


Viongozi na wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi kupitia Shina la Islington, jijini London, Uingereza, wakisherehekea kuzinduliwa kwa shina lao.
Shina hilo jipya la Chama Cha Mapinduzi jijini London, Uingereza lilizinduliwa rasmi tarehe 1 Machi 2008.
Shamra shamra za uzinduzi ziliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM London Ndugu Maina Owino na Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee. Mgeni rasmi wa katika tukio hilo la kihistoria alikuwa Mhe Martha Mlata (MB - Viti Maalumu, Singida).
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ahsante.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ahsante.
Wako Katika Ujenzi wa Taifa
Soames Phares
Reading
United Kingdom
hiki chama kina ajenda za siri siyo bure.Sielewi mantiki ya kuweka shina hapo. ooh ok! nilisahau wabeba mabox wanajihami wakirudi wameuwawa wakaponee kwenye mashina ya ccm bongo
ReplyDeletemdau
Pure comedy!
ReplyDeleteWEWE HUJUI SIO BONGO WANAKULA HUKU HUKU YAANI KWELI KWELI DUNIA HII
ReplyDeleteWow kwa hiyo kila mtaa London utakua na shina la ccm london? Hii babu kubwa....shina linahitajika kuwa na wajumbe wangapi kuwa qualified. manake bila hivyo yatakuwa mengi tu sasa
ReplyDeletemlikutana wapi hapo jamani?panaonekana kirabuni hapo!!!
ReplyDeleteCCM itaishia kufungua matawi huko huko United Kingdom, sidhani kama mtu anayekaa USA au Canada anaweza kukubali ujinga kama huu. Kweli elimu si ufunguo wa upeo na uelewa kwa baadhi ya watu.
ReplyDeleteWote wazushi tuu
ReplyDeleteOwino, kwa jinsi ninavyokufahamu hapa lazma unapiga hesabu kali.
ReplyDeleteCCm Oyeeeeeeeeeee !! iena iena iena iena iena iena CCM ni nambari wani eeeh !!
ReplyDelete(duh sijui wimbo nimepatia)!! anyway we anony said wa hapo juu mtajiju wenye chuki kunyweni klorokwini zikulaze milele, hata tukifungua mashina 100 nje ya nchi so what ?wewe kinakukereketa nini haswa? si na wewe ufungue ? umekatazwa ? its a free country !! na kwanza nani umeambiwa watu ulaya wanabeba maboksi tu ?? kwa taarifa yako hiyo ni means to an end na siku hizi fasheni kubeba maboksi na kupata kitabu kinoma hata watu wazima walio ulaya wanaamka!! wabongo wanaamka na hilo nawasifu !sisi hatuna mpango wa kukaa hapa ulaya milele tunataka kurudi kwetu na kama ujuavyo bongo hakuna maboksi kule so we endeleza tu chuki binafsi utajua hapo fainali uzeeni itakapokukumba!watu wengi wanaopendaga kukosoa wenzao ni kwamba wana viroho korosho na huwa hawaendelei!! we huoni Nondozz zinavyotangazika katika blogu yetuu hii ?? sasa kwa nini sie wa UK tubaki nyuma ?? kalaga baho !!KWa taarifa yako sisi tutabeba maboksi na by the time tunarudi bongo hayo mashina ya CCM tutakuachia mtu kam wewe hivyo mana sie ngoma yetu itakuwa too big for dat!! hater !! sisi twasonga mbele na mabox yetu na Chama chetu nawe utachonga sana juu yetu but it does not matter coz u just a hater !! ......CCM Oyeeeeeeee!! iena iena ienaaa iena na tuendeleze LIBENEKE hiloooooo !!
