KIONGOZI wa Upinzani Bungeni, Mh. Hamad Rashid Mohamedi, ametangaza Baraza la Mawaziri Kivuli linalojumuisha wabunge wa upinzani.
Aliwataja mawaziri vivuli kwamba, yeye ataongoza Wizara ya Mipango na Fedha, akisaidiwa na Mh. Fatma Fereji.
Waziri Kivuli wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Mh. Dk Willibrod Slaa, naibu wake Mh. Ania Chaurembo, wakati Sera, Uratibu na Bunge unashikwa na Mh. Halima Mdee.
Mh. Shoka Khamis Juma anakuwa Waziri Kivuli wa Nchi, Utawala Bora na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ni Mh. Grace Kiwelu.
Wengine Waziri Kivuli wa Muungano ni Mh. Riziki Omar Juma, Waziri wa Mazingira, Mh. Chacha Wangwe, Afya ni Mh. Dk Ali Tarab Ali na naibu wake ni Mh. Omar Ali Mzee, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni Mh. John Cheyo akisaidiwa na Mh. Ali Said Salim.
Waziri Kivuli Elimu na Mafunzo ya Ufund ni Mh. Susan Lyimo, Naibu wake atakuwa Mh. Nuru Awadh Bafadhil na Waziri Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Said Amour Arfi.
Mh. Zitto Kabwe ataongoza Wizara ya Miundombinu na atasaidiwa na Mh. Bakari Shamis Faki, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ni Mh. Mwanawetu Zarafi na Naibu wake ni Mohamed Ali Said na wakati Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Mh. Salim Abdulla Khalfani.
Mh. Mhonga Ruhwanya, amepewa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Naibu wake, Mh. Mkiwa Adam Kiwanga, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeenda kwa Mh. Salim Hemed Khamis akisaidiwa na Mh. Juma Said Omar.
Waziri Kivuli Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto itakuwa chini ya Mh. Maulidah Anna Komu, wakati Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itaongozwa na Mh. Mwadini Abbas Jecha na Naibu wake ni Mh. Ali Khamis Seif.
Waziri Kivuli Maliasili na Utalii, Mh. Magdalena Sakaya, Mambo ya Ndani, Mh. Mohamed Ibrahim Sanya, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Khalifa S Khalifa, Nishati na Madini, Mh. Mohamed Habib Mnyaa, naibu wake na Mh. Savelina Mwijagwe.
Wengine ni Waziri Kivuli Katiba na Sheria, Mh. Fatma Maghimbi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh. Masoud Abdulla Salim, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh. Abuubakary Khamis Bakari, Viwanda, Biashara na Masoko, Mh. Lucy Owenya akisaidiwa na Mh. Khadija Salum Alli.
Loooh! Hawa kweli ni mawaziri vivuli. Tunaomba tuone CV zao! Hawa ndiyo wapiga kelele wa serikali ya JK wanawataka. I wish wengepewa nafasi ya kuongoza nchi kwa mwaka mmoja tuone! JK fanya kazi yako kwa kufungua ukurasa mpya, umepata timu nzuri ya mchanganyiko wa vijana, middle age and wazee na wasomi wa uhakika. KEEP IT UP! Tupo nyuma yako tunakusupport!
ReplyDeleteUtafikiri Tanzania upinzani ni wa Waislamu - majina mengi ya "mawaziri vivuli"!!!!!!!!
ReplyDeleteBro Michu, tunaomba utuwekee list ya Wabunge wa upinzani hapa. Kama sikosei wako 40, na wengi wao wanatoka Pemba! Kuna mbunge wa upinzania aliyekosa uwaziri hapo?
ReplyDeleteMichu mi naomba CV za Mh.mbunge Mkiwa adamu Kimwanga, Pleeeeezz
ReplyDeleteHeeee waislamu tuuuu lol not fare!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete