chunlai ilikuwa bonge la fasheni enzi hizo, pamoja na kibandiko-upande kama anvyoonesha mh. oscar kambona

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mzungu mweusi aliyeishi na wazungu...akiwa na ndoto za kumwangusha mtume wa washenzi nyerere...ah lakini ilikuwa ndoto tu...long live azimio la arusha!!!

    ReplyDelete
  2. naona wala vumbi bado wanakumbatia maazimio ya kuleteana njaa hapo,huku ni capitalism mtindo mmoja,lazima ufanye kazi ili uishi,ila wala vumbi kucheza bao na kuangalia comedy siku nzima,poleni sana,leo vipi joto limepungua au? na mbu jee
    wenu mbeba box

    ReplyDelete
  3. salama alekhum mtoa maoni wa kwanza,Hiyo statement "mtume wa washenzi " una maaana Gani" wazazi wako walio kuleta ulimwengu huu hawakukuambia umuhimu wa huyo mwanadamu alie acha kufundisha na kuunda umoja wa Tanganyika waliiopigania uhuru wa nchi hiii, leo hii unaibuka kama condactor wa daladala anae dai nauli mara 2 ????

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe Anon 12:50 PM, sisi makondakta tumekufanya nini tena? Kwani ni kipi usichoelewa?, kwamba hata makondakta ni binadamu kama wanadamu wengine kuna kusahau ama unataka kutudhalilisha tu kwa kazi zetu? Heshimu kazi za watu bwana.
    Una bahati sina hela ya kukaa neti muda mrefu, na suka analeta kelele foleni haisogei.

    Konda,
    Mbagala

    ReplyDelete
  5. Michuzi naomba nikusahihishe kiduchu. Inaitwa Chou En Lai ( au wanavyosema Wachina Zou en Lai)...si kama ulivyoandika, Chunlai. Huu mtindo wa mavazi ulisambazwa na Mwalimu Nyerere baada ya uhusiano mzuri kujengeka kati ya Tanzania ya miaka ya Sitini na Wachina, waliokuwa marafiki zetu wakubwa.
    Enzi hizo Waziri Mkuu wa China alikuwa Chou En Lai na Mwenyekiti wa Chama chao Tawala cha komunisti, Mao Tse Tung (Wachina husema, Mao Ze Dung). Hili vazi lisilo na kifuniko chake chini ya shingo (kola) liliitwa pia Ki-Mao. Na ukiweka kifuniko, liliitwa Kaunda Suti. Hiyo ilianzishwa na Rais wa Zambia, Keneth Kaunda ambaye kama Nyerere alikuwa na mtazamo wa kujitegemea. Ilikuwa jitihada kuu ya baadhi ya viongozi wetu wachache kutaka kuondokana na kuiga iga mavazi ya Kizungu. Leo masuti ya Kizungu yamerudi tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...