Inasikitisha kuona watu licha ya kwamba wamebahatika kutoka nje ya nchi lakini wanakumabatia CCM. Hii ni jinsi gani inavyoonyesha CCM inajichanganya katiaka kuupotesha umma wa watanzania. Sielewi au ianbidi nieelezwe zaidi ni9 nani inabidi alete mabadili bongo kama si watu walioko nje ya nchi kuliko kuiabudu CCM. Kwa hilo nawanyooshea mikono Wazanzibari. Kwasabaubu wanaweza kueleza ukweli wa mambo. Tulio nje ya nchi ni lazma sasa tuache kuikumbatia CCM na tuueleze umma wa watanzania ukweli wa mambo. nafikiri wengi wetu hatujaletwa na CCM
ReplyDeleteWANATAKA WALE PALAINI MABOX YAPO KIBAO UKO CCM YANINI?
ReplyDeleteKweli siasa ina mambo, yaani watu wameona wenzao wanapata vyeo na kufaidi matunda ya ufisadi basi kila mtu anataka kuwa fisadi.
ReplyDeleteAu watu bado wanafikra za chama kimoja, kwamba ili upate kazi inabidi uoneshe kadi cha Chama Cha Mafisadi?
Lakini angalieni, wananchi wamechoka siasa, wananchi wanataka vyama vya kuleta maendeleo siyo risala majukwaani. Kwa hiyo ndugu zanguni nawashauri badala ya kuanzisha shina la CCM anzisheni SACCOS ndiyo tunayoimind huku bongo. Lakini mtu yeyote anayeleta mambo ya ufisadi tutamfuata huko aliko!
Ole wenu, ole wenu, ufisadi siku zake zimefikia mwisho!
Nadhani mtu aliyepost comment kwamba watanzania walio Marekani au Canada hawaelekei kufanya "ujinga" wa kufungua matawi ya CCM huko yuko sahihi. Si kwamba walioko Marekani wana akili zaidi, ila nadhani wamefuguka akili na wana uchungu wa kweli na nchi yao. Ni wazi baadhi ya watanzania wakijiunga na "kufungua tawi" mtaa fulani Uingereza, wana lengo tu la "kufanya ufisadi" huko mbeleni. Hiyo ni wazi. Inatia aina fulani ya kichefuchefu kuona watanzania nje ya nchi tena kwenye nchi yenye jina, wakiwa wamevalia kijani ya CCM. Aibu!! Endelea kuwawekea picha zao kwenye blog yako Michuzi lakini wanajichora, japo inawezekana kweli malengo yao yakatimia
ReplyDeleteHivi ni kweli watu wamechoka chama au watendaji? Tatizo la nchi yetu siyo chama gani ila watanzania hatuna malengo mmoja mmoja na kama nchi. Hii haijionyeshi tu kwenye CCM bali katika vyama vyote vya siasa, ofisi za serikali, vyuo vyetu vikuu na sehemu nyingine kibao. Utakuta mtu anatoa maelezo kibao kuhusu kufikia malengo fulani lakini ukimuiliza atafanyaje ili afikie malengo atakwambia anasubiri serikali ilete msaada, wafadhili watusaidie n.K. Hapa watu wanataka maisha bora bila kutoka jasho kwanza halafu wanawapaka matope wenzao waliofanikiwa kwamba ni mafisadi. Wabongo tubadilike, hata wakija CHADEMA, CUF, TLP (hiki siyo chama ila ni kampuni binafsi ya Mrema)hakuna jipya, lazima wenyewe tuwe na malengo na njia za kuyafikia hayo malengo. Tukiwa hivyo itakuwa rahisi kuwabana viongozi wetu badala ya kubaki kulaumu kila kitu. Watu wa vyama vya siasa na NGO's kulalamika ni kazi yao kwa sababu wanalipwa ili wafanye hivyo (wanapata ruzuku za wafadhili) bila hivyo hawapati pesa. Tusiwe watu wa kudandia hoja
ReplyDeleteHAYA TENA USHAHILI NA USHAMBA NDANI YAKE ETI CCM MPAKA MAMTONIIIIII.JAMANIII HAMUONI HATA AIBU KWANZA WENGI WENU NI KINA SHAHANGA,MNATOKE UBAJUNI.NCHI YENU MMESHAIKANA CCM YA NINI TENA HAO WOTE UKIANGALIA NI WABAJUNI,WATUSII,WASUDAN,WENGINE KESI YA KUKEKETWA,CCM CCM RUDINI HOME KWETU MNATUCHAFURIA TU MIJIIIII YETU ULISHA ONA WAPI HUKU MTU ANAJITOA AKILI NA MAMBO YA CHAMA
ReplyDeleteNyie kweli CCM,sisi huku bongo tunapapambana na U-richmond nyie mnafungua matawi ya chama kilekile kilicholea mafisadi.
