kosa lipo palepale, anazidi kulipa uzito.
ReplyDeletethis Fatma anahitaji kupigwa mti. Hako kamdomo dawa yake moja tu, tia mti ndani tuone kama atang'ata au atameza.
ReplyDeleteanony wa 9:42, 9:46 na 9:51 wote ni mtu mmoja unayetaka kutetea maovu. Tumekushitukia! na wote wanaosema Wazazi wake waondolewe katika hili wana lao jambo. hii yote ni MALEZI tu ya kujiona above all. mtoto wa kimasikini aliyekuwa na kusoma kwa shida na kukipata cheti chake kwa shida na sio kwa jina la baba yake asingediriki kudharau mahakama namna hio! acheni kutetea uovu.
ReplyDeleteSTUPID GIRL. LEARNED YOU ARE NOT! SHAME ON YOU AND THOSE WHO BROUGHT YOU UP. YOU BRING SHAME ON YOUR CHILDREN. POOR THEM. THEY WILL HAVE TO BEAR THE BRUNT OF YOUR PIGHEADEDNESS FOR YEARS TO COME. WAKE UP! ACT RESPONSIBLY. THINK BEFORE YOU ACT. ACHA JAZBA. KITAKUPELEKA WAPI????
ReplyDeleteJamani wadau wa globe hii ni vema tukaa kimya bila hata ya kumhukumu Fatma kwa hili!Hapa naongelea kwa wale ambao wamemhukumu huyu dada kwa kile kilichotokea pale Kisutu Mahakamani.Ingelikuwa hukumu za namna hiyo basi Dito Mwana wa Mzuzuri siangelikuwa shanyongwa sasa hivi?Tusiwe majaji wa suala hili watu wachache sana waliokuwepo pale mahakamani ile siku including Fatma mwenyewe na Hakimu ndo wanajua ukweli si yetu masikio tusubiri uchunguzi ufanyike!Manake Wabongo tumezidi kwa bendera fata upepo,Juzi tetesi za kujiuzulu Dr zilipotangazwa alipojitokeza mmoja tu kumponda wote tulimponda,leo kaukweli kameanza kupatikana watu washabadilika ooooooo wanaingiza siasa amini nawaambieni ikijajulikana Fatma hakukosea wote tutaanza kulaani Mahakimu!Tujifunze kuwa na subraaa.
ReplyDeleteNimekidharau hata hicho chama cha wanasheria, sasa kung'ang'ania kumuita wakali msomi ndiyo nini? Hana adabu, hata kama hakimu alifanya kosa hiyo haikuwa njia nzuri ya huyo "msomi" wenu kutatua tatizo? Halafu jamani tuacheni utani, si kila mtu tu anaweza kuwa wakili kwa sababu tu kulikuwa na hela za kumsomesha, acheni hizo.
ReplyDeleteNaona tusubiri ukweli. Tusisikilize hadithi za upande mmoja na kumhukumu huyu kwa vile ni mtoto wa baba
ReplyDeleteMahakimu bongo wana nyondo sana na mawakili vile vile sasa hapo hatujui nani nyodo yake ilizidi kamba
Hujui kilichokua kila mfanya kila hakimu kukimbia kuhukumu hiyo kesi. Mind you huyo ni hakimu wa tatu aliyekua anaisogeza mbele hiyo kesi au kutafuta sababu ya kutoisikiliza..
Tusubiri tu ukweli
pamoja na mdai ya rushwa aliyoyatoa fatma,sijui mnalionaje suala la yeye kulazimisha kesi yake isikilizwe siku anayopanga yeye!je huu ni utaratibu wa wapi?
ReplyDeleteje kila mtu akienda mahakamani na kulazimishwa siku anayotaka kesi yake isikilizwe si itakuwa vurugu?
fatma ni msomi,tena wa sheria,na taratibu za mahakama anazijua,nini kilimpa jeuri ya kufanya fujo zile kama si jina?
huyu binti ni arrogant anaona mahakimu wetu na hata majaji hawajui wajibu wao ila yeye ndie anaejua kila kitu lazima awe displined!
ReplyDeleteFatma alitoa tuhuma hizo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima jana jioni wakati alipotakiwa kueleza kile kilichotokea katika mahakama hiyo juzi na uamuzi wake, baada ya Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kutoa tamko la kusikitishwa na tukio hilo na kutaka uchunguzi ufanyike.
ReplyDeleteWakili huyo, alisema baadhi ya mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanajihusisha na vitendo vya rushwa, jambo aliloeleza kuwa alikuwa tayari ameshalitolea malalamiko yake rasmi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Akizungumzia matokeo ya mzozo wake huo wa juzi, Fatma alisema alikuwa tayari kukabiliana na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu tu ya kupigania haki anayoamini alidhulumiwa katika misingi isiyofaa.
“Niko tayari hata kufutwa uwakili. Natetea haki yangu ambayo naamini nilinyang’anywa, nimeingia kufanya kazi hii kwa sababu ya kutetea wananchi, hivyo siwezi kuona nikidhulumiwa nikanyamaza kimya. Enzi za utumwa zilishapitwa na wakati, ni bora nikalime nazi kuliko kupoteza haki yangu,” alisema Fatma kwa kujiamini.
Alisema hata kama yeye ni mtoto wa rais, bado anayo haki ya kudai kile anachodhani anadhulumiwa, kwani naye ni mtu kama walivyo watu wengine, na kimsingi akakataa suala lake kuhusishwa na urais wa baba yake.
Kuhusu kuwapo kwa rushwa, binti huyo wa Rais wa Zanzibar alisema anao ushahidi wa kutosha unaomuonyesha mmoja wa mahakimu waandamizi wa mahakama hiyo akiomba rushwa kutoka kwa mteja wake, Sadiq Walji.
“Ninao ushahidi wa uhakika hakimu (alimtaja jina), aliomba rushwa (akataja kiasi cha fedha zilizoombwa na hakimu huyo)…tena alimfuata mteja wangu katika Hoteli ya Sea Cliff Agosti 26 mwaka huu, na alimpatia fedha na akamrekodi bila ya yeye kujua ‘tape recorder’ (kinasa sauti). Hili ushahidi wa sauti yake tulishauwasilisha Takukuru na wamelifanyia uchunguzi kwa muda mrefu.
“Nasema hivi, Mahakama ya Kisutu inanuka rushwa. Inahusisha mahakimu na waendesha mashitaka. Rushwa imetawala pale, tena huyo hakimu kesho (leo) anapelekewa barua yake…mimi siyo mwehu hata kidogo, nasema hili kwa uhakika na serikali na watu wote wajue kuwa Mahakama ya Kisutu pana rushwa kila mahali,” alisisitiza wakili huyo wa kujitegemea.
Akizungumzia madai ya kufanya fujo ndani ya mahakama wakati kesi inaendelea, wakili Karume aliyefika kwa ajili ya kumuwakilisha Walji, kwenye kesi namba 60/2006 ya madai ya mtoto wa miaka miwili iliyokuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mwandamizi, Addy Lyamuya, alisema hakimu huyo alimkosea, hali iliyosababisha malumbano.
Alisema, Hakimu Lyamuya alitaka kuipanga kesi hiyo tarehe za mbali bila sababu za msingi, jambo ambalo wakili Karume alipingana nalo kwa kuwa Hakimu Adolf Mahay, alikwishatoa uamuzi Agosti mwaka huu kuwa mtoto huyo wa mteja wake anayeishi kwa Saeeda Hassam , awe akiruhusiwa kila Ijumaa kwenda kwa baba yake na kurudishwa kwa mama yake Jumapili.
Fatma alisema licha ya uamuzi huo, mama wa mtoto huyo alikuwa akikaidi amri hiyo, hali ambayo ilimfanya yeye awasilishe ombi la kutaka mwanamke huyo achukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kuidharau amri halali ya mahakama hiyo.
“Licha ya kumuomba hakimu aipange leo, alikataa na kunijibu kwa ukali na akanionyeshea kwa ishara kwamba mimi ni mwendawazimu….nikamuuliza, madaraka hayo nani kampa ya kunionyeshea kwa ishara mimi ni mwendawazimu? Akaanza kuniambia nisimpangie kazi…nikashikwa na hasira na kutoka mahala nilipokuwa nimesimama na kumwambia zama za utumwa zilishapita katika nchi yetu, hivyo siwezi kukubali kuona navunjiwa heshima nikanyamaza kimya na nikamweleza kabisa nakwenda kumshitaki kwa wakubwa wake wa kazi.
Alisema baada ya kumweleza maneno hayo, hakimu alikwenda kumshitaki kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangesi na pia alikwenda kumshitaki kwa Jaji Kiongozi Amir Manento lakini hata hivyo alisema malalamiko yake hakuwa ameyapeleka kwa viongozi hao kwa maandishi.
“Licha ya kumweleza yote haya, hakimu hakutaka kunisikiliza na badala yake akanionyeshea kwa ishara kwamba, mimi ni mwendawazimu….ndipo nilipomweleza kwamba hawezi kazi na kwamba naenda kumshitaki kwa wakubwa wake wa kazi,” alisema Karume.
Fatma alisema pia kuwa, juzi asubuhi alikwenda kumshitaki Lyamuya kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangesi, pia alikwenda kumshitaki kwa Jaji Kiongozi, Amir Manento, lakini hata hivyo alisema malalamiko yake hakuwa ameyapeleka kwa viongozi hao kwa maandishi.
