
mwanamuziki ali choki enzi hizo akiwa na twanga pepeta. hivi sasa amehamia tot plus 'wana achimenengule' ambayo imebadili jina na itaitwa T RESPECT PLUS. hivi tunavyoongea yuko kinshasa, kongo, kusaka timu ya madansa wanne na marapa wawili. nimeongea nae mchana huu kaniambia anasaidiwa kusaka vipaji hivyo na werrason na kwamba akirejea ni moto juu.
aidha hii inaashiria kwamba wanamuziki wa kongo wataendelea kutamba bongo kwani ukiacha kuwika sana kwa bendi za fm academia na akudo sound ambazo zina safu za wakongo ambao wamesababisha ushindani mkubwa, kuna bendi ingine ya kizalendo ambayo imeamua kuua bendi yake moja ili kuiunda upya na wanamuziki mchanganyiko toka kongo na bongo. yetu macho...
Mukubwa Choki natumaini utaokoa jahazi la uwanja wa nyumbani T RESPECT PLUS walisema tingatinga kwenye starehe limefikaje,leo upo nyumbani kwao aibu anyway uwezo unao kipaji unacho fanya kazi dont listen gossip!Reunion,Namalowe na Europe..
ReplyDeletehuko koote anazungukaa wee lakini mwisho wa siku anarudi twangapepeta
ReplyDeletetulishawazoea, tena wakienda kwenye bendi nyingine nje ya twanga wanapoteza umaarufu kabisa hata hawasikiki,tunakuombea urudi salama baba pale twanga maana pale panaitwa mtakuja tu