ReplyDeleteCCM ni chama cha mapinduzi kweli. Ukiangalia sana namna kilimo biashara,viwanda na maeneo mengi kiuchumi tunavyorudi kulinganisha na nchi nyingine tulizopata nazo uhuru,nakiri kwamba haya ni mapinduzi ya kileo na tunacho chama kinachosimamia haya mapinduzi. Kinaitwa chama cha mapinduzi! Kama unajua ni mafanikio gani unayoyapata wewe na jamii yako yanayokufanya useme kwamba CCM si chama cha mapinduzi niliyofikiria mie tuambiane. Maana uhuru na amani walileta TANU. Uzalendo ushapinduliwa hamna tena,umoja ndio huo unafifia,elimu,afya ndio usiseme. Au ndio Chukua Ch... Map...? wanayomaanisha CCM ni m
ReplyDeleteKweli kabisa haya mambo ni ya washamba wa huko huko UK.Upuuzi huu huwezi kuukuta hapa US au Canada..Viwanja vya kueleweka hivi
ReplyDeleteBig Up kwa wale waliotoa maoni ya kujenga hapo juu...ni kwa masikitiko makubwa maoni mengi ni ya kejeli na dharau. Watanzania wengi pamoja kwamba wako nje ya nchi lakini hawajui umuhimu wa kusimama na kuhesabiwa. Haijalishi wewe unaunga mkono sera za CCM, CUF, Chadema au TLP, au hukubaliana na Chama chocote cha siasa Tanzania; kama hauhesabiwi wewe nani na unasimia nini basi tatizo lipo kwako na sio kwa wale wanaoendesha vyama moja kwa moja au wanaokubaliana na sera za hivyo vyama.
ReplyDeleteWengi hapa wanasema wanataka mabadiliko, lakini wakati huo huo wanataka MABADILIKO hayo yaletwe na MALAIKA...wanaona aibu kuunga mkono CCM, Chadema, TLP, CUF etc. Hawataki kusimama na kuhesabiwa katika siasa yetu, lakini wanataka mabadiliko yatokee katika siasa hiyo hiyo..!! Ni rahisi sana kuwa USA, UK, Canada n.k na kusema CCM chama kibaya, lakini kumbuka CCM hii hii mnayoiona mbaya ndio ilimeshinda uchaguzi kwa 80% (iwe kihalali au vinginevyo; mna uhur wa maoni) Miezi na miaka itakuja na kupita, watakaokuwepo watangamua nani alikuwa Mshamba kati ya wale waliosisima na CCM, Chadema, CUF n.k na kuhesabika au wale waliopoteza muda kwenye blog kuwabeza waliosimama.
Tanzania ni nchi yetu wote, tupo hapa tulipo kwa sababu siasa yetu ina walakini. Siasa yetu inatugharimu kwenye Elimu, Ajira, Miundo Mbinu, Kilimo, Afya n.k. Sasa, iwapo kama bado mnaona maneno yenu ya kusema CCM ni Chama cha Mafisadi yatawaletea mabadiliko mnayoyataka nawatakieni Kila la Kheri.
Hongera CCM kwa kufungua Shina Islington, London...endeleeni na mwendo huo huo. Ni matumaini yangu kuwa ikitokea siku Mbeba Box (joke..) aliyesota na kujisomesha mwenyewe UK akafanikiwa na kuwa kiongozi wa nchi yetu atakuwa na nafasi ya kufanya maendeleo mengi kwa nithamu za uongozi aliyojifunza Ulaya.
Njaa kali....Hii nini sasa???????
ReplyDeleteLondon ni kama bongo tu...naona london inalemewa na wahamiaji...ndio maana hata kuna waarabu wanatka sheria law iwe halali hapo london....