“Habari zilizoandikwa jana kwakweli zimeniumiza sana…kwani Lyamuya aliniita mimi mwendawazimu na mbaya zaidi, Mahayi anasema kwamba alijitoa kwenye kesi ninayoitetea kwa sababu nilimfokea. Haya mambo si ya kweli,” alisema Fatma katika mahojiano jana.
Katika tukio la juzi, Fatma alikuwa akituhumiwa kutoa maneno makali dhidi ya Hakimu Lyamuya, hali iliyodaiwa kusababisha hakimu huyo ajitoe kuendelea kusikiliza kesi inayomhusu mwanasheria huyo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea katika chumba cha mahakama, wakati hakimu huyo alipotaka kuanza kusikiliza kesi ya madai namba 60/2006 ambayo ilianza kujadiliwa na hakimu huyo juzi hiyo kwa mara ya kwanza, tangu apewe jalada hilo.
Katika kesi hiyo, Fatma anamwakilisha Sadiq Walji, ambaye ni mdaiwa katika kesi hiyo ya madai ya mtoto. Mdai katika kesi hiyo namba 60/2006 ni Saeeda Hassam.
Kabla Hakimu Lyamuya kuanza kusikiliza kesi hiyo, Wakili Fatma, aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo.
Kutokana na hali hiyo, hakimu alimtaka karani wake kuangalia kwenye kitabu cha kumbukumbu (diary) kama siku hiyo itafaa kusikilizwa kwa shauri hilo. Hata hivyo, karani alimweleza hakimu kuwa siku hiyo zimepangwa kesi nyingi za kusikilizwa, labda waipange Januari 13, mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa za juzi, Hakimu Lyamuya alikubaliana na maelezo ya karani wake na kumweleza wakili huyo kwamba kesi hiyo itasikilizwa tarehe hiyo.
Baada ya hakimu kupanga tarehe hiyo, Wakili Fatma anadaiwa kuwa alianza kufoka kwa sauti ya juu akitaka mahakama isikilize kesi hiyo jana jambo ambalo Hakimu Lyamuya alilikataa kwa kueleza kuwa hakuwa na nafasi.
Wakili huyo aliendelea kuomba mahakama kupanga kesi hiyo Januari 2 mwakani, ombi ambalo hakimu huyo alilikataa na kumweleza tarehe hiyo mahakimu watakuwa mapumziko, ndipo wakili huyo alipoanza kutoa kauli kali dhidi ya hakimu huyo.
“Kwanza wewe hujui kazi na ni mara yako ya kwanza kuniona mimi… hunijui ni nani, sasa nitakuonyesha… nitaandika barua kwa wakubwa wako wa kazi na kuwaeleza kwamba hujui kazi,” alidaiwa kusema Fatma hiyo juzi.
Kutokana na tafrani hiyo, mahakama ilishindwa kuendelea kusikiliza shauri hilo wala kulipangia tarehe na badala yake jalada la kesi lilirudishwa kwa uongozi wa mahakama hiyo, ili limpangie hakimu mwingine kusikiliza kesi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tafrani hiyo juzi, Hakimu Lyamuya, alisema ameshangazwa na vitendo vya utovu wa maadili vilivyoonyeshwa na wakili huyo na kueleza hajafikiria kuchukua uamuzi wa kumfungulia kesi.
After reading the papers for the past 3 days, the system seems to be corrupt and nobody cares about the rights of the citizens. A 2yr old child is suffering between the parents. An order has been issued by the court of law to allow the child to see the father BUT nobody is taking any action against a citizen who is in contempt of court but the same magistrates are playing games instead of ensuring that the order is followed.
ReplyDeleteIF A LAWYER IS HAVING SO MUCH DIFFICULTY FIGHTING CORRUPTION AND FOR PEOPLE'S RIGHTS, HOW CAN A NORMAL CITIZEN FIGHT FOR HER/HIS RIGHTS???
kwenye gazeti la "Habari Leo" la siku ya leo, 24/11, imeripotiwa kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Kisutu amemaliza uchunguzi na ametoa matokeo kuwa Bi.Fatma alikiuka taratibu za kimahakama kwa kuingia,kumnyooshea kidole na kumtukana Hakimu Lyamuya na kwamba ripoti yake ameipeleka kwenye ngazi za juu kwa ajili ya action zaidi. mimi naona hizo ngazi za juu hazina haja ya kufikiria zaidi ila kum-suspend Bi. Fatma kwakuwa yeye mwenyewe alikiri kuwa alifanya vitendo vya utomvu wa nidhamu wakati wa mahojiano katika redio clouds. hakuna ushahidi mwingine mzuri zaidi ya kauli yake hiyo. Labda aikatae kauli yake hiyo na kudai kuwa alikuwa hana akili timamu au alikuwa amelewa au alilazimishwa kusema aliyoyasema wakati wa mahojiano hayo. Hata chama cha wanasheria hakina haja ya kufanya uchunguzi kwani ushahidi upo na kama watahitaji clip ya interview iliyofanywa na clouds wanaweza kuiomba ili kuthibitisha kauli za Wakili Bi. Fatma. Kwa kweli huyu Wakili amedhalilisha sana legal profession. Inajulikana kuwa Wakili pamoja na mambo mengine anatakiwa kuwa mvumilivu na kama imeshindikana basi afuate taratibu zilizopo kutatua tatizo. Kwa bahati mbaya sana Bi. Fatma hana uvumilivu na rekodi yake ya nidhamu mbele ya majaji, mahakimu na mawakili wenzie sio nzuri sana na hivyo kuzidi kuleta wasiwasi kama kweli Fatma ni wakili makini anayetambua etiquettes za uwakili.Namsikitikia sana yeye binafsi, lakini zaidi ni wale wote ambao dhahma la Fatma limekwishawakumba na pia wateja wake ambao inabidi wajiulize sana kuhusu utendaji wa Wakili wao.
