jk akikagua shamba lake la mananasi yaliyopandwa kwa ustadi mkubwa na kwa kuzingatia vipimo vya kitaalam huko kiwangwa bagamoyo jana katika ziara yake ya bamoyo ikiwa ni wilaya ya mwisho kutembelea kama sehemu ya ziara ya kikazi ya wiki moja ya mkoa wa pwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi mjomba uwe unasoma ulicho andika sababu makosa kidogo yanaharibu habari yote,Asante kwa kazi nzuri.(yaani edit)

    ReplyDelete
  2. Michuzi bana umezidi sana kuhusu stori za JK utadhani hii ni blogu ya Serikali????????????? Jaribu ku mix na wapinzani wengine mbona wapo wengi tuuuuuuuuuu, na sio utuwekee zitooo bali wanasiasa mbali mbali.
    Tutakuogopa sasa,ni mmoja wao nini?????

    ReplyDelete
  3. safi sana mh.mfano wa kuigwa huo,siyo kama wale waheshimiwa wanaojibidiisha kuwekeza nje ya nchi

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa bwana mkubwa wetu kwa kutukumbusha kuwa hata kama sicho kitakachotukomboa kutoka katika umasikini, kilimo kinapiga tafu walau hata kwa msosi. hakuna jambo la maana kwa binadamu yeyote kuliko msosi. Msalimiage be!

    ReplyDelete
  5. Bro we mwanahabari gani usiyejua kuandika? Yaani sentensi ndefuuu, haina kituo hata kimoja. Unatuumiza wasomaji maana hatupumui.

    ReplyDelete
  6. Pongezi kwa Mh.Rais kuonyesha nia na mfano wa kilimo cha kisasa cha mananasi.
    Mimi kama mdau wa kilimo cha mananasi ningeomba Mh. Rais atupatie jibu la soko la mananasi ndani ya TZ na soko la nje maana mazao yetu yanaozea shambani na ktk masoko yetu ya pembezonni mwa barabara.
    Je? Mh.Rais twaweza kuunganisha mzigo(mavuno) yetu ya mananasi ili tuingie ktk soko unakouzia kama ni ndani na nje ya nchi. Maana wewe Mh.Rais ndiyo jibu la kutupatia masoko ya mazao yetu.
    Na mwisho tungepewa habari kuhusu ukubwa wa shamba la Mh.Rais ili tuweze kulima shamba kubwa zaidi yake kama changamoto ya kuinuia kipato.

    Nawasilisha
    Mdau
    Kiparanganda
    Mkoani Pwani.

    ReplyDelete
  7. Jamani, ivi ukiwa kiongozi lazima unenepe, kikwete amejiachia na apa ni miaka miwili tu, akifikia kumi si takuwa kama kioski kinatembea, punguza cholestrol mzee, unatisha.

    ReplyDelete
  8. Sasa bepari,mnyonyaji,kupe nani...mbona JK analo shamba la mazao ya kibiashara? kazipata wapi hizo senti...au ni hadithi ya zamani...wakati uko ikulu maliza tuu hazina ya taifa!!!

    ReplyDelete
  9. kweli mheshimiwa ameacha mazoezi....!!!! labda muda hakuna.....sasa tusemeje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...