ReplyDeleteCCM london????? Njooni USA muone kama mtapata hata mmoja mjinga wakujiunga na nyie. Mafisadi bwana wana muda mrefu...wanaandaana hata wakiwa nje ya nchi..Wakirudi bongo resume tosha nilikua mwenyekiti wa shina la CCM london....wakati mwenyekiti wa shina la hapo hapo bongo atapigwa mkumbo...
Maina Owino tumesoma naye SHYCOM namfahamu hapo ana mahesabu makali ambapo wenzake labda hawamjui. You better be careful with that GUY. Anajitafutia umaarufu. Tulipoanza SHYCOM alilaghai wasicha kuwa ana mpango wa kwenda kutoa lbamu ya muziki wa injili huko Nairobi hivyo waungane naye kwenda Nairobi, akaishia kumdanganya msichana mmoja (jina tunalihifadhi). Mwangalieni sana huyo jamaa, mnachofanya ni ujinga mtupu na kweli kuelimika sio kwenda shule tu.
ReplyDeleteWabongo kwa mambo ya ushabiki hatujambo. Sasa hii itawasaidia nini? Hata kupiga kura hawawezi? Tatizo wabongo wengi wanadhani ili ufanikiwe kimaisha lazima uwe mwanasiasa. Maana huko ndio unaweza kuiba na kufanya ufisadi.
ReplyDeleteWenzetu wahindi wako pale mjini wanapiga mambo ya biashara na wala hawana habari na upuuzi wa siasa. Matokeo yake wahindi ndio wafanyabiashara wakubwa sana Tanzania. Wao wana win hapo hapo Bongo na wala huwaoni wakikimbilia nje ya nchi kubeba box.
I find it hard to believe watu wenye akili timamu wamekuja na idea ya kufungua tawi la CCM London. Na pia kuna some fools wananunua kadi! What a shame!
SAC
Chonde chonde haya matawi mnayofungua nje ya nchi msije mkawa mnatumia hela za walipa kodi kuyaendesha tutafika pabaya.kwanza nini ajenda yenu au ndio mafisadi wa baadae.huo ni unafiki tu kujifanya hamna kazi za maana huko kuanzisha matawi ya ccm na njaa zitawaua nyie kwanini msianzishe mfuko wa kusaidia watoto yatima na wenye magonjwa na mkaleta hio misaada huku nyumbani mnaenda kufungua mishina sijui tawi la ccm london.mnaonekana vituko tuu na njaa hizo zitawapeleka pabaya mnadanganyana sana kwamba mtapewa vyeo.mko nje saidieni matatizo yanyumba kwa kutuma misaada sio nyinyi mnaanza kutolea macho hela hiliyo kuwa nyumbani. Sasa kama kuna mmoja wenu anasoma haya maoni tunawaomba mtuwekee wazi ajenda yenu au majukumu na malengo ya tawi lenu tuyaangalia tutaweza kujua lengo lenu nini.
ReplyDeleteWewe wa 10:52 pm march 8th...hujasikia watu wanaitwa independent????? Watu hao hawahusudu mambo ya vyama bali wanaangalia ni kiongozi gani ana sera za kweli...Na Tanzania itabidi waamke wakubali watu wapige kura bila ya kuwa na chama...
ReplyDeleteHii itasaidia watu wanaojikomba kuacha kuteseka.
Vyama ni kama cult tu ila kiongozi ndio antakiwa kujulikana vizuri kabla hajawekwa kwenye uongozi .
Sio watu wanakua na maneno meeeengi kabla hawajapewa uongozi baada ya hapo kila kitu wamesahau....Inabidi wajifunze kuwapa watu kura kwa jinsi wanavyo mjudge mtu individual na sio chama chake. na pia kam kwenye bunge wakifanya vyama vyote viwe bungeni vitasaidia mambo ya kijinga jinga kutopitishwa.....