ReplyDeleteNDUGU ZANGU WATANZANIA MIMI NASIKITISHWA NA WATANZANIA WENZANGU AMBAO WANAMSIFIA FATMA KARUME,MIMI HUYO FATMA KWA KWELI AMENISIKITISHA SANA AMEIABISHA MAHAKAMA, AMEMUABISHA HAKIMU AMBAYE NI MOJA WA MAHAKIMU WA ZAMANI NA WENYE UZOEFU NA KAZI HIYO,AMEKIAMBISHA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA, BWANA MICHUZI KISHERIA FATMA ALITAKIWA KWENDA JELA KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA STRAIGHT AWAY TENA HUYO HAKIMU AMEMUESHIMU SANA YAANI SHERIA IKO VERY CLEAR PALE ALITAKIWA ATANDIKWE SIX MONTH IN JAIL HAKIM ALITAKIWA ASEME TU PUT HER IN JAIL WAKATI ANAPELEKWA JAIL HUKU HAKIMU ANAANDIKA CHARGE YAKE,BWANA MICHUZI FATMA AMEONYESHA NI JINSI GANI MAADILI YAMEPUNGUA KWENYE VYOMBO VIKUBWA KAMA HIVYO HIVI SASA KAMA WAO NDIUO WASIMAMIZI WA SHERIA WANAFANYA HIVYO SISI WANANCHI WA KAIDA KWENYE SAKATA LA BOT, MADINI,UNGEKUTA NA WANANCHI WANAJICHUKULIA SHERIA MKONI TUNGEKUWA WAPI? KWA KWELI KWA KOSA HILI DADA HUYU AKISHINDA KWELI TUTAJUA SHERIA NI KISU SIO MSUMENO MANAKE TAYARI HUYO MWANASHERIA SIO MARA YAKE YA KWANZA KUFANYA KITENDO CHA UTOVU WA NIDHAFU.
ReplyDeleteKWA USHAURI WANGU MIMI NAPENDA SANA HUYU DADA AENDE KWENYE COURSE INAYOITWA ANGER MANAGEMENT HIYO ITAMSAIDIA SANA KUWEZA KUCONTROL HASIRA ZAKE NA PIA ITAMKUZA KIPROFFESIONAL NA PIA ITAMJENGEA TABIA AMBAYO KILA MTU ATAPENDA KUIGA AU KUJIFUNZA KUTOKA KWAKE, KAMA AKISHINDWA KUPATA HIYO COURSE HAPA NCHINI MIMI NIKO TAYARI KUJITOLEA NIMPATIE COURSE HIYO BILA MALIPO YEYOTE REAL FROM MY HEART I WILL DO IT FOR HER AS PART OF MY CONTRI IN THE THE SOCIETY, NIMEANDIKA NA KIZUNGU KUONESHA MSISITIZO.
ballyathanas@hotmail.com
KIPEPEO
Kuna kasumba fulani haswa miongoni mwa baadhi ya watanzania waliosoma na wenye uwezo, wanafikiria wako juu ya kila kitu, hawaheshimu mahakama wala kitu gani, sheria hawazitambui. Sasa huyu binti yeye ni mwanasheria kwa nini anakuwa na nidhamu mbovu namna hii, tena mbele ya mahakama.
ReplyDeleteHasira kila mtu anayo, na kazi kila mtu anaijua kazi yake kwa hiyo asijichanganye hapa kufanya ujinga kupoteza kibarua chake. Hivi ni nani kwa akili yake atakayekubali kuwakilishwa na mtu kama huyu.
Akiwa mwanamke angetakiwa kuwa mfano bora, na sio kuonyesha kuwa wanawake hawana control over their emotions, tunataka kuelimisha wanawake zaidi na sio kuwarudisha nyuma kwa mifano mibaya kama hii.
Tena ana bahati alikuwa anatakiwa kuwa jela saa hizi. Lakini kwa vile baba yake ni mtu mkubwa aah , ana RUKSA kuitukana sheria.
