Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata, anaondoka leo usiku nchini akielekea Budapest, nchini Hungary ambapo atahudhuria sherehe ya kitamaduni inayojulikana kama Budapest Opera Ball.

Mwaliko wa mrembo huyu kupitia waandaji wa Miss Hungary, inalenga kujenga mahusiano ya kitamaduni kati ya Tanzania na Hungary. Flaviana Matata anatarajia kuhudhuria tafrija kubwa tarehe 2 mwezi Februari 2008 na atarejea nchini tarehe 6 Februari.

Budapest Opera Ball ni sherehe inayofanyika kila mwaka na ni tafrija yenye hadhi kubwa nchini Hungary ambapo wanasiasa, wakuu wa nchi, mabalozi na watu mashuhuri kutoka nchi ya Hungary na nchi zingine za jirani barani Ulaya hudhuria.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mrembo kutoka Afrika kuhudhuria halfa hii.
"Hii ni heshima kubwa sana kwa mtu yoyote kualikwa kwani watu wengi hulipa pesa nyingi sana kupata mwaliko wa Budapest Opera Ball. Miss Universe Tanzania inaendelea kuweka rekodi nchini na duniani", Maria Sarungi Tsehai, mkurugenzi wa kitaifa wa Miss Universe Tanzania, ameiambia globu hii sasa hivi.
Akizungumzia safari yake, Flaviana ameeleza kufurahishwa kwake na mwaliko huu " Hii ni kutokana na ukweli kwamba nchi za wenzetu wanatambua umuhimu wa warembo katika jamii. Mimi naenda pale kama balozi wa Tanzania."
Tanzania iliweka historia katika mashindano ya Miss Universe ambayo yalifanyika May 28 mwaka jana, Mexico City, huko nchini Mexico.
Flaviana Matata mwakilishi wa kwanza wa Tanzania katika mashindano aliwakilisha nchi yetu katika mashindano ya kumtafuta Miss Universe, na alifanikiwa kuingia katika kumi Bora (Top10) katika mashindano hayo akishika nafasi ya sita, ambapo yalishirikisha warembo 77 kutoka nchi mbali mbali duniani.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Compass Communications:
Tel: 2182405/ 2182596
au 0784 305122

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. michuzi kila binadamu ana uzuri wake, visichana vinavyopenda kusema sema watu waache, kila mtu ana uzuri wake.

    ReplyDelete
  2. kila mtu ana uzuri wake, wivu ni mbaya wabongo hamtaendelea all the best flaviana.

    ReplyDelete
  3. kaka michuzi alijitahidi sana sana, kati ya watu 77 alikuwa kwenye top 10, keep it up flaviana.

    ReplyDelete
  4. Rekebisha hiyo USIKU, na si USIKI

    ReplyDelete
  5. Kweli ni mzuri na anafaa lakini sasa isije kuwa kama Ruddy alivyokalia ku base tuu 9/11 wakati kuna mada nyingine pia za nguvu za kuongelea na kuonyesha.
    kaka Michu wako pia wengi wa kuongelea kuliko hapa kuliko kurudia tuuuuuuu juu ya huyu mdada.

    Watu watamchoka kama walivyochoka topic ya 9/11 mpaka Giuliani sasa amejitupia taulo mwenyewe ulingoni!
    Ni ushauri tu na hapa yeyote anaweza kutofautiana nami lakini hili nimeliona na nikafikiri kumegeana navyi kwa nia nzuri tu.

    ReplyDelete
  6. Good work naimani haijawahi tokea mrembo kualikwa na nchi nyingine,Mungu azidi kumtangulia huyu mtoto jamani afanikiwe

    ReplyDelete
  7. Eti huyu mtoto ni wa kitanga?

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Flaviana!!Kila la heri katika safari yako na tafadhali fungua macho sana,usisimame kwenye uzuri wako tu.

    ReplyDelete
  9. We Maria usituletee za kuleta hapa..kwanza why Hungary, sababu mama yako anatokea huko ? .
    Kwanza tena usituabishe kwa mara ya pili , msimvishe gauni likampwaya akawa kama anoreic hottie ,halafu je anajua kwenye Opera Ball wana vaaje, msije mvalisha jeans au hivi vigauni vyeni vya kileo vyenye kama unatokea una mimba ..lol
    I trust u Maria na ninauhakika utafanya kazi nzuri ..Hongera Flaviana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...