Mbona mie naishi UK sijasikia hayo matawi ya CCM? Ndio kwanza nasoma humu kwa bwana michuzi, sikujua kuna CCM huku. Mie huku vijijini/miji midogo (kwa wazungu waingereza asilia) ni sawa na mwisho wa dunia jamani. Nimejitahidi kwa miaka mingi sana kuitangaza kata ya Nkokoto (Tanzania) hapa mjini. Nashukuru mungu waingereza wameonyesha sana moyo. Hivi sasa mji wetu wa Minchinhapton umekuwa officially link with Nkokoto. Wakazi wote hapa mjini wametoa misada ya hali na mali na wengi wao wamekuwa wakijitolea kwenda huko kijijini/kata ya Nkokoto (mkoani Tabora) kusaidia kusimamia ujenzi wa shule, kanisa, visima, zahanati, vitabu, vyerehani, mashine za mafundi seremala, etc. Hivyo mambo ya CCM huku hakuna, kwani CCM imeshindwa kuinua maisha ya wananchi hasa wale walioko vijijini Tanzania kama hicho cha Nkokoto ambacho kimekuja kukombolewa na wanananchi wa kawaida wa kingereza wakati mafisadi yako hapo hapo Tanzania yanashiba matumbo, iweje leo nihangaike na CCM?
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania na watu wake.
kwa habari zaidi bofya hapa
http://en.wikipedia.org/wiki/Minchinhampton
pia bofya hapa kuona fundraising ajili ya NKOKOTO, iko katikati ya page
http://community.stroud.gov.uk/general.asp?pid=5&pgid=145
Mama Chantelle
Minchinhapton-UK
[b]Mdau ulituma maoni yaoni yako: Tarehe Sunday, March 9, 2008 6:45:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous [/b]
ReplyDelete[b]
Kwenye paragraph yako ya kwanza UMERUDIA tena maono ya wengi humu kwenye blogu, nanukuu “Na Tanzania itabidi waamke wakubali watu wapige kura bila ya kuwa na chama...” Naomba nikuulize unaposema Tanzania, unamaanisha nini..??!! Nimesema hapo juu kuwa Tanzania ni yetu wote uwe popote pale ulipo kama damu yako au Utaifa wako ni Tanzania, basi ni muhimu usimame utekeleze majukumu yako kama Mtanzania kwa faida ya Tanzania. Hawa waliofungua Shina la CCM Islington, London wao kwa nafasi zao ndio wameona uwezo na jitihada zao utazaa matunda kwenye Siasa, kupitia CCM.
Umeendelea kusema , nanukuu “Inabidi wajifunze kuwapa watu kura kwa jinsi wanavyo mjudge mtu individual na sio chama chake.” Hapa tena ni makosa yale yale, mnasahau nguvu ya Siasa kwenye haya MABADILIKO mnayoyataka...Kwa kuangalia Mfumo wa Siasa yetu ulivyo leo, ukimpigia Mtu unayemuamini ni muadilifu na kiongozi mzuri, huyu kiongozi mzuri ni lazima asimame kupitia chama Fulani ndio watanzania waweze kumchagua kwa kupigia kura; pindi akiwa kiongozi utakuwa ni wajibu wake kutekeleza sera za Chama chakea. Hapo unaonekana kana kwamba utategemea huyu kiongozi aje kutekeleza sera zake binafsi kwa sababu ni muadilifi..!! Again, mabadiliko wote tunataka lakini, je ni wangapi wanaojitolea kufanya lile wawezalo? Wengi wamebakia kulaumu na kuthihaki.