Binti wa Karume sasa auanika mtandao wa rushwa Kisutu.
ReplyDelete*Adai haki inauzwa, wanyonge wanaonewa
*Akiri anajua ni msalaba mzito, lakini ataubeba
*Asema hana tatizo na Mahakimu, bali rushwa
*Asema mteja wake alitishiwa kwa kesi ya Babu Seya
Na Hassan Abbas
SIKU chache baada ya kutokea hali ya sintofahamu kati yake na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bibi Addy Lyamuya, Wakili wa Kujitegemea ambaye pia ni binti wa Rais Amani Karume wa Zanzibar jana amefanya mahojiano maalum na gazeti hili na kusisitiza kuwa hana ugomvi na hakimu yeyote bali anapigania haki za wanyonge, wanaolazimika kununua haki kwenye mahakama hiyo.
Fatuma katika mahojiano hayo, amewabainishia Watanzania kuwa yeye kama wakili aliyefundishwa vyema maadili ya kazi yake na pia anayeenzi wosia wa babu yake, hayati Mzee Abeid Amani Karume, siku zote amefundishwa kupigania haki inapotaka kuchafuliwa na ubatili.
"Nilipoanza kulishughulikia suala hili, nilijua utakuwa msalaba mkubwa kwangu, lakini kama babu yangu alivyokuwa jasiri kiasi cha kuwaongoza Wazanzibar kupata haki zao, nami nimejifunza kutonyamazia uovu," alisema wakili huyo ambaye jana aliuweka hadharani mtandao wa rushwa ulioenea katika mfumo wa mahakama hasa kwa baadhi ya Mahakimu wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam na kuitaka jamii ilijadili tatizo hilo.
Chanzo cha yote
Anasema yeye kimsingi anaifanya kazi ya uwakili ikiwa ni sehemu ya wito wake binafsi aliokua nao tangu mdogo wa kutotaka kuona wanyonmge wanaonewa.
"Nilipoanza kazi hii nilikuwa natetea sana wanyonge hasa katika hizi kesi za madai na mambo ya ndoa, lakini nikaziacha na kujihusisha zaidi na masuala mengine," alianza kusema.
Akaongeza kuwa hata hivyo kutokana na kuwa na moyo wa huruma akajikuta akishindwa kukwepa kuwatetea wanyonge hao kila walipomfuata awasaidie.
"Hata hii kesi ilipokuja, kimsingi mteja wantu ni mtu wa kawaida, lakini nikajitoa kama sehemu ya wito wangu nimsaidie apate haki yake ya kuonana na mtoto wake mpendwa," aliongeza.
Wakili Fatuma akieleza msingi wa kesi hiyo, aliliambia gazeti hili kuwa inahusu baba na mama waliotengana ambapo mume ambaye ndiye mteja wake, aliiomba mahakama awe na fursa ya walau kuonana na mwanae kwa siku chache katika wiki.
"Nilimtetea katika kesi hiyo na Agosti 2, mwaka huu tukashinda. Hukumu ilimpa haki mteja wangu ya kuwa na mwanawe kuanzia kila Ijumaa kisha Jumapili awe anamrudisha kwa mama yake," alifafanua.
'Kansa' yaanza
Wakili Fatuma akiwa anaonekana mwenye huzuni, alisema wakati mteja wake akifuatilia hukumu hiyo ndipo alipoanza kuombwa rushwa ili hati ya hukumu yake isainiwe na akalazimika kutoa.
Anasema katika tukio la pili, baada ya kupewa hukumu yeye akiwa wakili alibaini kuwa mteja wake hakuwa amepewa hati ya amri ya mahakama na akamshauri aende tena Mahakama ya Kisutu kuiomba ili aweze sasa kuanza kupata haki yake ya kuwa na mwanawe.
"Alipofika kwa Hakimu akaambiwa alichotoa siku ya kwanza kilikuwa hakitoshi. Akajipapasa na kutoa alichokuwa nacho lakini bado akaambiwa hakitoshi.
"Hii ni aibu kwa taifa hili kwa msimamizi wa haki kufikia hatua anauza haki namna hii," alisema wakili Fatuma na kuongeza: "Yule mteja wangu akawa ameishiowa hela hivyo akamwomba rafiki yake aliyekuwa akisubiri nje ya mahakama amsaidie."
Akaongeza kuwa jamaa huyo alilazimika kwenda benki ya Barclays na kutoa dola 100 ambazo walimkabidhi Hakimu huyo.
"Huyu jamaa aliyekwenda kutoa fedha zake benki ili amsaidie mteja wangu, yupo na yuko tayari kutoa ushahidi," alisema.