Mwisho, “na pia kam kwenye bunge wakifanya vyama vyote viwe bungeni vitasaidia mambo ya kijinga jinga kutopitishwa.....” Labda nikuulize, unataka hao wabunge wa vyama vingine wafikaje huko bungeni, iwapo CCM (chama kiongozi) wanafungua matawi mpaka nchi za nje na wewe kama shabiki/mwanachama/mpenda sera za vyama vingine unatumia muda wako kukosoa tu badala ya kusimama na kufanya liwe uwezalo. Sio lazima iwe siasa, kwani siasa siyo ya kila mtu lakini kama siasa huwezi waachie wanaoiweza. Ila kuwa makini ukiawaachia wengine wacheze na siasa ya nchi yako kwa sababu moja au nyingine au tu kwa sababu ya uvivu wa kufikiri, iko siku hao wanasiasa wanaweza kuja kukumbia wewe sio Mtanzania, ukaishia kulaumu kwenye blogu. Kila la kheri, stand up and be counted...Tanzania ni yetu sote. [/b]
MIMI PONGEZI ZANGU ZOTE ZINAENDA KWA MAMA CHANTELLE HAPO JUU WA MINCHINHAPTON-UK SIO HIO MIZEE MIZIMA INAENDEKEZA NJAA KUANZA KUJIPENDEKEZA CCM.KAMA UNAUCHUNGU NA TANZANIA FANYA KAMA MAMA CHANTELLE YEYE KAFANYA KWA MOYO WA KUSAIDIA NYUMBANI SIO NYIE MNAKIMBILIA KUFUNGUA MASHINA HILI MPATE NJIA YA KUFANYA UFISADI.VITUKOO WOTE NA MNACHEKESHA KWENYE JAMII NA TUTAWAFUATILIA KUJUA MATAWI NA maSHINA yENU ZA CCM MNAZIENDELEZAJE?. Chama Cha Mafisadi Tawi la london
ReplyDeleteMAMA CHANTELLE NIMEONA LINK HONGERA SAAAAAAANA UNAFANYA KAZI NZURI SIO MAFISADI ASWA HUYO DADA KWENYE JACKET NYEUSI SIJUI NDIO MWENYEKITI WAO UMEMUONA ANAVYO JISHEBEDUA KWENYE PICHA ZAKE.YAANI ANAJIFANYA YUKO VERY CLOSE NA MAMA MAAJAR KULIKO HATA WATOTO WA MAMA BALOZI
ReplyDeleteTarehe Monday, March 10, 2008 12:08:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteSasa wewe hapo juu, muda huo wa kuwafuatilia ili kujua iwapo hayo Mashina yanatekeleza malengo yaliyowekwa, si bora bora ungejiunga nao tu..!! Ili kama ni kufuatilia ufuatilie kikamilifu ukiwa na sauti ndani ya hayo Mashina?
Mama Chantelle hongera kwa kufanya Nkokoto ipate misaada hiyo. Wewe ni mfano mzuri wa wale wanaosimama pale walipo kwa uwezo wao na kutafuta misaada. Hongera sana, changamoto kwa wengine humu; sio lazima muwe wanaSiasa, fanyeni kila uwezalo pale mlipo kama mmoja mmoja au vikundi badala ya kuja na kukejeli wenzenu humu kwenye blogu.
Ni wanasiasa waadilifu pamoja na Watanzania wengine wengi wenye moyo kama Mama Chantelle (wengine nikimaaniisha kwenye fani na uwezo tofauti) popote pale walipo ndio wataokomboa Tanzania.
Wanaofikiri kukejeli ndiko kutamaliza Ufisadi kwenye nchi yetu, bado wamelala usingizi mzito.
Pongezi kwako Mama Chantelle, kazi nzuri hiyo. Ningekushauri ujiunge na wana CCM huko UK ili wakuongezee nguvu; umoja ni nguvu siku zote. Hasa kama kuna mambo ambayo huku nyumbani yanakusumbua, hao Ccm ndio chama tawala na wana ofisi yapo UK watumie ipasavyo; wasipokupa ushirikiano wewe lete habari hapa kwenye blogu ya Mhe Michuzi au www.jamboforums.com tuwape vipande vyao.
ReplyDeleteWatanzania wa UK mnanishangaza sana, yaani ninyi ccm imewafungulia ofisi hapo badala ya kuwakaba roho wawatumikie ipasavyo mnakuja kuwatukana kwenye internet. Kwa taarifa yenu hiyo ndio siasa ya Tz, hata JK mwenyewe kama akija UK akishamuona Balozi mtu mwingine atakayemuona ni Mwenyekiti wa CCM UK, huo ndio ukweli. Shauri yenu endeleeni kubwabwaja humu.
Hakuna kulala wakabeni wawatumikie hao mpaka kieleweke.
wewe uliyeimba iena iena ccm nambari wani, unatakiwa urudi bongo ukapimwe akili, au upungwe dogori. Huna akili kabisa wewe
ReplyDeleteNyinyi mnaokaa marekani acheni vidomodomo. Chemi Chemponda anakaa marekani na alikuwepo kwenye ufunguzi wa hilo china hapo juu na yeye ndiye mweka hazina wetu wa hilo shina. Hata kama hatutofungua shina au tawi marekani lakini wakereketwa wengi wa CCM wanaoishi marekani bado wanajihusisha na chama chetu tawala. Hongera dada Chemi kwa mchango wako. Karibu tena London.
ReplyDeleteHuyu jamaa wa hapo juu anayemuomba mama chantelle ajiunge na ccm wewe ni kundi moja wa hilo shina la ccm na sasa unaona aibu huyu mama peke yake kafanya mengi kuliko kundi lenu ambalo njaa inawasumbua kiasi cha kwamba mnajipendekeza kwa ccm .ajiunge na nyinyi hili mumuingize kwenye ufisadi? Eti jakaya akija uk anaenda kuonana na mwenyekiti wa ccm? Who give a fcuk about the person jk visits in abroad if its not for any benefit of the poor tanzanians strugling to survive just because the goverment doesn't have money to provide medicines,clean water ,good studying enviroments for our kids but they have 133 billions to disapear without them saying a word and millions to pay bogus companies that doesn't exist? .hao wanaojifanya wana ccm london ni wanafiki wakubwa .
ReplyDeleteHamruhusiwi kuanzisha vyama vya siasa ktk nchi hiyo!
ReplyDeleteWEWE....Tarehe Monday, March 10, 2008 7:45:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous.
ReplyDeleteUkiona Chama au Serikali YOYOTE duniani wanachukua $ 133 Milions na kuziweka kwenye matumbo yao....bila wananchi kuandamana, wafanyakazi kugoma, bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali, rais kutokujiuzulu au hata kulazimika kuhutubia bunge, polisi haijakama mtuhumiwa yoyote...n.k UKIONA YOTE HAYA YANATOKEA KATIKA NCHI HIYO. HEBU TAFAKARI NA USIWE MVIVU WA KUFIKIRI. JIULIZE KAMA TATIZAO NI VIONGOZI AU HAO WALIOWACHAGUA!!
Inaonekana baadhi ya Wabongo wengi hapa wanaotoa maoni, wana degree za Unafiki, Umbea na Viroho papo,nipeni link basi niapply kwenye hivyo vyuo mlivyosomea ili nami nikasomee hizo degree. Cuf Chadema,nccr - Mageuzi, kifupi CCM, hivyo sioni tofauti yeyote. Nasubiri maoni mengine najua yanakuja tu,tena yenye pumba sana ili nicheke - Kwi! kwi! kwii! Ni mimi Harufu Mbaya
ReplyDeletenasikia jk alifungua tawi la ccm huko london, aibu tupu, sasa jk anamaanisha hawa jamaa ni wakimbizi wa nchi gani? uhamiaji wa huko walipata kibali kupitia zile pesa walizoibiwa wananchi au vipi? ninachofurahi wabongo kwenye blogu hii wanashangaa na upuuzi wa ccm. uwanja wa mpira wa ccm,nyumba za wananchi kwa mfano bunge la zamani limekuwa la ccm, RTD ni ya ccm sasa kweli kitu gani bongo sio cha ccm ? hapo ndio mtajua nyerere alikuwa jambazi kama vile banda,mobutu,barre,bokassa,bongo,moi,biya n.k.
ReplyDeleteHao Watanzania wa Uingereza wanaosema idumu CCM hawaitakii nchi yetu mema. Watasemaje kidumu chama ambacho kimefuga mafisadi wanaoangamiza nchi namna hii? Aibu tupu. Watanzania wa Marekani na Canada msikubali kujidhalilisha kama hao wa Uingereza. Lindeni heshima ya Tanzania.