Wakili Karume akieleza jinsi Mahakamu walivyofikia hatua ya kuwa na mtandao wa aina yake wa kudai rushwa na ambao unawakera wananchi wengi, anasema baadaye kesi hiyo ilichukua taswira nyingine tena kufuatia mawakili wa upande wa mke kuwasilisha maombi ya kutaka kesi hiyo ifanyiwe marejeo kwa kuangaliwa upya.
Anasema Hakimu huyo (jina tunalo), alimpigia tena simu mteja wake na kumtaka waonane kwenye hoteli ya Sea Cliff.
"Mteja wangu alisita kwenda kwa sababu alikuwa akijua huko angeendelea kuombwa hela zaidi. Hakimu yule akatuma hata sms (ujumbe mfupi wa maandishi) ambao tunao kama ushahidi akimsisitiza mteja wangu waonane," aliongeza.
Sea Cliff-Agosti 26, 2007
Wakili Fatuma anasema kuwa kabla ya kwenda kuonana na Hakimu huyo kwenye Hoteli ya Sea Cliff iliyoko pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam, mteja wake alimpigia simu na kueleza nia ya kutaka kumrekodi Hakimu huyo.
"Aliponieleza nia yake nikamwambia sawa, fanya hivyo kwa sababu hali ile iliendelea kumchosha mteja wangu," alisema wakili Fatuma.
Kitisho cha Babu Seya
Anasema wakiwa hotelini hapo bila Hakimu huyo kufahamu kuwa alikuwa akirekodiwa, alianza kwa kumrubuni mteja wa wakili Fatuma kwa kumshangaa anavyowalipa hela kwa watu wengine (mawakili) ambao alidai hawezi kumsaidia.
Katika kanda hiyo yenye urefu wa takribani dakika 12, Hakimu huyo pia katika mazingira mengine yenye utata, alisikika akimshawishi jamaa huyo aachane na suala la kutaka akae na mtoto wake kwani kuna athari siku atakazokuwa akikaa naye, anaweza kusingiziwa mambo kama yaliyomkuta Babu Seya.
"Hakimu yule anasikika mbali ya kudai hela akimtishia pia mteja wangu kuwa yanaweza kumkuta ya Babu Seya kama ataendelea kung'ang'ania kukaa na yule mtoto," alisema kwa uchungu wakili Fatma.
Hoi kwa wiki moja
Akizungumzia jinsi alivyostushwa na yaliyokuwa yakiendelea mara baada ya kupelekewa rekodi ile, wakili Fatuma ameliambia gazeti hili kuwa alipatwa na mshituko mkubwa.
" Nilipata 'broken heart' (jakamoyo), sijui unaweza kueleza vipi katika Kiswahili, lakini niliumwa sana na niliumia kiasi cha kushindwa hata kwenda ofisini kwa muda wa wiki moja.
"Nikajiuliza nafasi yangu ni ipi katika kusaidia suala hili?Nilijua pia kuwa hilo linaweza kunigharimu na ni msalaba mkubwa kwangu?Nikafikiria niliache,lakini nikajiuliza ni wanyonge wangapi wanalazimika kuinunua haki na nani ataibadili hali hii?
"Mimi nimefundishwa vyema sheria kule Uingereza, nayajua maadili yangu kama mwanasheria, nina moyo wa uchungu kama mwanajamii mwingine na pia hii kazi siifanyi kwa shida, ningeweza kukaa nyumbani, mume wangu akanilisha, lakini naifanya kazi hii kwa wito.
"Nilipoisikiliza ile sauti ya yule Hakimu anavyoomba rushwa kwa kujiamini, nilijua pia moyoni mwangu kuwa huu ni mtihani katika maisha yangu na haya yaliyotokea niliyawaza kabla," alisema.
Anasema rafiki yake mmoja ambaye kwa sasa ni wakili nchini Uingereza aliyekuwa hapa nchini ndiye aliyempa moyo kulisimamia kidete suala hilo na kutolinyamazia.
Kazi yaanza
Wakili Fatuma anasema baada ya kuamua kulisimamua suala hilo, alimpigia simu Hakimu husika na kumuuliza ni kwa nini alikuwa anachukua rushwa kwa mteja wake.
"Nilipoongea naye kwa simu awali tuliongea vizuri lakini nilipomgusia suala la kwa nini anachukua rushwa kutoka kwa mteja wangu na kumueleza ushahidi nilionao, alijifanya yeye si Hakimu wa Kisutu na akakata simu.
"Mteja wangu aliwasilisha malalamiko yake TAKUKURU. Nami sikukata tamaa nililifikisha suala lile tena kwa kumwekea rekodi ile aisikilize Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Kisutu, Bw. Sivangilwa Mwangesi lakini nikashangaa Hakimu yule aliendelea kusikiliza kesi yangu na nyingine za wananchi wakati uadilifu wake ulishakuwa shakani.