ReplyDeleteWatanzania wa Marekani na Canada, mna Uraia wa Nchi Mbili ama? sijaelewa bado! au unamaanisha Watanzania wanaoishi Marekani na Canada. Sijaelewa kabisa, naomba unifafanulie kuhusu "msikubali kujidhalilisha kama hao wa Uingereza" na ni nini maana halisi ya "lindeni heshima ya Tanzania" Nilishaomba tangu mwanzo mnitumie hizo link za vyuo vyenu - degree za Unafiki, Umbea na Viroho papo,nipeni link basi niapply kwenye hivyo vyuo mlivyosomea ili nami nikasomee hizo degree. Nasubiri maoni mengine najua yanakuja tu,tena yenye pumba nyingi ili nicheke - Kwi! kwi! kwii! Wewe uliyetuma maoni - Tuesday, March 11, 2008 5:25:00 PM EAT, una level gani katika hizo degree zilizotajwa? naona unashusha pumba za nguvu. Ni mimi "Harufu Mbaya"
ReplyDeleteDuh, hii kweli kali; Kulinda heshima ya Tanzania kwa kuona aibu kujihusisha na juhudi za kuikomboa Tanzania kisiasa..!!!
ReplyDeleteMimi na ujinga wangu nilifikiri mkiwa huko nje ya nchi iwe Uingereza au Ujerumani au Marekani kitu muhimu kuliko vyote kwenu nyote ni UTAIFA wenu kwanza!Mkianza kujibagua kwa misingi ya vyama vya siasa na nyie mko ugenini itakuwaje?Haijatulia hiyo.Mngekua na akili sana la kwanza kabisa ambalo mlipaswa kulipigania ni haki ya watanzania wote waishio nje ya nchi wawe na haki na pia washiriki kupiga kura katika kila uchaguzi mkuu ili kumchagua Rais wao kama nchi za wenzetu zinavyo fanya.Kwenu nyie la maana zaidi mmeona ni kufungua matawi ya CCM katika nchi za ugenini.Waingereza watawaelewaje?Na Watanzania wenzenu wa vyamavingine vya siasa watamichukuliaje mkitambua kwamba CCM ndicho kinacho tawala hivi sasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa?Mtakapo kuja takiwa mshiriki kupiga kura ya kumchagua Rais katika uchaguzi mkuu mtapiga kura kwasababu ni raia wa Tanzania lakini siyo kwa sababu ya uanachama wenu katika CCM!Nchi yetu bado haijakomaa katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa.Nyie mlioko huko nje ndio tuliowategemea sana kwamba mtatusaidia katika kuboresha demokrasia hiyo.Rushwa na Ufisadi uliokithiri hapa nchini umetokana zaidi na Ukiritimba wa kutawaliwa na Chama Kimoja cha siasa kwa zaidi ya miaka 40 bila ya kuwepo na CHECKS & BALANCES zozote kutoka katika vyama vingine vya siasa ambavyo bado vichanga na vitahitji msaada wenu.Sasa mkianza huo ulimbukeni wa kuanzisha matawi ya vyama vya siasa huko ugenini,lini mtapata wasaa wa kuketi pamoja kama watanzania mkazungumzia shida za huku nyumbani na jinsi ya kuzitatua?Hata nyie wasomi mmeingizwa mkenge katika hilo?Kwa kweli imenisikitisha sana.Wenzetu huko mmetutupa mkono,mnachofikiria ni matumbo yenu tu pindi mtakaporejea huku nyumbani na kunyakua uongozi katika nafasi za CCM kwa kivuli hicho cha Uingereza na kuendeleza Ufisadi!Poleni sana.
ReplyDeleteJamani hii sasa ni kali kuliko hayo yote ni matatizo ya njaa,nimezoea kuona watu wasio na kazi yaani walala hoi wakiwa ndio wanaokaa kwenye matawi ya ccm kila siku utawakuta wanacheza bao kama si karata sasa na hao wa huko nje nao wanafanya hivyo?.Na je huyo aliyeenda huko mlala hoi hiyo nauli alipata wapi au ndio wale wazamiaji?
ReplyDelete