"Mimi tulipokutana naye Hakimu huyo (anayetuhumiwa) mahakamani nikamwomba ajitoe katika kesi yangu kwa sababu tayari uadilifu wake ulikuwa shakani na kimaadili hakupaswa kuendelea kusikiliza kesi za wananchi. Alisita lakini nikasimamia hoja yangu na hatimaye akajitoa," alisema.
Mtandao wa njama
Wakili Karume anawahakikishia watanzania kuwa hakuwa na ugomvi na Hakimu Addy Lyamuya wala Hakimu mwingine wa mahakama hiyo, lakini anasema tangu kesi hiyo ilipohamishwa kutoka Hakimu mmoja hadi mwingine alikuwa akihisi maofisa hao wa mahakama kama vile wamechukizwa na vitendo vyake vya kufuatilia mambo kwa kina.
"Sijui nini kilitokea. Sikuwahi kugombana na Mahakimu awali kwa sababu uwakili sijaanza mwaka huu wala mwaka jana. Nahisi baada ya kuona ninasimamia haki ipasavyo, walikuwa na hali fulani tofauti dhidi ya kesi yangu," alisema.
'Tume' ya Kisutu
Akizungumzia ripoti iliyotolewa juzi na Mahakama ya Kisutu kuhusu sintofahamu iliyotokea, wakili Fatuma anashangaa kuona jinsi misingi ya asili ya haki yake ya kusikilizwa ilivyokiukwa.
"Sikuitwa kujieleza na hili linashangaza, kwani hata maelezo yangu ya maandishi niliyawasilisha jana (juzi) mchana wakati ambapo kumbe tayari Hakimu Mwangesi alikuwa akiongea na waandishi akitoa ripoti ya uchunguzi wake,sidhani hata kama alisoma maelezo yangu wala kuwaita mashahidi wangu.
Juzi Hakimu Mwangesi alisema hajapokea tuhuma za rushwa dhidi ya mmoja wa mahakimu wake na jana alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu suala la kutomsikilia wakili Fatuma Karume katika uchunguzi wake, alikiri kutofanya hivyo lakini akasema alitumia maelezo ya awali ya malalamiko ya wakili huyo.
Akizungumzia hilo Fatuma ansema: "Misingi ya haki za asili inaeleza bayana kuwa lazima uitwe na kujitetea dhidi ya tuhuma zako. Hili halikufanyika lakini pia nashangaa kwa nini hata nilipotoa tuhuma za rushwa, haukufanyika uchunguzi na wala sikuitwa kutoa ushahidi zaidi."
Anasema kwa uzoefu wake akiwa wakili, sehemu kubwa ya haki za wananchi inauzwa na kuitaka jamii isimame kidete kuibua maovu zaidi yaliyoko katika idara ya mahakama kwa sababu kama haki itauzwa hakuna thamani tena ya maisha ya mwanadamu.
"Wazee wetu, Mwalimu Nyerere na babu yangu, Mzee Abeid Karume walituasa sana kuhusu rushwa. Ni heri mtu ale rushwa sehemu nyingine lakini si katika sehemu ya utoaji wa haki kama mahakamani.
"Rushwa ikishamiri katika mahakama kuna haja gani ya watu kusomea taaluma kama sheria, Ni bora kesi zikasikilizwe Jangwani ambako watu watakuwa wakiweka dau kwa kutumia fedha ili wenye nazo washinde.
"Lakini kama kuna taaluma na misingi ya sheria inayopaswa kufuatwa, basi wananchi na vyombo husika viamke. Kuna mtandao mbaya sana wa rushwa katika mahakama hasa kwa baadhi ya Mahakimu wa Kisutu," alisisitiza.
Tuhuma za wakili Fatuma Karume kuhusu rushwa katika mahakama, zimekuja wakati pia ikiwa ni miaka takribani 11 sasa tangu ripoti mashuhuri ya Jaji Warioba, ilipobainisha kuwepo kwa vitendo viongi vya rushwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Idara ya Mahakama.
Wananchi mbalimbali pia wamekuwa wakilalamikia vitendo vya kukithiri kwa rushwa katika mahakama mbalimbali hapa nchini.
Katika mahojiano yake na gazeti hili hivi karibuni, Jaji Warioba alionesha kutilia shaka kama muongo mmoja sasa, ripoti yake imefanyiwa kazi katika kuwabana wala rushwa.
Pamoja na ukweli wowowte utakaokuja kubainika lakini huyu Fatuma nae anaonekana nae ANA NYODO na ubishoo kama yule LINDA dadake Richard.
ReplyDeleteSasa kutuambia "..ningeweza kukaa nyumbani na mume wangu akanilisha..." ndio nini?
Kutukoga au?
Wacha hizo!
Huyu Fatuma Karume asitake kuwaongopea watu kuhusu kile alichokifanya pale mahakamani Kisutu. Yeye alikuwa anailazimisha mahakama isikilize kesi yake siku anayoitaka yeye.Kwa taratibu za kimahakama inaruhusiwa endapo siku hiyo mahakama itakuwa haina kesi nyingi za kusikilizwa.Kama kesi zipo nyingi mahakama hupanga tarehe itakayoona hamna kesi nyingi za kusikiliza.Huo ndio utaratibu unaofuatwa kwenye mahakama zetu.Fatuma anatafuta public sympathy-anajaribu kukwepa kitu halisi alichokifanya. Hapa kulikuw hakuna mambo ya rushwa wala nini.Na wala hakuna mtu aliyedhulumiwa haki.Ila issue ilikuwa kupanga tarehe ya kesi tu na sio vinginevyo.Pia kwa faida ya wanakijiji wasiofahamu vizuri taratibu za mahakama ni kwamba mahakama ndio inakuwa sauti ya mwisho endapo kutatokea kugongana kwa tarehe za kusikilizwa shauri kutoka pande zote mbili yaani mlalamikaji mlalamikiwa.Fatuma aache kukimbilia vyombo vya habari na kuvipa habari zisizo za kweli ili aonekane eti mahakimu wanamwonea eti kwa kuwananga wananuka rushwa.
ReplyDeleteFatma Karume is one of the best we have in our country and it is an honour to have her fight for our citizens' rights!
ReplyDeleteIt is quite obvious the magistrates who are corrupt and sell the law / rights of people want to destroy her but some of us, the CITIZENS of our beloved country are there to back her up.
All the parents of TZ are backing her up as she is fighting for the right of a parent. Imagine if anyone of you or the magistrates is deprived of her child of 2 yrs!!
Lets step into Fatma Karume's shoes before we judge anything. Plus none of us was there in court that day when this issue is supposed to have happened. Lets get all the witnesses to comment and the TLS to come to a decision about it.
GO FATMA KARUME GO, let us fight the corruption and make sure people get their RIGHTS!
Tatizo sisi watanzania tumezoea sana mteremko, ata rushwa ni vile vile kama ugali wa kila siku tu. Ukishikwa na askari, si kwa ajili ya makosa kwenye gari yako lakini ni njaa zake tuu, vile vile system yote hapo tanzania. Hii kesi ni sawasawa na ukiwa na askari wa kulinda nyumbani, ungependa huyo askari alinde nyumba yako na ulale kwa usalama au askari mpumbavu anaye lala tu na akipewa hela na wezi aanze kuwa saidia wezi namna ya kuvunja nyumba yako. Huyo dada Fatma ndiyo kiboko yao, Fatma wachape viboko hawa sawasawa na tuwaondoe ugonjwa wa cancer mahakamani.
ReplyDeleteSAFI FATMA, KOMAA NAO HAOOOOO...MIJIZI MIKUBWA, HAWAJAJENGA NYUMBA ENZI ZAO WANATAKA KUMALIZIA MABATI KWA HELA ZA DHURUMA!! UMEWAKOMESHA DADA, RUSHWA INANUKA MAHAKAMANI..
ReplyDeleteMahakimu wa Mahakama hiyo inaonekana wanchukua rushwa na wanaharibu kesi nyingi.
ReplyDeleteMaoni yangu ni kwamba kwasababu hakimu wa kwanza alipelekwa Takukuru na wengine wantaka kumkomoa Karume lakini wanamkomoa mtoto wa miaka miwili.
TUPAMBANE NA RUSHWA!
endelea tuu dada...HONGERA!
mimi ningependa kujua wadau wa sheria nchini wana hoja gani kuhusu mtafaruku alioleta Bi. Fatma mahakamani kisutu. kwasababu mi nina hakika kuna guidelines kuhusu conduct za mawakili wakiwa mahakamani. Sasa wangetueleza hizo guidelines ni zipi ili tuweze kujua kama Bi Fatma alizikiuka na kama ndivyo kwa kiwango gani na anastahili adhabu gani. Kama hajakiuka taratibu zozote basi TUMSHANGILIE tumpe BIG UP tufunge mjadala....sasa wanasheria wenyewe wamekaa kimya sisi tunabwabwaja au ndio COLLECTIVE RESPONSIBILITY?
ReplyDeleteI agree with the above comments but along with that, I would like to question the magistrate if it is allowed under any guidelines to make an action with ur hands/fingers and saying that the advocate is insane/crazy?
ReplyDeleteIf there is, then I think anything and everythin else should also be allowed in the court chambers.
If not, then what Karuma did was absolutely right to tell the Magistrate Eddy Lamyuya that she has no right to imply that Karume is crazy and that she would complain officially to the higher authorities.
I believe that this is the reason the magistrate called a press conference and falsely accused Karume as she would be in hot soup for saying Karume is crzy and to withdraw from the case for no particular reason.
Request to the owner of the blog: PLEASE ALLOW THIS REPLY TO BE POSTED AS I FEEL ITS IMPORTANT FOR PEOPLE TO KNOW!
Thanks in advance!